Hotel Mövenpick Dar es Salaam

KADA ONA PUMBA ZAKO HAYO YALIKUWA MANENO YA BOB MARLEY DHIDI YA WAZUNGU NA WATU KAMA WEWE WENYE UTUMWA WA KIAKILI. ENDELEA KUNITUKANA TU KUHUSU UANAMKE WANGU KAMA VILE HUJAZALIWA NA MWANAMKE. LAKINI UKWELI UNABAKI KUWA WEWE NI 'KADA PUMBA'

tokea ujue kuandika umekuwa ukisumbua watu ! ndio uhuru huo wa kuongea mpenzi, so get it !
 
watu wa JF saa nyingine wanakuwa kama wazungu, yaani mtoto wa mwezi mmoja tu akisema mama, basi inakuwa NATIONAL NEWS. ndio hawa hapa !

Hhahahaha au wanafikiri mtoto "genius"..
 
Swadakta MOVE "N" PICK
Nilikumbuka wakati wa shule tulikuwa tunafanya mazoezi ya mbio za kupokezana vijiti. Hii thread you move and some one pick it and moves fast. Hapo Movenpick kumekuwa na mbayuwayu wengi sana kumbe wana-move na ku-pick. Hakika majina haya yatatudhalilisha sana nasi tutaback kusaini mikataba tu bila hata kujua tunang'ong'wa sana na wadau. Lakini kuna mdau mmoja aliwahi kusema maana halisi ya CCM ni CHUKUA CHAKO MAPEMA mbona naona kama ni sawa kabisa na MOVE 'N' PICK kasoro hakuna neno EARLY.
MOVE "N" PICK = CCM (CHUKUA CHAKO MAPEMA)
 
Swadakta MOVE "N" PICK
Nilikumbuka wakati wa shule tulikuwa tunafanya mazoezi ya mbio za kupokezana vijiti. Hii thread you move and some one picks it and moves fast. Hapo Movenpick kumekuwa na mbayuwayu wengi sana kumbe wana-move na ku-pick. Hakika majina haya yatatudhalilisha sana nasi tutaback kusaini mikataba tu bila hata kujua tunang'ong'wa sana na wadau. Lakini kuna mdau mmoja aliwahi kusema maana halisi ya CCM ni CHUKUA CHAKO MAPEMA mbona naona kama ni sawa kabisa na MOVE 'N' PICK kasoro hakuna neno EARLY.
MOVE "N" PICK = CCM (CHUKUA CHAKO MAPEMA)
 
Wanabodi,
Heee hee heee! Duh, ama kweli Wanbongo kwa kutoa tafsiri hatujambo!

Hii kampuni asili yake ni kutoka Swiss na kweli maana yake ni Move and Pick lakini kwa maana tofauti kabisa. kampuni hii imekuwa miaka yote ikijishughulisha na chakula yaani wanatoa huduma kama Buffet, tofauti yake tu ni kwamba hawa chakula chao kinapikwa wakati huo huo mbele yako na mteja huhitajiwa ku - move na Ku pick kile unachokihitaji kula. Katika kuongeza ama kujiimarisha zaidi nadhani ndio wamejipanua zaidi na kuingia ktk maswala ya Hotels pia yawezekana kuwa ni Frachise!
Kwa hiyo, tusije vikana kanzu, hali mpira tunao wenyewe!
 
Jamani Wana Jf

Ninaomba Kuliweka Wazi Swala La Hii Hotel. Lakini Kabla Ya Kusema Hivyo Ninaomba Niwaambie Kuwa Hakuna Swala La Kukwepa Kodi Katika Kubadilika Badilika Kwa Jina La Hoteli Hii. Swala Hili Ni Kutokufamu Tuu Kinachotokea Na Mimi Leo Ninaomba Niweke Wazi Swala Hili;

1. Hiteli Hii Haijawahi Kumilikiwa Na Sheraton Hotel, Royal Palm Hotel Wala Movenpick Hotel. Hoteli Hii Ni Mali Ya Taruss Investment Limited, Kampuni Ya Kitanzania. Hao Watu Wanaobandika Mabango Yao Nje Ni Hotel Managers Tuu. Wote Wanaingia Mikataba Ya Kuendesha Hoteli Na Siyo Mali Yao, Ni Sawa Tu Na Kumfukuza Meneja Mmoja Kumuweka Mwingine Kulingana Na Mwenye Mali Anavyotaka Aone Mali Yake Inavyosimamiwa. Mabadiliko Yanayoonekana Ni Mabadiliko Ya Mikataba Ya Kuendesha Hoteli Tuu Na Siyo Vinginevyo.

