Hotuba Ya JK: Tafsiri Yangu

Doooh!
Majjid kuna mengi umenena na sijakubaliana nayo.
Kwamba JK ametumia busara, sidhani kama uko sahihi - Shinikizo ni kubwa kwa sasa (watu wana mwamko).
Kwamba JK si mwendawazimu, labda uko sahihi - ila mbona alikuwa anaongea kimajungu sana juu ya watu wanaotaka kusababisha vurugu? kama rais wa nchi amewashindwa wafanya vurugu nani atawaweza? (hapo namaanisha kuwa mleta vurugu namba moja ni yeye)
Kwamba JK amefocus miaka 50 ijayo, si kweli - Angeanza na kuisafisha system

I have a strong feeling of Hatred towards my President.. Yes, i said so!
 
I believe rais anapata ushauri kutoka sehemu nyingi ambao sometimes is confusing but kwa kusikiliza kilio cha watanzania kuhusu katiba nampa credit. Anayesema CDM ndo walianzisha movement ya katiba huo ni uongo maana nakumbuka mtikila ashawahi hadi kulipandisha mahakamani hili swala. Just tuwe wa kweli kwamba now hili swala limepata mwamko mkubwa kutoka kwa wananchi ndo maana limepita.
Mkisema rais anafanya kazi kwa kushinikizwa huo ni uongo maana rais kachaguliwa na wananchi so anasikiliza wananchi wanataka nini bila kubagua chama, kabila, rangi wala dini.
But hotuba ya rais ina mapungufu mengi hasa kwenye swala la ufisadi wa mikataba ya umeme ambao amekua muda mrefu ameweka pamba maskioni. TANESCO imekua mwiba kwa kodi za wananchi lakini yeye kama rais hajawahi kutoa msimamo wake juu ya kashfa za Tanesco.
 
jaamani tusiwe watu wa kulaumu kwa kila kitu, kunapokuwa na kizuri japo kidogo basi tutoe pongezi. mimi siku zote napinga sana uongozi wa JK kwa ujumla maan ni wa kishikaji zaidi.
Lakini kwa hili inagwa ni kweli amesoma majira na nyakati, yey kama Raisi hata kama angekataa ,kwani ungemlazimisha ? kuna serikali nyingi tu duniani haka USA zinafanya vitu vingine sababu tu ya influnce ya media, kwahiyo sioni ajabu kwa kikwete kukubaliana na kitu kulingana na upepo halisi.
 
SIJASOMA THREAD hii .... kwa kuwa naamini KILA ANACHOONGEA KIKWETE huwa ni MANENO.... mimi nitasema BAADA ya kuunda katiba... no comment
 
mnasahau kuwa wenzetu walifika kwenye katiba mpya baada ya kumwaga damu na kutiana jela.

JK tunampongeza kwa kutupeleka kwenye mjadala wa jambo hilo bila ya kufika huko na kwa hilo ndio tunapomsifia

JK ni kiongozi na sio mtawala


Na yeye kakubali katiba baada ya kuiba ushindi wa urais. Tofauti iko wapi?
 
Wewe nadhani unaufinyu wa mawazo, mtu anayefanya vitu baada ya kushinikizwa unamuona kwamba ni shujaa, kwa nini asianzishe mwenyewe? Pia watu mnafurahia tu bila kujua, Kwa nini aseme ataunda tume yeye na si bunge kuunda tume? angekuwa na nia njema na si shinikizo kwa nini hakusema timeframe? Tatizo huwa unajifanya mchambuzi lakini kinachokusumbua ni elimu.

