Hongera Dr. Makaidi kwa kuliona hilo.

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487

Binafsi naomba nikupigie saluti ya ukweli kwa kuonesha uwepo wako katika nafasi yako kama mwenyekiti wa vyama vya siasa. Mimi kama mwana mageuzi ningeshangaa kama sekeseke hili lingepita kimyakimya pasipo kulifanyia kazi.

Pamoja na juhudi zako; lakini kubwa lililonifurahisha ni hii kauli yako ya…… “Wapo watu wanaoweza kubeza na wengine wakaona kama Chadema wanabembelezwa. Hapana, katika hali kama hii ni vigumu kuiepuka Chadema katika mazungumzo.

“Kwanza Chadema ndiyo official opposition (kambi rasmi ya upinzani) bungeni. Pia ni chama kikuu cha upinzani nchini, hakuna namna ya kuikwepa.

“Napenda kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wa Chadema wakiitwa na msajili wakubali ombi la msajili ili kumaliza tofauti zilizopo. Kuendelea kubaki na msimamo haitusaidii kama taifa,” alisema.

Nakutakia usuruhishi mwema! Na kwa viongozi wetu wa pande zote tukubali yaishe ila kwa kumwambia huyo Tendwa kuwa hayupo hapo kwa ajili ya CCM tu bali kwa vyama vyote.
 
Back
Top Bottom