2. Misamaha Ya Kodi Hutolewa Wakati Wa Kuanzisha Mradi Tuu Na Hutolewa Kwa Vifaa Vya Ujenzi Tuu- Yaani Capital Equpment/goods Na Nafuu Ya Kodi Ya Ya Mapato Ya Asilimia 50% Ya Ngarama Ya Kuanzisha Mradi Huo Na Siyo Vinginevyo. Na Mwenye Haki Ya Kupata Misamaha Hiyo Ni Mweyemali Na Siyo Meneja. Kwa Sasababu Mwenye Mali Ndiye Aliye Wekeza Na Ndiye Aliye "take Risk". Kwa Mantiki Hii Basi Mwenye Mali Yupo Tanrus Investment Limited Na Mali Iliyopewa Misamaha Ipo(hoteli Inaonekana) Ila Mameneja Waliokuwa Wanasimamia Mali Ile Ndiyo Wamekuwa Wakibadilika Badilika Kutokana Na Sababu Mbali Mbali Ikiwa Ni Pamoja Na Kutokuelewana Na Mwenye Mali Au Mwenye Mali Kuuza Sehemu Ya Hisa Zake. Lakini Watu Hawa Wakibadilika Hainamaana Wanpata Tena Msaamaha Ya Kodi. Kwa Sababu Kilichopewa Msamaha Wa Kodi Ni Lile Jengo Na Vifaa Vyake Ambavyo Tunaviita Hoteli.

Asanteni Sana


[/list]
 
Tema

Karibu JF. Kama unaweza kutupatia kiasi cha kodi ambacho hii kampuni imelipa tangu waanze hii biashara inaweza kuweka mwanga kidogo ni jinsi gani wameweza kutimiza wajibu wao katika kulipa kodi na sio wababaishaji kama wengine.
 
DUA
aSANTE KWA KUNIKARIBISHA, SINA TAKWIMU YA KIASI CHA KODI KAMPUNI HII INAYOLIPA LAKINI NINAJUA WAKO KWENYE KUNDI LA WALIPA KODI WAKUBWA
 
Samahani wanajamii forum, mie ni mgeni hapa, na nimekuja na dukuduku langu sijui hapa ndio mahali pake, lakini naamini wana jamii foruma mtanisaidia.

Kuna ndugu yangu anafanya kazi katika Hoteli moja maarufu ya Nyota tano japo sina uhakika kama imefikia hivyo viwango vya nyota tano kweli au ni longolongo. Hoteli hiyo iliyoko katikati ya Jiji na ambayo iliwahi kubadilishwa majina mara tatu kutokana na kukwepa kodi na kwa sasa inamilikiwa na mtoto wa Mfalme wa Saudia inasemekana kuna mgogoro unafukuta humo na siku yoyote bomu litalipuka.

Nimedokezwa na mtoa habari kuwa uongozi wa Hoteli hiyo unataka kumuajiri Meneja rasilimali watu (Human Resources Manager) raia wa Kenya kwa kigezo kuwa eti Watanzania ni wezi na wanalindana, kwa hiyo akiajiriwa meneja Mtanzania anawalinda Watanzania wenzie hata kama ni wezi, hivyo uongozi wa Hoteli hiyo umedhamiria kuajiri Meneja Rasilimali watu kutoka Kenya maana atakuwa hana mchezo na atawakomesha Watanzania kwa kuwa hawajui na hana undugu nao.

Angalizo wanalotumia ni Hotuba iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua Hoteli ya Snow Crest kule Arusha, pale aliposema kuwa Watanzania waache udokozi, kwa sababu wawekezaji watakimbia, kauli hiyo imechukuliwa na uongozi wa Hoteli hiyo kama tuhuma za moja kwa moja kuwa Watanzania ni wezi kwa hiyo hawafai na ndio maana wanataka kumleta Mkenya ili awatie adabu.

Meneja aliyekuwepo na ambaye ni Mtanzania anamaliza muda wake mwishoni mwa mwezi huu wa Disemba na uongozi wake ulikuwa ni mzuri na unaozingatia haki, kama ni mtu kufukuzwa kazi alikuwa anafukuzwa kwa haki bila ya uonevu na hata migogoro ya kesi za madai katika mahakama ya kazi zimepungau kwa kiasi kikubwa kutokana na kuzingatia sheria za kazi.

Sasa hilo lilikuwa haliwafurahishi hawa wenzetu wazungu kwa kuwa wao walikuwa wanataka wakisema huyu simtaki hapa basi afukuzwe, kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani. Nchi hii inaendeshwa kwa katiba na sheria na hata katika maeneo ya kazi zipo sheria zianazomlinda mwekezaji na mfanyakazi, sasa iweje mtu akurupuke na kusema huyu simtaki halafu afukuzwe kazi bila kuzingatia sheria wala taratibu za kazi, hivi inawezekana kweli?

Ninavyofahamu mimi, ni kwamba sheria za kazi zimeweka bayana kuhusiana na kazi zinazopaswa kufanya na wageni na zile zinazopaswa kufanya na wenyeji, na ninafahaku kuwa nafasi ya Meneja Rasilimali watu (Human Resources Manager) inatakiwa ishikwe na mzawa ambaye anazifahamu sheria za nchi vilivyo na sio mgeni.

Hivi mgeni anaweza kujua sheria zetu za kazi na za nchi kweli? Na kwa kushika hiyo nafasi ina maana kuwa hakuna Watanzania wazawa ambao wanaweza kushika hiyo nafasi, mpaka aletwe mgeni?

Je nini majaaliwa ya Watanzania wanaofanya kazi katika Hoteli hiyo, watatendewa haki kweli?

Baada ya baadhi ya Wafanyakazi kuhoji kuhusu suala hilo katika mamlaka zinazohuzika wakianzia na chama cha wafanyakazi wa majumbani na mahotelini yaani CHODAWU walipewa ufafanuzi kuwa hilo haliwezekani kabisa kwa kuwa sheria iko wazi kuwa nafasi hiyo inatakiwa ishikwenna mzawa anayezijua sheria za kazi za nchi.

Sasa hivi baada ya kuona kuwa wafanyakazi wameshituka na wanahoji vigezo vinavyotumika ili kumleta Mkenya huyo, uongozi wa Hoteli ukiongozwa na Meneja Mkuu Msaidizi unasisitiza kuwa ni lazima huyo Mkenya aletwe hata kama itagharimu kiasi gani cha pesa kwani Money Talks.

Na jana Meneja huyo alikuwa na ahadi ya kukutana na Mkurugenzi wa TIC Bwana Ole Naiko ili kuomba asaidiwe kufanimikisha mkakati wao.

Taarifa ambazo tunazo ni kwamba Ole Naiko ametumiwa sana na Uiongozi wa Hoteli hii katika kuhakikisha kuwa wageni wanapata vibali vya kufanya kazi hapa nchini. Kwa mujibu wa maelekeza ya mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete aliagiza kuwa haitakiwi Hoteli yoyote kuajiri wageni zaidi ya watano, kwani hizo nafasi zinapaswa kushikwa na Watanzania na wapo, lakini katika Hoteli hio kuna wageni Kumi wanaofanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na Watanzania, na wengine wameishi hapa nchini zaidi ya miaka sita huku wakibadilisha nafasi za kazi kila kibali kikiisha muda wake.

Ukweli ni kwamba kuna kukinzana sana kati ya TIC na uhamiaji na haifahamiki kuwa ni nani mwenye mamlaka ya kuidhinisha wageni kupewa vibali vya kuanya kazi hapa nchini, uhamiaji wanawatupia mpira TIC na TIC wanawatupia mpira Uhamiaji.

Naomba wataalamu wa sheria walioko humu watujuze kama hii ni halali na inakubalika ndani ya nchi hii?
 
Rais akishateleza kwa nini aseme kwa media na nini ajadili na mawaziri wake kwa siri, haya hutokea. Baba hawezi kusema watoto wake ni wabaya unless ameshindwa kuwafanya wawe wazuri. Na zaidi yeye pia ni mdokozi kama ameshindwa kukemea au kuzuia udokozi wa wanawe. FULL STOP.
 