We kichwa sana Mkuu! Ningekuwa na uwezo wa kukugongea Thanks nyingine 50 basi ningefanya hivyo. Sijui kwanini huyu jamaa hakusema ni lini jopo hili litaundwa. na kwa maoni yangu hii ya kuwa kimya ilikuwa ni makusudi kabisa ili waendelea kuangalia upepo kuhusu mjadala huu wa katiba. Wakiona wanaweza kuendelea kusubiri basi si ajabu hii 2011 ikakatika bila jopo hilo kuundwa maana ameshazoea kufanya kazi kwa kushinikizwa vinginevyo hawezi kuchukua leadership role.

 
acheni kutisha watu; ajenda ya Katiba mpya si ya Kikwete,siyo ya CCM na haijawahi kuwa ya CCM ever. Ajenda yao ni kuwa Katiba ya sasa inafaa na msimamo huu wamekuwa nao wakati wote wa kampeni na siku chache zilizopita. Sasa leo kugeuka huku lazima kuendane na maelezo.

Kwani ni Dr. Slaa aliyesema kuwa ndani ya siku 100 ataanzisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya; well angempa basi credit Dr. Slaa kwanza maana yeye amefanya hivyo ndani ya siku 100 japo siyo suala la kuandika upya katiba. Alichokifanya hakihusiani na mahitaji ya TAnzania zaidi ya mazingaombwe. Na to tell you the truth JK angesema hakuna Katiba Mpya watu wangempa pongezi vile vile kwa vile "rais kasema". Ni kikao gani cha CCM kilichopitisha uamuzi huu wa kubadili mawazo na kukumbatia wazo la Katiba Mpya au ni prerogative ya Rais?



Hivi wewe bado unafiki suala la katiba mpya limeletwa na mchungaji Slaa?

haya ni malalamiko ya Muda mrefu kwa upinzani hasa CUF toka zamani, Slaa wakati huo ana support ccm akiwa kanisani kabla ya kunyimwa kugombea ubunge kwa ticket ya ccm, hivi ulikuwa wapi wakati ule ??
 
So far What JK is doing now ni kujaribu kupunguza Pressure, hapo ana buy time tu hana Lolote, kwamba Watu wakisema basi ionekane hakuna Sababu maana Mkulu ameshalizungumzia ha ha ha
 
Redet: JK soma alama za nyakati Send to a friend Friday, 31 December 2010 20:48

Salim Said
MWENYEKITI Mwenza wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (Redet), Dk Benson Bana, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kusoma alama za nyakati na kubeba ajenda ya katiba mpya ili kuweka vipaumbele vyake na kujijengea heshima baada ya kustaafu kwake.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu jijini Dar es Salaam jana, Dk Bana alimtaka Rais Kikwete kuwapa Watanzania salamu bora za mwaka mpya kwa kuwaahidi katiba mpya kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka 2014.

"Kama napata fursa ya kukutana na rais leo (jana), kabla hajaanza kuwahutubia Watanzania, ningemshauri na kumuomba kabisa asome alama za nyakati, ni aibu ajenda ya katiba mpya kuongozwa na wapinzani, wanaharakati na watu wengine wakati serikali ipo," alisema Dk Bana na kuongeza:
"Mifano ipo ya kutosha, wenzetu wa Kenya na Uganda wameachana kabisa na katiba hizi za watu waliojifungia vyumbani na kutunga katiba bila ya kushirikisha jamii husika."

Dk Bana anaungana na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Jaji Omar Makungu, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mawaziri wakuu wa zamani, Joseph Warioba na Frederick Sumaye na Jaji Mkuu mstaafu Augostino Ramadhan kuunga mkono hoja ya kuundwa katiba mpya.

Madai ya Katiba mpya, pia yamewahi kutolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ambaye alisema bayana kuwa katiba mpya iandikwe mapema kabla ya mambo kuharibika.
Dk Bana anapingana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, aliyetaka katiba iliyopo iwekewe viraka.

"Suala la katiba mpya halitaki mjadala mrefu na wala sio la kuweka viraka, haya tumeweka viraka halafu iweje? Itasaidia nini? Hivyo viraka tumeweka mpaka tumechoka, lakini hakuna mabadiliko matatizo yanaendelea kuzidi," Dk Bana alipinga vikali kauli ya Jaji Werema.

Alisema katiba mpya ni msingi kwa Tanzania ya sasa na kwamba, serikali haipaswi kupata kigugumizi katika kuchukua ajenda hiyo ya kuanzisha mchakato wa kuipata haraka.
Dk Bana ambaye pia ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema katiba iliyopo haijibu maswali ya msingi ya Watanzania kuhusu mustakbali.

"Katiba ndio msingi wa taifa kwa kila kitu, hivyo pamoja na mambo mengine, lazima ijibu maswali ya msingi ya Watanzania, mambo ya Tume huru ya uchaguzi, nguvu ya rais, viongozi wa umma wawajibike kwa nani, katiba lazima iweke wazi mambo haya mazito," alisema Dk Bana.

Alifafanua kuwa, katiba mpya lazima iwe na fikra na mawazo shirikishi sio suala la mtu au kikundi cha watu kujifungia ofisini na kuandika katiba kwa niaba ya Watanzania.
Madai ya katiba mpya yalizidi kupamba moto baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo Rais Kikwete alitangazwa mshindi kupitia CCM.

Pia, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, tayari amewasilisha hoja binafsi ofisi za Bunge ili iweze kujadiliwa katika kikao kijacho cha bunge na CUF wamewasilisha mapendekezo yao ya katiba mpya kwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.
 
Mimi nataka kusikia yafuatayo:
1. Tume itaundwa na Bunge Februari 2011,
2. Maoni ya wananchi yatatolewa kwa siku 90, yaani Machi 2011 hadi May 30, 2011,
3. Katiba itaandikwa kwa siku 60, yaani Juni-Julai, 2011,
4. Wakati bunge la Bajeti Juni/Julai linamaliza bajeti yake, pia LIPITISHE KATIBA MPYA.

NAWASILISHA

Nadhani hujaisoma post ya mwanzo ya thread hii kiukamilifu.

Uelewe kuwa katiba si hoja mpya na wala si hoja ya Chadema au dk silaa!

CUF walishaandika rasimu ya katiba zamaaaaani.

CCM chini ya Mwinyi, kundi la wana CCM wakiongozwa na fundikira walishadai zamani katiba mpya.

Uelewe kuwa, katiba si msahafu, itakwenda ikibadilika na hakuna jipya hapo.

Kikwete jana kafunga kazi na nnakuhakikishia ataondoka kaacha, si tu katiba mpya au mwelekeo wa katiba mpya bali mengi mazuri na mema kwa Taifa. Maendeleo tuliyopata Tanzania katika miaka mitano ya Kikwete hayajawahi kufikiwa hata robo kwa awamu zote zilizopita kwa pamoja.
 
Kwanini jambo kubwa hili namna hii halikuwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM miezi michache tu iliyopita? Au ilipoifika Disemba 31, ndio walikumbuka kuwa tunaanza miaka hamsini ya uhuru wetu?

Ni kikao gani cha CCM kilichopitisha suala kuingizwa na CCM maana hadi hivi sasa Katiba mpya siyo sera ya CCM; sera ya CCM ni "kufanyia mabadiliko hii Katiba iliyopo kwani inatufaa" au tuanze kukumbushia kauli zao hizo tangu enzi za kina Mary Nagu, Mathias Chikawe n.k?

Yeye amepata wapi madaraka ya kuanzisha mchakato wa KUubadilisha ya nchi au kwa vile ni "Rais" basi tunaamini anaweza kufanya lolote wakati wowote with impunity?
 
Kwanini jambo kubwa hili namna hii halikuwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM miezi michache tu iliyopita? Au ilipoifika Disemba 31, ndio walikumbuka kuwa tunaanza miaka hamsini ya uhuru wetu?

Ni kikao gani cha CCM kilichopitisha suala kuingizwa na CCM maana hadi hivi sasa Katiba mpya siyo sera ya CCM; sera ya CCM ni "kufanyia mabadiliko hii Katiba iliyopo kwani inatufaa" au tuanze kukumbushia kauli zao hizo tangu enzi za kina Mary Nagu, Mathias Chikawe n.k?

Yeye amepata wapi madaraka ya kuanzisha mchakato wa KUubadilisha ya nchi au kwa vile ni "Rais" basi tunaamini anaweza kufanya lolote wakati wowote with impunity?

The past is history in files. We are longing for issues to be resolved. Tume ya kusimamia mabadiliko ya Katiba itaanza kazi lini, na kazi hiyo itaisha lini, to mention a few.

Kumbuka Rais hayuko kwa maslahi ya chama chake tu. Issue iwe ya chama cha upinzani au chama tawala, kama ni valid kwa ustawi wa wananchi wote na inahitaji mkono wa Rais, hana makosa kuichukua na kuifanyia kazi.
 
Nadhani hujaisoma post ya mwanzo ya thread hii kiukamilifu.

Uelewe kuwa katiba si hoja mpya na wala si hoja ya Chadema au dk silaa!

CUF walishaandika rasimu ya katiba zamaaaaani.

CCM chini ya Mwinyi, kundi la wana CCM wakiongozwa na fundikira walishadai zamani katiba mpya.

Uelewe kuwa, katiba si msahafu, itakwenda ikibadilika na hakuna jipya hapo.

Kikwete jana kafunga kazi na nnakuhakikishia ataondoka kaacha, si tu katiba mpya au mwelekeo wa katiba mpya bali mengi mazuri na mema kwa Taifa. Maendeleo tuliyopata Tanzania katika miaka mitano ya Kikwete hayajawahi kufikiwa hata robo kwa awamu zote zilizopita kwa pamoja.
Dar-es-Salaam,
You keep talking of maendeleo tuliyoyapata Tanzania katika miaka mitano ya uongozi wa Kikwete. Naomba unifahamishe hayo maendeleo kwa sababu mimi mwenzako sijaona kitu. Hasa pale unaposema hayajawahi kufikiwa hata robo kwa awamu zote zilizopita. Nitajie angalau mawili matatu na mimi niondoe tongotongo machoni.
 
Ndugu Zangu,

NIMEMSIKILIZA Rais wetu akilihutubia taifa jana jioni. Hii ni tafsiri yangu ya alichokiongea.


Kwanza kabisa nataka niseme, kuwa hotuba ile ya Rais Kikwete ni ya kihistoria. Ni moja ya hotuba muhimu sana katika historia ya nchi yetu tangu tupate uhuru. Maana, jambo lile la nne na la mwisho lililozungumzwa na Rais wa Awamu ya Nne kwenye hotuba yake, ndilo jambo lililofungua ukurasa mpya wa taifa letu baada ya miaka 50 ya uhuru. Rais

Jakaya Kikwete ameongea jambo kubwa sana usiku wa jana. Hakika, Kikwete hatabiriki na ni mtu wa rekodi. Jana ameweka rekodi nyingine.


Gwiji wa fasihi ya Kiswahili katika Tanzania na Afrika Mashariki, marehemu Shaaban Bin Robert alipata kuandika kitabu chenye kuhusu maisha yake; "Maisha Yangu Na Baada Ya Miaka 50".



Kwa hotuba ile ya Kikwete iliyobeba vision ya Kikwete kwa Tanzania kwa miaka 50 ijayo, inaweza kabisa kumweka JK katika nafasi ya kuanza kuandika kitabu juu ya kumbukumbu za maisha yake. Jinsi yeye, kama Jakaya Kikwete alivyoiona miaka yake 50 ya alikotoka na anavyoiona miaka 50 ijayo, si kwake tu, bali kwa nchi kubwa aliyojaaliwa kupata bahati ya kuiongoza. Nchi ya Tanzania.

Maana, JK kama binadamu, kuna mazuri na mabaya aliyoyafanya katika utendaji wake wa kazi maishani mwake. Na katika hili la Uona Mbali juu ya Katiba yetu, basi, kama JK atafanikiwa kuongoza juhudi hizi za Watanzania kupata Katiba iliyofanyiwa marekebisho makubwa, sina shaka yeyote, kuwa ataacha legacy kwa maana ya haiba. Katiba Mpya itakuwa moja ya jambo kubwa atakalokumbukwa nalo.


