Hotel Mövenpick Dar es Salaam

Waliojenga jengo ni kambuni ambayo inaitwa Taruss Investment Limited ( imesajiliwa Tanzania lakini wamiliki wake ni bwana moja ambaye kama sijakosea anaasili ya Ugiriki) na hujy jamaa alipata mkopo alipojenga hilo jengo na kwa kipindi kile Dar kulikuwa haakuna hoteli nzuri ya kimataifa nchi ilikosa opportunities nyingi saana. So mwenye jengo hana hata kidogo utaalamu wa kuendesha hotel alingia mkataba na Sheraton wao wakaja kama MANAGEMENT COMPANY kuiendesha baada ya Sheraton walitofautiana na mwenye mali ( Taruss Investment Limited) ikabidi awafukuze then aka hire Royal palm ambayo ni MANAGEMENT company wakaanza kuiendesha ikumbukwe walipotofautiana na mwendeshaji wa kwanza na alipondoka ilibidi aondoke na jina lake yaani SHERATON, hawa wasouth africa walipokuja wao jina lao ni royal palm moja kwa moja jina likabadilika, baada ya muda Taruss Investment Limited waliuza majority share yaani (jengo) kwa kambuni moja ya mtoto moja wa falme za kiarabu ambaye na yeye ana mahoteli nchi mablimbali lakini mahoteli yake yanaendeshwa na SWISS hotel managment company ( Movenpick) ndo ikabidi waje waanze kuindesha ikabidi ibadilishwe jina kuwa moven pick.

Biashara a hoteli inavyoendesha ni tofauti kidogo kwa mlio DSM naamini mnajua Holiday INN walikuwa wanendesha ipo karibu ocean road hospital lakini walitofautiana na wenye mali wakaondoka wakaingia mkataba na mwenye jengo mwingine sasa wanaendesha hotel iliopo karibu na posta mpya, ile ya zamani waliokuwa wanaimiliki wanaindesha kwa jina lo Southern sun, haya mambo katika hii biashara yapo

swala la kusamehewa kodi pale mwanzoni TZ ilikuwa na sheria ambazo zilikuwa zinawanufaisha wawekezaji saana naamini ile sheria wameshaibadilisha haitoi tena manufaa kwa wawekezaji kama ile miaka hawa Taruss Investment Limited walipo jenga hoteli yao na kupata misamaha ya kodi

Ikumbukwe hata the real owner of kilimanjaro hoteli sio yeye anaye iendesha hiyo hoteli, mwendeshaji ni Kempinski ambayo wakitofautiana na mwenye mali anaweza wafukuza na kuajiri management company nyingine.

cha msingi ni serekali kushawishi hizi management company kujenga hoteli zao wenyewe hapa nchini kama SERENA wanavyofanya hapo ndo tutaweza kufaidika vizuri

cha msingi serekali inatakiwa iwe makini kwakushawishi
 
probably umesahau kwamba nchi inapata aina nyingine za kodi kama VAT na nyinginezo halafu si bora hata sisi tunaonekana tuna 5 star hotel kwani ingekua mikononi mwa serekali mpaka sasa, nadhani ingekua na hadhi ya 1 or 2 star so better to be in the hand of so called investors
 
Hili ni jina la biashara kwa mtandao mahotel na resorts duniani zinazoendeshwa na kampuni ya ki-swiss. jengo lipo tanzania( mwenye nyumba) na wanaoendesha biashara hii ni wapangaji kwa njia moja au nyingine. Naamini serikali/nchi inafaidika kwa uendeshaji wa biashara hii Ebu zuru hapa kwa taarifa zaidi juu ya hoja ya "Move N Pick". Je na huko kwingineko una hoja gani? nako wanaMove N Pick??.
Samaki mmoja akioza ameliwa na funza!!!! Si wote! tumtafute huyo alieoza TUMTOE kapuni...asije akaozesha wengine.

http://www.moevenpick-hotels.com/en/pub/homepage.cfm
 
Back
Top Bottom