Rais akishateleza kwa nini aseme kwa media na nini ajadili na mawaziri wake kwa siri, haya hutokea. Baba hawezi kusema watoto wake ni wabaya unless ameshindwa kuwafanya wawe wazuri. Na zaidi yeye pia ni mdokozi kama ameshindwa kukemea au kuzuia udokozi wa wanawe. FULL STOP.

Kweli RAIS Tanzania tunaye!!! Hebu sote mini na wewe tufikirie mdhara ya neno au kitendo kabla ya kutenda!!! Watatumia slogan hiyo!!!! Na Ole Naiko si wa kule kule kwa mzee wa mamvi. Si unakumbuka jinsi ambavyo aliropoka wakati mzee wa mamvi alipoamua kuwajibika?? Hana lolote ni msanii sana yule.
 
Nchi zenye media na middle class hiyo kauli ilitosha kumuondoa Kikwete madarakani, maana ni kashfa na tusi kubwa kwa rais kuwaita watu wake wadokozi.

Kwanza ni vast generalization, hata kama kuna wadokozi wengi si sahihi kusema Watanzania ni wadokozi.Kuna mtu ana direct quotes na audio za Kikwete? Kweli nchi imepata rais.

Nashangaa Tanzania hii haikuwa habari kubwa.

Na hawa "wawekezaji" wasitake kutumia kisingizio cha Kikwete.Granted Kikwete ni mchemfu na kafanya mistake inayowapa mwanya kusema wanachosema.Lakini kama Tanzania nzima hamna mtu wa kufanya kazi hii, na Watanzania ni wadokozi kweli, sasa wao wamekuja kufanya nini katika nchi ya wadokozi? Si waende huko Kenya?

Hawa warabu ambao mostly ni washenzi wasiojua human dignity ndiyo tumeona watu wa kuwapa hoteli? Hamuoni wahindi wanavyojiua Dubai kutokana na kuishi kama watumwa? Haw
 
Akiulizwa tena na media au wananchi siku moja (kama akirudia kile kipindi - mpigie simu Rais) kuthibitisha kauli yake hiyo JK atasema wamemnukuu vibaya.
 
GOGORO LAFUKUTA MOVENPICK DAR ES ES SALAAM??

2571532.jpg



Kaka Issa Michuzi,

Sisi wafanyakazi wa Hoteli ya Movenpick Royal Palm Hotel tunaomba utufikishie kilio chetu dhidi ya uongozi wa hoteli hii ambapo unatunyanyasa kiasi cha kutuona sisi wafanyakazi wazawa kuwa wote ni wezi.

Uongozi wa Hoteli hii unataka kumuajiri Meneja rasilimali watu (Human Resources Manager) raia wa Kenya kwa kigezo kuwa eti Watanzania ni wezi na wanalindana, kwa hiyo akiajiriwa meneja Mtanzania anawalinda Watanzania wenzie hata kama ni wezi, hivyo uongozi wa Hoteli hiyo umedhamiria kuajiri Meneja Rasilimali watu kutoka Kenya maana atakuwa hana mchezo na atawakomesha Watanzania kwa kuwa hawajui na hana undugu nao.

Angalizo wanalotumia ni Hotuba iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua Hoteli ya Snow Crest kule Arusha, pale aliposema kuwa Watanzania waache udokozi, kwa sababu wawekezaji watakimbia. Kauli hiyo imechukuliwa na uongozi wa Hoteli hiyo kama tuhuma za moja kwa moja kuwa Watanzania ni wezi kwa hiyo hawafai na ndio maana wanataka kumleta Mkenya ili awatie adabu.


Meneja aliyekuwepo na ambaye ni Mtanzania amemaliza muda wake na anaondoka katikati mwezi huu na uongozi wake ulikuwa ni mzuri na unaozingatia haki, kama ni mtu kufukuzwa kazi alikuwa anafukuzwa kwa haki bila ya uonevu na hata migogoro ya kesi za madai katika mahakama ya kazi zimepungau kwa kiasi kikubwa kutokana na kuzingatia sheria za kazi.