Ndio, JK atakumbukwa kama Rais aliyeongoza mabadiliko makubwa na ya kihistoria yaliyopata kufanyika katika nchi yetu. Kukumbukwa kwa kuchangia kuifanya nchi yetu kuwa mahali pema pa kuishi; kuwa nchi ya kisasa zaidi kuliko ilivyo sasa. Hofu yangu, ni kama JK ataweza kuachwa kuifanya kazi hii bila kukwamishwa na nguvu hasi za wahafidhina ndani ya chama chake, CCM.


Kwa anachotaka kufanya JK yaweza kabisa ikawa mchango wake katika kukinusuru chama chake, CCM. Kwamba CCM, kama chama, kisije kikapotea kabisa kwenye ramani ya kisiasa. Kwamba hata CCM ikija kushindwa, ibaki kuwa Chama cha Upinzani chenye nguvu na kinachoweza kurudi tena madarakani.


Maana, huko twendako, upo, uwezekano wa CCM kushindwa uchaguzi. Kwa Katiba ya sasa, siku CCM ikishindwa uchaguzi, itakuwa na maana ya chama hicho kuporomoka kama nyumba ya karata. Si hata Mzee Makamba mwenyewe alipata kutamka hadharani, kuwa Mtaji wa CCM ni Kikwete!


Na juzi hapa Mzee Makamba akatamka; kuwa hana maoni juu ya Katiba, anamsubiri JK atoe tamko. Hicho pia ni kielelezo cha mapungufu ya Katiba yetu. Na tushukuru nchi yetu haijapata bahati mbaya ya kuwa na 'mwendawazimu' pale Ikulu ya Magogoni.


Na wenye kutanguliza ubinafsi wao ndani ya CCM hawauoni ukweli, kuwa si miaka mingi kutoka sasa, Chama Cha Mapinduzi kitakuwa chama cha upinzani. Hawautambui ukweli, kuwa himaya zote duniani hujengwa na kuporomoka. Hakuna himaya iliyodumu daima. Hata Roma iliporomoka. Kwa vijana wa sasa, salamu ya " CCM Daima!" ni kielelezo cha watu waliopitwa na wakati.

Na kumsaidia JK katika kutupitisha kwenye njia hii salama tunayoitaka sasa ni kwa Watanzania kutambua ukweli, kuwa demokrasia yetu bado changa. Tumefanya chaguzi zenye walakini mwingi, ni sehemu ya kujifunza. Na sasa tuna fursa ya kuandaa Katiba itakayotufanya tujenge misingi imara ya demokrasia yetu.


Kumsaidia JK ni kukubali ukweli kuwa Uchaguzi uliopita umeshapita. Kwamba Serikali iliyo madarakani kwa sasa ndio hiyo inayoongozwa na JK kama Rais. Hatuna Rais mwingine. Hatuna Serikali nyingine. Rais tuliye naye sasa ni Jakaya Mrisho Kikwete.
Na tuukubali ukweli pia, kuwa wakati umebadilika na kuwa wananchi wanaukubali upinzani. Na kwamba kwa sasa CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani kikifuatiwa na CUF. CCM, CHADEMA , CUF na wengine wana lazima ya kushirikiana katika mambo ya msingi na yenye maslahi kwa taifa letu.

Ndio, tumeumaliza mwaka jana na mjadala wa Katiba mpya. Tunaingia mwaka 2011 na mjadala wa Katiba Mpya. Hili ni jambo jema. Na lililo muhimu kabisa katika mjadala wowote uwao ni kujiuliza; nini shabaha na malengo yetu? Nionavyo, shabaha na leo letu liwe kudumisha Umoja wetu wa Kitaifa, amani na utulivu tulio nao.

