Sharp lady
Senior Member
- Feb 23, 2011
- 129
- 13
Ni kwa muda mrefu sasa TBC kama chombo cha serikali cha habari kimeshindwa kabisa kutii kiu ya watazamaji wao na si kwakutokujua wanafanya nini ila kwa makusudi makubwa mnabana au hamtoi kabisa taarifa za msingi na kwa coverage yakutosha kumwezesha mtazamaji kuelewa na kujivunia chombo hiki cha taifa letu. Kwa ushauri tu hiyo kauli mbiu yenu ya ukweli na uhakika ni bora muifutilie mbali kwani hamuitendei haki, mnachagua nini cha kutangaza na kwa manufaa ya nani mnapenda sana kuruka habari za msingi hasa zile zinazolihusu taifa na jamii moja kwa moja, hebu igeni japo kidogo kutoka kwa ITV kwa sababu nikiwaambia mfanye hata nusu ya ufikishaji habari kwa kiwango na ubora kama wafanyavyo BBC hamuwezi kwani hamtaweza kuwafunika vizuri wale muwapendao. ITV inafanyakazi kihalali unaangalia taarifa mpaka unaifurahia unaelewa inahusu nini na point za msingi zote unazipata wanajua kupangilia matukio yao ipasavyo. Hongereni sana ITV mnafanyakazi nzuri sana mko up minute na mnatekeleza wajibu wako ipasavyo. TBC jirekebisheni mnakoenda siko kama huo usiku wenu wa habari ndo kabisa hamna kitu. Watazamaji tunataka taarifa za kina na upminute ndiyo maana watu wanalipia CNN/BBC n.k wapate kupata taarifa ipasavyo. Mnashindwa hata na chipukizi Mlimani TV wenye coverage ndogo??? vijana wanakupa taarifa mpaka unatamani wangekuwa wanawafikia hata nusu ya Tz. TBC fanyeni mabadiliko ya haraka nyie msijivue gamba bali mjitoe ngozi kabisa alafu muache UPENDELEO. Acheni nakutengeneza TBC kibao zisizokidhi haja imarisheni hiyo 1 kwanza. Good day.