Sasa hilo lilikuwa haliwafurahishi hawa wenzetu wazungu kwa kuwa wao walikuwa wanataka wakisema huyu simtaki hapa basi afukuzwe, kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani. Nchi hii inaendeshwa kwa katiba na sheria na hata katika maeneo ya kazi zipo sheria zianazomlinda mwekezaji na mfanyakazi, sasa iweje mtu akurupuke na kusema huyu simtaki halafu afukuzwe kazi bila kuzingatia sheria wala taratibu za kazi, hivi inawezekana kweli?

Tunavyofahamu sisi, ni kwamba sheria za kazi zimeweka bayana kuhusiana na kazi zinazopaswa kufanya na wageni na zile zinazopaswa kufanya na wenyeji, na ninafahaku kuwa nafasi ya Meneja Rasilimali watu (Human Resources Manager) inatakiwa ishikwe na mzawa ambaye anazifahamu sheria za nchi vilivyo na sio mgeni.
Hivi mgeni anaweza kujua sheria zetu za kazi na za nchi kweli? Na kwa kushika hiyo nafasi ina maana kuwa hakuna Watanzania wazawa ambao wanaweza kushika hiyo nafasi, mpaka aletwe mgeni?

Je nini majaaliwa ya Watanzania wanaofanya kazi katika Hoteli hiyo, watatendewa haki kweli?

Baada ya baadhi ya Wafanyakazi kuhoji kuhusu suala hilo katika mamlaka zinazohusika wakianzia na chama cha wafanyakazi wa majumbani na mahotelini yaani CHODAWU walipewa ufafanuzi kuwa hilo haliwezekani kabisa kwa kuwa sheria iko wazi kuwa nafasi hiyo inatakiwa ishikwe na mzawa anayezijua sheria za kazi za nchi.


Sasa hivi baada ya kuona kuwa wafanyakazi wameshituka na wanahoji vigezo vinavyotumika ili kumleta Mkenya huyo, uongozi wa Hoteli ukiongozwa na Meneja Mkuu Msaidizi unasisitiza kuwa ni lazima huyo Mkenya aletwe hata kama itagharimu kiasi gani cha pesa kwani Money Talks.

Taarifa ambazo tunazo ni kwamba Kigogo mmoja amekuwa akitumiwa sana na Uiongozi wa Hoteli hii katika kuhakikisha kuwa wageni wanapata vibali vya kufanya kazi hapa nchini.


Kwa mujibu wa maelekezo ya mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete aliagiza kuwa haitakiwi Hoteli yoyote kuajiri wageni zaidi ya watano, kwani hizo nafasi zinapaswa kushikwa na Watanzania na wapo, lakini katika Hoteli hio kuna wageni Kumi wanaofanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na Watanzania, na wengine wameishi hapa nchini zaidi ya miaka sita huku wakibadilisha nafasi za kazi kila kibali kikiisha muda wake.

Ukweli ni kwamba kuna kukinzana sana kati ya TIC na uhamiaji na haifahamiki kuwa ni nani mwenye mamlaka ya kuidhinisha wageni kupewa vibali vya kuanya kazi hapa nchini, uhamiaji wanawatupia mpira TIC na TIC wanawatupia mpira Uhamiaji.

Tunaomba mtufikishikie kilio chetu kwa wahusika watueleze kama hii ni halali na inakubalika ndani ya nchi hii? Ni sisi wafanyakazi Moevenpick Royal Palm Hotel Dar Es Salaam.

Wadau JF hivi working permit huwa nani anatoa? Na je inaruhusiwa kutoa vibali hivi vya kazi hata kwa kazi ambazo hata watanzania wanaweza kuzifanya?
 
Wakuu wanaJF kuna mgogoro uliwahi kulipotiwa ktk blog ya michuzi na ukatolewa maoni na wadau mbali mbali. Nimeona si vibaya tukishiriki pia kuona ni yapi yanaendelea kujiri ktk mgogoro huo.

Yafuatayo hapa chini ni maelezo ya wafanyakazi wa hoteli hiyo kujibu michango ya wadau mbali mbali wa blog ya Michuzi.



Kaka Michuzi,

Pole na majukumu yako ya kila siku, pia tunashukuru kwa kuweka malalamiko yetu katika blog yako ya jamii na wadau wengine wakapata fursa ya kuchangia maoni yao.