Kama swali ni je, Katiba yetu ya sasa, na kwa wakati uliopo, inakidhi matakwa ya shabaha na malengo yetu kama taifa? Jibu langu ni HAPANA. Na ndio maana nimekuwa na nitaendelea kuunga mkono juhudi za kufanya marekebisho makubwa ya Katiba yetu.

Na katika hili hatuna sababu za kugombania fito ilihali nyumba tunayojenga ni moja na ni yetu sote.
Ieleweke, kuwa madai ya Watanzania kupata Katiba mpya ni madai muhimu na ya kihistoria. Tumewasikia hata wanaojidanganya, wakiandika, kuwa madai haya yanatokana na ' Njama za mabeberu!'. Hizi ni propaganda za miaka ya 70, zimepitwa na wakati.

Ni busara kutambua, kuwa wakati umebadilika. Mtanzania wa mwaka 1977 si Mtanzania wa mwaka 2010. Hoja hii ya Katiba si kama nzi anayetua na kuruka. Hoja ya Katiba kwa sasa inaongozwa na kundi kubwa la vijana wanaotaka mabadiliko. Hawa si nzi wanaotua na kuruka, ni siafu wanaokuja kwa kuongezeka idadi yao.

Na madai ya marekebisho ya Katiba si madai mapya. Si madai ya chama au kikundi kidogo cha 'wapinzani' wasioitakia mema nchi hii. Ni madai ya msingi ya Watanzania, bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kidini, rangi na makabila.

Kama ni shauri mahakamani, basi, lilishafunguliwa. Kinachofanyika sasa ni mwendelezo wa shauri. Ndio, tunapongia mwaka 2011, madai ya Katiba mpya yatatimiza miaka 20. Yalianza tangu mwaka 1991.

Ndio, si wengi, miongoni mwa vijana wa sasa, wenye kumbukumbu ya ukweli huu. Tayari mwaka 1991 vuguvugu la kudai vyama vingi na Katiba mpya lilishaanza. Wakati huo madai makubwa yalikuwa mawili; vyama vingi na Marekebisho ya Katiba. Kuna mnaokumbuka ' KAMAKA'- Kamati ya Marekebisho ya katiba iliyondwa na wanaharakati. Hayo yalikuwa ni madai ya Watanzania ndani ya mfumo wa chama kimoja.

Marehemu Chifu Abdalah Fundikira aliongoza Kamati iliyoundwa, si na Serikali, bali wanaharakati, kuratibu mchakato wa kudai vyama vingi na Katiba mpya.



Hata wakati huo Mzee Mwinyi, kama Rais, aliweka ' mkwara', kuwa madai hayo yasiendeshwe na watu au makundi ya watu bila kibali cha Serikali. Presha ya madai ilipoongezeka, tunakumbuka, kuwa Mzee Mwinyi aliweza kusoma alama za nyakati. Aliongea pale Chuo Kikuu Mlimani na kuweka bayana dhamira ya Serikali ya kuunda ' Tume ya Nyalali' . Tume hiyo ilizunguka nchi nzima kuwauliza Watanzania kama wanataka kuendelea na Chama kimoja au Vyama vingi.

Itakumbukwa, Chifu Fundikira alipata kutamka; kuwa huko ni kupoteza muda na fedha za wananchi. Itakumbukwa pia, Mabere Marando alikuwa Katibu wa Kamati ile ya wanaharakati ya kuratibu mchakato wa madai ya kuwepo na vyama vingi na marekebisho ya Katiba. Marando alipata kutamka na kunukuliwa na Daily News, April, 12, 1991; " We have a bad political system because our Constitution embraces political discrimination. What we want is that all of us should shout out that our Constitution is bad." ( Mabere Marando, Daily News, April 12, 1991)

Ndio, Marando aliyasema hayo katika Semina ya kwanza ya Kamati ya kuratibu mchakato wa madai ya vyama vingi na Katiba mpya iliyoongozwa na Chifu Fundikira. Semina hiyo iliudhuriwa na watu wapatao 800 kwa mujibu wa taarifa ya Daily News la April 12, 1991.

