Hongereni WAPO Radio

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,037
Kama pongezi zangu zitawaudhi watu falni basi ni juu yao but Napenda sana kutoa pongezi zangu binafsi kwa jinsi Radio hii ilivyo na vipindi makini na kuhoji watu makini na kupata habari makini bila upendeleo wowote.

Nilitegemea sana kama ilivyo kwa wengi kuwa, kwa kuwa na RADIO ya Kidini basi muda woote ingekuwa ikizungumzia dini tuuuuu na biblia au na Ukristo, la hasha, radio hii imekua chanzo kikuu ( kwa upande wangu) kunipataia habari ambazo hua naridhika sana nazo.

Hongereni kwa jinsi mlivyoripoti kuhusu Uchanguzi Mkuu, hongereni sana sana kwa jinsi mlivyowasaidia Waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto ( Hakika mliwaunganisha wengi regardless ya dini zao) Hongereni pia kwa kipindi chenu cha PataPata na kile cha jioni pia ambacho mnahakikisha kabla ya kurusha habari hiyo inakuwa imethibitishwa na mamlaka husika.

Ni mengi mliyoyafanya, hongereni, naomba na ile redio ya kulaumu tuuuuuu ijaribu kuiga mfano wa radio kama hizi, hongereni tena, Kwa wale walioko Dar ni 98.0 Fm
 
Hongereni WAPO kwa yote mliyosifiwa...
... sasa ongezeni masafa msikike mbali zaidi ....!!!
 
Wanasikika kwa baadhi ya mikoa, sijajua bado ila Pwani, Tanga, Kilimanjaro n.k wanasikika
 
hii sio ndiyo ile redio iliyochini ya CASFETA?? au nimekosea?
naomba kusahihishwa tafadhali?
 
hii sio ndiyo ile redio iliyochini ya CASFETA?? au nimekosea?
naomba kusahihishwa tafadhali?
Mpwa, kwa hakika sijui the real Owner lakini ambacho nina uhakika nacho ni kwamba ni ya dini na habari zake ni changamoto kubwa sana kwa radio nyingine...nimejaribu kukujibu, ngoja tusikilize na wadau wengine
 
Katika Redio zote zinazomilikiwa na taasisi za kidini, hii Redio wapo haina mpinzani, mimi sigusii vipindi vya kidini ila kuna kipindi kinaitwa meza ya busara, kwa hakika ni meza ya busara kweli na cha kufurahisha zaidi unakuta watu wenye majina yanayotambulika kama ni majina ya kiislamu ndio wanakuwa wachangiaji wengi zaidi bila jazba kwa kujenga nchi. kwa kweli big up Wapo redio.
 
Ni radio ya jamii kweli, haichagui haibagui inawakilisha habari zote ziwe ni za kidini ama kijamii kwa usahihi kabisa.
Ni radio ambayo imenishangaza kwa kuwakutanisha wahadhiri wa kiislamu na wahubiri wa kikristo kujadili mada mbalimbali kwa upendo na busara ya hali ya juu kiasi kwamba hawa watu wanajijenga kama familia moja yenye kutegemeana mmoja kwa mwingine.
Naifagilia!! Laiti zele redio zilizo na sura ya kushabikia upande mmoja zingekuwa hivi, amani yetu ingedumu sana.
Kituo hiki nadhani kinamilikiwa na mtu aneitwa mchungaji Gamwanya.
.
 
Ni Gwamanya
 
namm nawakilisha pongezi zangu za dhati kwa wapo radia kwa kweli wapo juu ni nuru ya jamii aibagui dini wala serikali kuna kipindi cha pata pata asubui na ucku zilizotufikia bila kusahau meza ya busara hapo ni funga kazi mana imesheheni kila idara kila jambo lenye utata ujadiliwa hapa aijalishi ni la dini, serikali binafsi. Hii ipo chini yawapo mission inayoongozwa na bishop gamanywa
 
Saafi, nadhani wanastahili hizi sifa
 
Back
Top Bottom