Kaka Michuzi sisi wafanyakazi wa Hoteli ya Movenpick tumesoma kwa makini maoni ya wadau wote waliochangia kuhusiana na sakata lililoikumba Hoteli yetu, pamoja na maoni mazuri lakini tumesikitishwa sana na baadhi ya wadau kuchanganya mada aidha kwa kutaka kumaliza hasira zao au tuseme kutojua kuwa sisi tunazungumzia nini.


Kwa mfano wapo waliotoa maoni ya jumla kuwa ni kweli sisi watanzania ni wezi na kutuunganisha sisi na wafanyakazi wa Bandari na wale wa Airport. Hawa naamini ni watanzania wanaoishi Ughaibuni, kwamba baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa hizo taasisi mbili wamekimbilia kutuunganisha nao.


Sisi tunasema hiyo sio sawa, sisi hatuhusiki na kutoa mizigo bandarini wala kukagua mizigo Airport. Kuna mdau mmoja yeye alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hata Ivory Coast ililalamikia Hoteli yetu kuwa ina huduma mbovu na vyumba na vyoo ni vichafu pia, huyu tunadhani alishindwa kutofautisha kati ya Movenpick na Kilimanjaro Kempinski. Timu ya taifa ya Ivory Coast haikulala Movenpick bali ililala katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk, na hayo ndio matatizo ya kudandia mada bila kufanya utafiti.


Kuhusu swala la wizi, na udokozi, tunaomba kuweka bayana kuwa ni kweli vitendo hivyo vipo kama ilivyo katika taasisi yoyote, huwezi kuendesha taasisi iliyoajiri wafanyakazi zaidi ya 300 halafu uwe na wafanyakazi wote wasafi, labda kama umeajiri malaika.


Kuna wafanyakzi wengi wamefukuzwa kwa makosa ya aina hiyo na wengine wamevuliwa vyeo kwa uzembe, pale inapoonekakana kushindwa kutekeleza majukumu yao.


Hoteli yetu, na labda hili wengi hawalifahamu. Katika Hoteli zote zilizopo hapa nchini Movenpick ndiyo Hoteli pekee yenye tawi la CHODAWU na kuna kamati maalum ya nidhamu inayoshirikisha uongozi wa hoteli na wajumbe wa CHODAWU ambapo jukumu lake ni kusikiliza kesi za wafanyakazi kabla ya mfanyakazi kufukuzwa.


Kamati hii imekuwa ikishirikiana na uongozi wa Hoteli katika kukomesha tabia ya wizi na uzembe kazini na hili limekuwa likifanyika kwa ushirikiano wa Meneja rasilimali watu anayeondoka.


Tatizo lililopo ni kwamba hawa wenzetu wazungu na hasa Meneja mkuu msaidizi bwana Shousha, na mpishi mkuu Bwana Vicenzo kutaka kuindesha hoteli hii kwa mkono wa chuma, wamekuwa hawaheshimu sheria za kazi na wamekuwa na maamuzi ya kuonea wafanyakazi. Ni watu ambao wanapotaka mfanyakazi aondolewe kazini hilo lifanyike bila kufuata taratibu na sheria za kazi, na huyu bwana Shousha ndiye anayesisitiza zaidi kutaka Meneja rasilimali watu kutoka Kenya aajiriwe akiamini kuwa yeye anaweza kufanya kazi bila kufuata sheria na kanuni za kazi za hapa nchini.


Sisi hatulalamiki kwa sababu ya huyo mkenya kuletwa, sisi hatuna matatizo na yeye, kilichotusukuma kuleta malalamiko yetu katika blog ya jamii ni kupinga ile nia ovu ya kuletwa kwa mkenya huyo, yaani ile kauli ya kusema kuwa atatukomesha, pili ni kutaka taratibu zote na sheria za uhamiaji zifuatwe.


Tunaamini kuwa ajira yoyote inayohusu mgeni ni lazima idhibitike kuwa hakuna mtanzania mwenye sifa hizo. Je ina maana tangu tupate uhuru mwaka 1961 serikali yetu imeshindwa kusomesha watu wenye uwezo wa kuwa mameneja rasilimali watu?


