Homoni za Testosterone kwa Wanaume

Jun 5, 2023
12
28
๐—›๐—ผ๐—ฟ๐—บ๐—ผ๐—ป๐—ฒ ๐˜†๐—ฎ ๐—ง๐—˜๐—ฆ๐—ง๐—ข๐—ฆ๐—ง๐—˜๐—ฅ๐—ข๐—ก๐—˜

Kichocheo hiki ndio silaha ya mwanaume kwani ndicho kichocheo ambacho kinakufanya uwe na sifa zote za kiume na ndicho kichocheo ambacho kinakufanya uwe imara katika tendo la ndoa na tezi dume pia.

Hii ni homoni muhimu katika afya ya mwanaume ambayo husaidia kurekebisha mood, kuongeza kumbukumbu, uwezo wa kufikiri , na pia kuimarisha misuli na mifupa mwilini..

Upungufu wa kichocheo hiki kinasababisha kupungua kwa matamanio kwa jinsia tofauti,kupungua kwa nguvu za misuli yako kiutendaji,mafuta kurundikana ovyo mwilini( BELLY FAT AND OBESITY) na hata Matatizo kwenye Viungo au mifupa.

Kadiri umri unavyoenda mbele basi kiwango cha uzalishaji wa kichocheo cha testosterone hupungua, Na kutokana na mtindo wa maisha ulivyobadilika kupungua kwa kichocheo hiki huanza baada ya miaka 30 na kuendelea,
Sasa kupungua kwa uzalishwaji wa kichocheo hiki huambatana na:
Ukuaji wa tezi dume (prostate gland),
Kupotea kwa nywele
Kupungua Uzalishwaji wa Mbegu
Kupungua uwezo wa misuli ya Uume kusimama imara
Na pia hupelekea kuanza kwa maambukizi ya awali ya saratani mfano saratani ya tezi dume.

Ili kuhakikisha uzalishwaji wa kichocheo hiki cha kiume unafanyika vyema jitahidi Kufanya yafuatayo:

- Kula vyakula vyenye zinc kama pweza, Mayayi, karanga, korosho, maziwa, mbegu za mboga, vitunguu swaumu nk.

-Fanya Mazoezi ya nusu saa Walau mara Tano Kwa wiki.

- Kula samaki kama salmon mwenye vitamin D3

Tunajua kwamba ni vigumu Kupata Lishe bora kutoka kwenye Vyakula vyetu vya Kila siku, toka vikiwa shambani utumiaji wa mbolea zenye kemikali, Tunaweka Vyakula kwenye friji Kwa muda mrefu pia vinapelekea Upungufu wa Virutubisho ndani ya miili yetu.
IMG_20230515_154307.jpg
 
Kivipi chakula cha kwenye fridge kinapungua virutubisho?
Hii Ni kwasababu Uhifadhi wa vyakula kwenye jokofu hasa kwa muda mrefu unaweza kusababisha baadhi ya bakteria kuzaliana na kusababisha kupata madhara ya kiafya kama vile kuhara na magonjwa mengine.

Chakula pia huweza kupoteza virutubisho vyake na husababisha mazalia ya bakteria kwenye chakula hicho

Naamini ume gain knowledge kiasi mkuu
 
Hii Ni kwasababu Uhifadhi wa vyakula kwenye jokofu hasa kwa muda mrefu unaweza kusababisha baadhi ya bakteria kuzaliana na kusababisha kupata madhara ya kiafya kama vile kuhara na magonjwa mengine.

Chakula pia huweza kupoteza virutubisho vyake na husababisha mazalia ya bakteria kwenye chakula hicho

Naamini ume gain knowledge kiasi mkuu
Bacteria wanazalianaje kwenye baridi kali?? Maana tunaweka kwenye fridge ili visiharibike
 
Back
Top Bottom