Hosni Mubarak Ana Kansa ya Tumbo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Aliyekuwa rais wa Misri kabla ya kulazimika kung'atuka madarakani kufuatia maandamano ya raia, Hosni Mubarak maisha yake yako hatarini kutokana na kansa ya tumbo.
Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak ambaye alitupwa jela akisubiri kesi inayomkabili ya kutoa amri ya kuuliwa kwa watu waliokuwa wakiipinga serikali yake, anasumbuliwa na kansa ya tumbo kwa mujibu wa mwanasheria wake.

Mubarak pamoja na wanae anatarajiwa kupandishwa kizimbani mwezi wa nane mwaka huu kujibu mashtaka ya mauaji ya waandamanaji ambapo iwapo atapatikana na hatia huenda akahukumiwa kunyongwa.

"Ana kansa ya tumbo na uvimbe kwenye tumbo lake unazidi kuongezeka", alisema mwanasheria wake Farid al-Dib.

Mubarak mwenye umri wa miaka 83, amelazwa kwenye hospitali ya jela kwenye mji wa Sharm el-Sheikh kutokana na matatizo ya moyo yaliyomuanza aprili 13 wakati alipokuwa akihojiwa kuhusiana na mauaji ya waandamaji.

Mubarak na watoto wake na baadhi ya waliokuwa mawaziri wake watapandishwa kizimbani tarehe tatu mwezi wa nane wakikabiliwa na tuhuma za mauaji na makosa mengine ya rushwa na ubadhirifu.
 
Back
Top Bottom