Hotel hii inayo wafanyakazi wageni zaidi ya 10, ambao hata hivyo vibali vyao vina mashaka matupu, wamekuwa wakikitumia kituo cha uwekezaji cha TIC kufanikisha malengo yao ya kuleta wageni kuchukua ajira zetu.


Kuna siku walikuja watu wa uhamiaji kutaka kuona vibali vya hawa wageni, mbona wote walikimbia, kwani kuna ambao wanaishi hapa hotelini na vibali vyao vya kuwepo hapa nchini vinaonyesha kuwa ni watalii.

Tunachotaka ni sheria za uhamiaji na taratibu zote za ajira kwa wageni zifuatwe kwa mujibu wa sheria, hatuna shida na wageni, lakini ikumbukwe kuwa ni serikali hii hii iliyoahidi katika kampeni za mwaka 2005 kuwa itazalisha ajira milioni moja, sasa kama ajira zenyewe zinachukuliwa na wageni, hizo ajira milioni moja zitapatikana wapi?


Wale mliosema kuwa ni heri waajiriwe wageni kwa kuwa watanzania ni wezi, jaribuni kutafakari kauli zenu, mkumbuke kuwa hata nyie ni watanzania na kwa kusema kuwa watanzania ni wezi, ni sawa na kuuambia ulimwengu kuwa sisi sio watu wa kuaminiwa, kwa wale walioko nje mjue kuwa hata nyie mmejitia kitanzi, hamtaweza kuaminiwa kabisa.

Je hamjui kuwa kuna nafasi za ajira ambazo zingeweza kushikwa na wake zenu watoto wenu, wajomba zenu, shangazi zenu, dada zenu, na ndugu zenu watanzania ambazo zimeshikiliwa na hawa wageni?

Kuhusu kuwa wakenya ni wachapa kazi, sawa tunakubali, lakini je nao ni wasafi kiasi gani? Hivi mnajua kuwa kuna baadhi ya mawaziri nchini Kenya hawaruhusiwi kuingia nchini Marekani na Uingerza kwa sababu ya makosa ya Rushwa, je Uzalendo wao uko wapi, uadilifu wao ulo wapi? Je sisi, ni mawaziri wangapi wamezuiwa kuingia katika nchi hizo?


Hawa wazungu, wanasema kabisa kuwa katika nchi ambazo wananchi wake ni wapole na wanyeyekevu hata uwafanyie nini ni Tanzania, na ndio maana hapa Movenpick kuna baadhi ya wazungu wameongeza muda wa kuishi na kufanya kazi hapa nchini zaidi ya mara nne kwa kubadili nafasi zao za ajira ili kupata ridhaa ya kuendelea kuishi hapa nchini.


Hawataki kuondoka kwa kuwa nchi yetu ni Corrupt katika kila sekta. Wazungu hawa wanajilipa mishahara mikubwa tofauti na wazawa. Mtanzania anaweza kulipwa shilingi milioni 2 lakini akija mzungu kwa nafasi hiyo hiyo analipwa dola elfu sita, sio shilingi za kitanzania namaanisha dola za kimarekani achilia mbali malazi chakula na huduma nyingine kama kufuliwa nguo na kadhalika.

Mshahara mkubwa kabisa wa mtanzania hapa ni shilingi milioni mbili na mshahara wa mzungu wa chini kabisa ni dola elfu sita, na huyu mzungu anayelipwa hizi fedha ni nokoa tu, hajui kazi, kazi zote zinafanywa na mtanzania, rangi tu ndiyo inayomlinda.

Tunapenda kumalizia kwa kusema kuwa Mkenya aletwe lakini sheria na taratibu za uhamiaji zifuatwe.


Ni sisi wafanyakazi wa Hoteli ya Movenpick
Dar Es Salaam.
 
Watu wa uhamiaji lazima wazinduke kwa sababu TIC inakula rushwa kupitia uwekezaji uchwara.
 
Hii COMPLEX ya kushabikia Wazungu sijui itaisha lini.

Ndiyo matatizo ya kuwa na CCM/TANU and ASP kwa miaka zaidi ya 40.

Hadi aje Mkorofi ndiyo atawapa hawa jamaa kibano.
 
Back
Top Bottom