Hongera ACT Wazalendo, Hongera Zitto Kabwe Kwa Input Hii Muhimu Kuhusu Bandari na DP World, Serikali Imezingatia Ushauri Wenu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,060
49,744
Nimefurahishwa na constructive criticism ya ACT Wazalendo ambayo mara zote Huwa hawaishii kupinga na kupayuka tuu Bali Huwa Wana offer alternative way.

Nimekuwa nawafuatilia kwenye masuala mengi sana ila Kwa siku za hivi karibuni ni ishu ya Sakata la Bandari na DP World.

ACT Wazalendo hawajawahi pinga uwekezaji Bali walipinga modelity ya uwekezaji wa DP World na wakatoa maoni Yao kwamba Serikali iunde kampuni Shirika ambayo itaendesha Bandari ya Dar.

Bila shaka Serikali baada ya kuchakata iliona ni vyema na ikachukua Ushauri wao na Sasa uwekezaji wa Bandari kati ya Serikali na DP World utakuwa wa ubia chini ya kampuni Mpya amnayo itaundwa Kuendesha Bandari
Screenshot_20231029-163943_1.jpg


Tanzania kama Nchi nyingi zinazoendelea hapa Afrika Zina shida ya kuwa na Vyama vya upinzani vya kulalamika na visivyo na majibu mfano ni Chadema.

Ambae amewahi ona Chadema wanatoa alternative ya jambo wanalopinga na kulaumu,kutukana na kulalamika aweke hapa Ili tujifinze na kuweka rekodi sawa.

Niliona hata kwenye issue ya bima ya Afya iliyokwama ACT walikuja na Mpango mbadala na namna ya kufadhili nadhani Serikali itakuwa imesoma na kusingatia kabla ya kurejesha mswaada wake Bunge la Novemba.Nasubiria kuona.

Ila wale wengine Sasa kama kawaida Yao ni kutukana ,kulalamika,kuponda ,na upuuzi kama huo huku Wakiwa hawana majibu ya nini kifanyike.Vyama kama Chadema zaidi ya kwamba wamebahatika kuwa na ushabiki wa watu wasiojua wanachoshabikia ni hovyo kbaisa.

Chadema wamewahi ongoza Halmashauri kadhaa ila kutokana n kwamba hawana plan Wala hawaelewi wanataka nini hakuna Cha maana wamefanya si ajabu licha ya kupata mabilioni ya ruzuku hawajawahi rudisha hata dawati Kwa jamii kana kwamba shida za jamii haziwahusu wao ni exceptional yaani then watu wajinga wanawashabikia.

Kwa watu wanaotaka kujadili issues na wenye majibu ya matatizo ya jamii basi ACT ni mahala salama kwao.

Binafsi sio Mwanachama wa Chama chochote ingawa zamani niliwahi kuwa Mwanachama wa Chadema nikatoka baada ya kuona Kuna upuuzi mwingi na watu wako after madaraka na ulaji zaidi but ACT inanivutia Kwa kuwa wanajadili issues na wanatoa majibu ila sio Chadema.(Kwa Sasa ni shabiki wa Samia Kwa sababu ni Rais wa issues sio porojo,anasimamia mtizamo wa sera za Uchumi na biashara nazozihusudu).

ACT Wananivutia ngoja niendelee kuwafuatilia zaidi ila wale wanaopenda bendera fuata upepo ushabiki mbuzi waendelee kubakia Chadema maana huko ni kama Simba na Yanga no reasoning,mara mia hata CCM wakikosea Huwa wanaambiana ukweli na kujirekebisha.

Si ajabu hata wanaharakati wamewaona Chadema ni miyeyusho na kuachana nayo Kwa sababu ya Utapeli wa Kisiasa Wana capitalism kwenye ujinga wa watu wengi.

Chadema Kwa Ukubwa wenu ilitakiwa muwe na majibu ya Changamoto.Katiba Mpya haileti Ugali mezani Wala haikuzi uchumi.Chama Cha Siasa ambacho hakina majibu ya kile wanacholaumu na kukosoa ni sawa na kikundi Cha matapeli wa Kisiasa.

View: https://twitter.com/zittokabwe/status/1718854935075311868?t=pc-JbTpjYlM7583_gG3tcQ&s=19
 
Nimefurahishwa na constructive criticism ya ACT Wazalendo ambayo mara zote Huwa hawaishii kupinga na kupayuka tuu Bali Huwa Wana offer alternative way.

Tanzania kama Nchi nyingi zinazoendelea hapa Afrika Zina shida ya kuwa na Vyama vya upinzani vya kulalamika na visivyo na majibu

Niliona hata kwenye issue ya bima ya Afya iliyokwama ACT walikuja na Mpango mbadala na namna ya kufadhili nadhani Serikali itakuwa imesoma na kusingatia kabla ya kurejesha mswaada wake Bunge la Novemba.Nasubiria kuona.

Kwa watu wanaotaka kujadili issues na wenye majibu ya matatizo ya jamii basi ACT ni mahala salama kwao.
Naunga mkono hoja kuhusu ACT, Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The Underdogs, Huwezi Kuwapuuza na kuhusu upinzani Tanzania, niliwahi kuendesha darasa kadhaa humu ikiwemo Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane! na pia Japo kazi ya upinzani ni kupinga, lakini sio kupinga kila kitu. Kwenye maslahi ya taifa, tutangulize utaifa, tuwe wamoja, wakweli na tusipotoshe

P
 
Duh!
Dah!
Duh!

Ukirudia haraka haraka utanielewa na utamwelewa Makonda.

Zama za kupotosha zinaenda kupigwa stop. Wangalau kwa muda huu wa Probation.
 
Kiufupi hao Chadema naona wamewekeza kwenye sheria Kwa sababu Wana siasa za confrontation na Serikali na sio siasa za majibu Kwa Changamoto za Jamii.

Sasa sijui lengo lao ni lipi bila kuwa na ajenda mbadala yenye kuleta majibu ya kile wanacholaumu na kukosoa.
 
Kule migodini ACACIA, Kampuni ya Twiga, mlishapata mgao hata wa Shs 100?
 
Hizi sifa za kinafiki kwa ACT zina lengo la kuwapumbaza chadema ili nao wawe wanafiki kama Zitto group (ACT).
 
Hizi sifa za kinafiki kwa ACT zina lengo la kuwapumbaza chadema ili nao wawe wanafiki kama Zitto group (ACT).
Hizi sifa za kinafiki kwa ACT zina lengo la kuwapumbaza chadema ili nao wawe wanafiki kama Zitto group (ACT).
Kwanza Bora hata msiandike mnachafua Uzi Kwa ujinga wenu.

Hii hapa tofauti ya Chadema na ACT Wazalendo nayoizungumzia,soma upate Madini sio kupayuka hovyo

View: https://twitter.com/zittokabwe/status/1718852406891389112?t=_ciySkm7tJECFfCIR_YVXQ&s=19
 
Back
Top Bottom