Hongera Rais kwa usajili wa alama za vidole, ila tambua kwamba haupo salama!

Ili kuondoa utata huu ni bora TCRA waje na mfumo mwingne wa maulizo ya ID ya mtu moja #ime tumika ktk usajili wa simcard ngapi ili kugundua kama kuna usajiri fake ambao umefanywa na ID husika bila ya mtu huyo kuhusika
Sasa kwa mfano wakagundua id moja imesajili line 10 katika mikoa 8 tofauti watamjuaje origianal?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu utaratibu ni mzuri na utapunguza utapeli na matumizi yasio mazuri ya line za simu .Changamoto zitakuwepo lazima NIDA wajipange, kwa mfano kuwe na namna ya kuulizia namba ulizosajili alafu kama hauzitambui basi unaziblock na kufuta usajili wake, kama unazitambua basi unaacha kama zilivyo .
 
Nafikiri taarifa hizi zinafikirisha kweli ingawa mimi siamini kuwa TCRA wameiacha system porous kiasi cha kufanyiwa ujanja na wanaosajili hizi laini. Ukweli ni kwamba hii haraka ya kuwatambua raia na kuwapa namba naitilia shaka kiasi kwamba ni rahisi kuwapa uraia watu wasiostahili. Pale mwanzo kulikuwa na mchakato bora sana wa kumfanyia vetting mlengwa uliohusisha watu wa uhamiaji, lakini kinachoendelea sasa huku mitaani yaelekea ni kwa ajili ya kusajili laini za simu tu na si kutambua yupi ni raia anayestahili ID na yupi sio.
Hata hivyo ni wajibu wa NIDA kuutolea maelezo kitaalamu kila wasi wasi wa wadau juu ya uwezekano wa mfumo kuingiliwa na kusajili line nyingi kwa taarifa za mtu mmoja, kwani kama hii inaweza kutokea basi itakuwa hatari sana na zoezi zima likawa halina maana. Yawezekana ni wasi wasi tu wa wadau lakini ni vizuri TCRA na NIDA wakatuhakikishia raia sisi mambumbu wa taaluma ya Tehama usalama wa mfumo wetu. Huku mitaani ni vululu vululu kwani kuna maeneo watu wanalipisha kusajili line kama mdau alivyodai line iliyosajiliwa inauzwa elfu tatu.
Rekebisha sehemu kwenye andiko lako. Kwa maelezo ya NIDA wenyewe,, vitambulisho vya NIDA havitolewi kwa RAIA tu bali kwa kila mtu anayeishi Tanzania kihalali.

Maana yake hata raia wa nje wanaoishi nchini kihalali na hata wakimbizi wanapewa vitambulisho hivi. Lengo ni kutambuana na hivyo kupunguza matukio ya kihalifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ss wakikukamata finger print zitamatch wewe wa Dar na za tukio lililopo Mbinga?..
Mkuu kikubwa chukua tahadhari, kwa mfano wakakuambia tuonyeshe huyo uliemsajilia line alafu ukamtuma mbinga akaibe benki yupo wapi manake kila kitu ni chako kuanzia majina, finga printi, tarehe na mwezi uliozaliwa hadi mwaka, then uulizwe useme humjui? Hapo ndo utaposhangaa na roho yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nisaidiwe na mimi swali hili:

Kawaida ukishasajiliwa kwa alama za vidole kwa ajili ya kupewa kitambulisho cha NIDA namba ya kitambulisho hicho hupewi hapo hapo. Inachukua siku hata miezi kuja kuipata.

Sasa watakaojisajili, mfano wiki ya mwisho au siku ya mwisho kabisa watasajilije line zao maana namba zitakuwa bado hazijapatikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...
Niliaminishwa usajili wa laini ya simu kwa dole ni kitendo cha dole unalopachika kwenye kadude, alama zake zinaoanishwa na zile za kitambulisho cha taifa . .
Kumbe sivyo..
Alama za dole na taarifa zako zinalambwa na kampuni ya simu
...
 
Njia sahihi ni kupunguza makampuni ya Simu za mkononi mfano sasa Tigo wamemnunu Zantel na kuipunguzi hiyo moja, Voda wawanunue Halotel na TTCL wawanunue Airtel, zibakie kampuni 3 chache za simu kama Uganda, kenya, South Africa, China, America na ulaya ambapo hakuna utitiri wa makampuni ya Simu za mikononi itasaidia kuwadhibiti watumiaji wa simu, kuliko kubuni Mbinu zingine zisizo na Tija kwa Taifa.
Sio kweli mkuu, wengi wakipoteza line hawaendi kurenew wanaona shida kwenda polisi, wanachofanya ni kusajili line mpya kwa id ile ile na wapo hewani kama kawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani watakaowaajiri huko mbeleni Fingerprints zao si zitaendelea kuwa kwenye servers za makampuni binafsi yanayochukua hizo fingerprints leo?.
Watu hawawazi mbali kwa mfano Leo TISS wamenirecruit baada ya kusajili line kwa finger print,

recruitment ya tiss ni endelevu na usajili pia ni endelevu,

Sikh watashtukia data za watu wao wote ziko Washington

Jiulize Ikitokea hizi data zikaangukia kwa wahalifu.

Labda selikali inataka kuwablackmail watu isiowapenda, kwa hiyo itakuwa rahisi kuwabambika jinai kirahisi, kwa kuwatengenezea mazingira ya uhalifu ambayo mtuhumowa atashindwa kujitetea, na mabakama itashawishika na ushahidi hatimaye kumtia mtuhumiwa hatiani, kwa ushahidi wa kuchonga
 
Missile of the Nation,
Huenda walibuni hili ili waweze kutrap mawasiliano ya wanaowahisi wakosoaji bila kujua wanatengeneza tatizo lingine LA kiusalama, kwa kuexpose data za watu kwenye private entities ili iwe rahisi kuwablack mail, kama walivyoitumia Voda kinyume na haki za mteja kuwa trap akina nape na wazee wa CCM
 
Hakuna agent anayesajili line za mitandao tofauti? Kama yupo basi hii theory inaweza kuwa kweli. Anachukua finger prints na details alizomsajilia mtu wa tigo kumsajilia wa voda. Bongo wajanja wengi tusipuuze.
 
[QUOTE="Private investigator, post: 33925226, member: 116521"
Ninazo line mbili mtandao mmoja na hakuna process yoyote nimefata.
Acha uzuzu
Nyie watu hata hamfikirii.... Kwa hiyo ukirudia kuweka fingerprint kwenye kile kidude unasajili mara ya pili.. ? Inamaanisha laini zinakuwa mbili mamba moja...Na vipi zote zikiwa hewani.... Ww ni Muongo.
[/QUOTE]
We jamaa unakichwa kigumu sana
 
Back
Top Bottom