Na akina Chifu Fundikira waliandamwa sana. Kwa mujibu wa Daily News la April 26, 1991, Mbunge wa Shinyanga, Ndugu Paulo Makolo alimshambulia Fundikira kwa kusema kuwa , katika hilo la kuwa na vyama vingi na katiba mpya , Chifu Fundikira hawasilishi mawazo ya Wasukuma na Wanyamwezi wenzake; " This is not a Wanyamwezi and Wasukuma movement. It is the selfish interests of Fundikira and his ten colleagues. Our people are not after parties. They want food, water, education and health care." ( Paulo Makolo, MP, Shinyanga, Daily News, April 26, 1991). Mwenyezi Mungu umrehemu Chifu Abdalah Fundikira.
Maggid
Iringa,
Januari Mosi, 2011
mjengwa

:frusty::frusty::A S 114::A S 114::blah: You Maggid, ww kazi yako si Journalist wa Siasa, bakia Global publishers, UDAKU fits you best, acha kuandika

usichojua, koma, kaandike nani KAFUMANIWA,na GUEST GANI, Nani na nani wanatoka kungonoka etc, hii ndio kazi yako, umbea Journalism
& kujua Ubongo wako how low u r, ETI JANA JK KAFANYA JAMBO KUBWA SANA.....!!!!!!!!!!???? :frusty::frusty: :smash::smash: hii njaa hii, mbaya sana,
hasa unapokuwa na njaa ya akili, kwani nani alianzisha hoja ya katiba mpya? hata hujui unaandika nini, na TUNATAKA TUME HURU IUNDWE NA BUNGE na Dowans mbona hujamuuliza
hajasema chochote?, nadhani umeelewa why i said ww UMBEA, UDAKU, Upaparazzi unakufaaaaa, hivi have you even Graduated F4? Kaandike Amani, Ijumaa, Uwazi, Risasi usiingilie kuandika Siasa, get out, hata hufanani na Kinyonga wala Bendera fuata upepo, shame on you, hufaiiiii period
 


:frusty::frusty::A S 114::A S 114::blah: You Maggid, ww kazi yako si Journalist wa Siasa, bakia Global publishers, UDAKU fits you best, acha kuandika

usichojua, koma, kaandike nani KAFUMANIWA,na GUEST GANI, Nani na nani wanatoka kungonoka etc, hii ndio kazi yako, umbea Journalism
& kujua Ubongo wako how low u r, ETI JANA JK KAFANYA JAMBO KUBWA SANA.....!!!!!!!!!!???? :frusty::frusty: :smash::smash: hii njaa hii, mbaya sana,
hasa unapokuwa na njaa ya akili, kwani nani alianzisha hoja ya katiba mpya? hata hujui unaandika nini, na Dowans mbona hujamuuliza
hajasema chochote, nadhani umeelewa why i said ww UMBEA, UDAKU, Upaparazzi unakufaaaaa, hivi have you even Graduated F4? Kaandike Amani, Ijumaa, Uwazi, Risasi usiingilie kuandika Siasa, get out, hata hufanani na Kinyonga wala Bendera fuata upepo, njaa yako mbaya, hufaiiiii period

Maggid katoa maoni yake, na wewe toa ya kwako. Mijitusi kwako ndio hoja.
 
Ukweli kuhusu hili ni kuwa kaanza kutekeleza ilani ya CHADEMA - within the first 100 days in office (though through the tunnel - like any other thief), ametangaza kuanza mchakato.

Ingawa ni mapema mno kusherehekea - maana wazaramo wana msemo wenye tafsiri ya 'kilonga mbali, kitenda mbali'

Time will tell
 
Maggid katoa maoni yake, na wewe toa ya kwako. Mijitusi kwako ndio hoja.

Most u r comments show u r KIHIYO as Maggid, arrogance dominates u r mind, you never say the truth, hatutaki Kiongozi of copying & pasting, pure & simple
 
Back
Top Bottom