Home Work hii imenitoa jasho....msaada!!

Mtoto wa jirani (miaka 5 anasoma chekechea) kanijia asubuhi akaniambia eti nimtafutie CHAWA na KUNGUNI ajue jinsi walivyo. Anasema wamefundishwa ubaya wa hao wadudu na wameambiwa kila mmoja awatafute aone wanafanana vipi, alivyowauliza wazazi wake wakamwambia aje kwangu. Nimemwambia nitamletea kesho na kumuonyesha namna walivyo. Msaada namna ya kuwapata kwa urahisi hao wadudu.....
uwanja wa fisi kuna gest inaitwa 'mlango wazi' nenda hapo utawapata kibao.
jana waliniuma kweli aisee.
 
Wale wenye nywele ndefuuu afu wanakula pilipili sana huwa wanazo, katiza mitaa ya kariakoo tu.
 
mkuu wazazi wake wamemwambia aje kwako?
Wewe una chawa?
Una kunguni? Tooooooooooooooooooooobbaaaaaa
 
Wale wenye nywele ndefuuu afu wanakula pilipili sana huwa wanazo, katiza mitaa ya kariakoo tu.


halafu wanapenda kupaka mafuta ya maji (ya nywele)
wakichana nywele zinang'aa kwa mafuta, halafu mayai ya chawa yanajitokeza meupe meupe hadi raha...........
 
Mkuu unashotakiwa kufanya ni kufngua tuition center afu uwalipishe kama kawa.
Kwani kuwafuga mchezo, si lazima uwe na roho ngumu kuishi nao. hicho ni kipaji, fungua center uongeze mapato!
 
Tafuta nyumba nyingine uhame,ipo cku atajisaidia kwenye poti aambiwe alete kwako!washakuchoka hao swaiba!
 
sasa si uingie kwenye mtandao uwatafute then muonyeshe picha..sijui kama kuna boarding schools zenye kunguni siku hizi
 
sijapenda dharau za hao wazazi wa kijana!anyway kazi unayo kwa vile KUNGUNI NA CHAWA ni miongoni mwa viumbe hai vilivyo ktk hatari ya kutoweka duniani!-source mimi mwenyewe!
 
Nenda pale HOSTEL ya MAKONGO SEC. wako kunguni wa kumwaga.
MAPROSPOO.
 
mahaitaji ya kutengeneza chawa

1. maji kidogo
2. karatasi jeupe amabalo halina maandishi yeyote
3 uchafu utokaomwilini

njinsi ya kufanya
1.chua maji na kisha upake kama mafuta kwenye mwili wako af sugua na utapata uchafu mweusi
2. chukua huo uchafu uuweke kwenye karasi jeupe
3. funga karatasi vizuri na uiweke sehemu yenye giza sana
4.fungua karatasi hilo baada siku saba
5. chawa watakuwepo wa kutosha na utatatua homework uliyonayo
 
Mimi kilichonivutia kuliko voote ni kitendo cha wazazi kuona wewe ndio wafaa kutoa majibu ya hio homework....lol
 
Chawa kwa kiengereza anaitwaje niko na mtaalam hapa kutoka mbele anaweza kukusaidia nimestuck kwenye jina ??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom