Hongera Mh. Regia Mtema kumgomea OCD

Hongera sana Mhe. Regia Mtema kwa msimamo wako.

Wabunge wote wa Chadema (na vyama vingine wakipenda) wajue wana haki ya kisheria na kikatiba kuwa na mikutano na wananchi kuzungumza na kusikiliza matatizo ili yaweze kutatuliwa.

Kama hakuna hali ya hatari ya uvunjifu wa amani (na hii inatakiwa kutangazwa rasmi na Rais), Mbunge ana haki ya kukutana na wananchi wakati wowote. Taarifa inayotolewa na Mbunge kwa Polisi ili afanye mkutano, sio kuomba ruksa au kibali, bali ni kuomba Polisi watoe ulinzi kusiwe na wavurugaji.

Itafaa wanaChadema viongozi wazingatie msingi huu wa uhuru na haki, wakati huu, ili mabadiliko ya kweli na demokrasia yasimikwe nchini wakati huu wa msisimko.
 
si lazima ,kama Ocd halikubali mkutano uendelee basi hajavunja sheria yoyote,kama mbunge ametimiza jukumu lake la kuwasikiliza wananchi naye yu sawa. Sasa mambo ya kupelekana kwa pilato yanatoka wapi? Ebu tafakari kwanza! Alaf bill of Rights?for what and how for this issue? B constructive bwn!

wewe unamafao na ufisadi au ccm, huu ni mwanzo tu mbona magereza yatakosa nafasi!
 
Domo Zege na wewe umesoma haraka mno hujamwelea Mwanakijiji. Rudi soma tena ndipo utaelewa ana maana gani.
 
Huyu OCd kama kuna mtu anayemfahamu amuulize kama ana knowledge ya computer ajiunge JF itamsaidia sana
 
Nimemkumbuka sana yule mama wa kimarekani, aliekataa kunyanyuka kwenye kiti ndani ya basi kumpisha mzungu akae. Yes, huu ni mwanzo wa mapinduzi!!!
 
kwani angetii amri asingekuwa shujaa au asingekuwa mbunge? .mnashabikia ujinga humu
 
kwani angetii amri asingekuwa shujaa au asingekuwa mbunge? .mnashabikia ujinga humu
Asingekuwa shujaa maana angekuwa ametii kitu ambacho hakifahamu. Angekuwa sawa na polisi ambao wanatii amri yoyote hata ile ambayo ni kinyume cha sheria. Kutotii amri uchwara imeonesha ni shujaa maana alionesha anatetea sheria. Requiescant In Pace! dada Regia!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom