Home Shopping Centre wazusha taharuki Kariakoo

Natoa pongezi kwako Mhe.Mwakyembe, endelea kusukuma huo mkakati ili makusanyo ya Bandari yawe halisi, maana hao TRA wenyewe wameshajipambanua wako sambasamba na wakwepa kodi. Ktk mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Makamishina wa TRA na Forodha, Makampuni ya Wakala na Wafanya biashara wa Kariakoo, mmoja wapo wa wasemaji kwa niaba ya Wafanya Bishara wa Kariakoo alibainisha kuwa hawana tatizo na TRA, wanakwenda nao sawa. Hata Kitilya ameagiza wapewewe mizigo yao. Lakini mtinndo huo hsc si wao peke yao, wako wengi sana wanaoendesha huo ufisadi wa kukwepa kodi kwa kusaidiwa na TRA wenyewe.
 
kama ni kweli anakwepa kodi,sheria ichukue mkondo wake,bz anaidhulumu nchi na wananchi wake.
 
Sio wivu ni jamaa wanakwepa kodi pengine nawe unanufaika unaagiza vitenge doc unaandika tooth pick

Hawa jamaa ni wahuni wa siku nyingi! Kuna mmoja wao aliua mtu kariakoo na kesi ikaisha hivi hivi. Sijui kama watawaweza kwani wanalindwa na familia ya Kikwete
 
Duh kumbe ni kweli, kuna mtu nilipingana nae sana. Kuna mzigo ulikua tuuchukue China to Dar but ushuru tukaona utakua mkubwa sana basi mshkaji Fulani akanitonya kuwa niwatumie hawa jamaa issue itaenda uzuri.....baadae nikaghairi. Kumbe ni kweli wanapiga issue
 
Huu ni umbea mwingine HSC ilikuwapo kabla hata mkuu wa kaya unayemsema kuingia madarakani na walikuwa wapo vizuri ile mbaya jamaa wamejipanga wanapiga kazi na ndio mana wanasikikafanyeniresearch na muache kurukia habari nendeni TRA mkacheki wanalipa kodi zote VAT, MAPATO,PAYE,NSSF etc kwa muyjibu wa sheria acheni chukibinafsi watanzania tufanye kazi..

Kuna deliberate effort ya kuhakikisha kuna bonge la ukuta baina ya rais na mwananchi wa kawaida. Sijui kama Mh. Rais analiona hili. Poor guy anajitahidi kufanya mambo lakini feedback inakuwa negative matokeo yeye anaona ameplay part yake ila wananchi wakorofi na huku chini sisi wananchi tunaona anatudharau. There is a serious communication breakdown between the government and the wananchi that needs the his direct and immediate attention!
 
Kimondo umepita kama upepo huku povu limejaa, hongera nape kakuona leo una buku saba
 
Hapa tatizo si mawakala wala TRA, tatizo ni serikali kuwaacha TRA kujipangia viwango vya ku-report mapato (makusanyo) ya kodi kila mwezi. Who's the watchdog?
 
Duh kumbe ni kweli, kuna mtu nilipingana nae sana. Kuna mzigo ulikua tuuchukue China to Dar but ushuru tukaona utakua mkubwa sana basi mshkaji Fulani akanitonya kuwa niwatumie hawa jamaa issue itaenda uzuri.....baadae nikaghairi. Kumbe ni kweli wanapiga issue

Jamaa hawa wanafaidi nchi kwa kukwepa kodi wakitoa mzigo wanakuletea wao wenyewe mpaka mlangoni
 
Baada ya kuiona hii habari kwenye source ya kuaminika kama ITV na kulinganisha na tangazo la mkutano wa Waziri wa Fedha Dr. Mgimwa naanza kuamini kuwa hapa hakuna uzushi.
Halafu hapa sio mambo ya kuishia kwenye mikutano sijui na waziri au nani maana hawa jamaa nasikia wameshajenga mtandao mpaka ndani ya taasisi kama TRA kuna hadi mameneja wanawatumikia wao, kampuni za meli nasikia wanachukua meli nzima kwa hiyo hata wizarani huenda wana mtu wa kuwasimamia.
Kwa maana hiyo wale wasiopenda mchezo wao wasidhani itakuwa kazi rahisi kuuvunja huu mtandao lakini kama kweli nia ipo itafanikiwa.
Kampuni ambayo ilitoa msaada wa kujenga shule ya waanga wa Mabwepande kwa 800m na mkuu wa mkoa ananyenyekea huwezi jua mkono unaowalinda unaanzia wapi.

ITV Tanzania
Liked · 18 hours ago
Zaidi ya wafanyabiashara elfu mbili wa Kariakoo wameazimia kufunga biashara na kuandamana kutokana na kuzuiliwa kwa bidhaa zao toka China kwa zaidi ya miezi miwili katika bandari ya Dar es salaam baada ya baadhi ya mawakala wao walioainishwa na serikali kubainika wanakwepa kulipa ushuru.
 
Wadau,kuna habari za uhakika chini kutoka kwa wadau wangu wa karibu kuwa hali ya mfanyabiashara said wa home shopping center si nzuri kibiashara...
kama thread moja iliyowahi kuandika habari zake humu ndani,inasemekana zaidi ya makontena 860 yamezuiwa bandarini kwa kile kinachoelezwa kufanya uchunguzi zaidi,mengi ya makontena haya yamewekwa bidhaa nyingine huku documents zikionyesha bidhaa nyingine.

hv karibuni amekuwa na ugomvi na mfanyabiashara mwingine Said salim bakhresa,na pia ameshagombana na Manji na yule muhindi mwingine tajiri zakaria,pia amekorofishana na subhashi Patel pale alipoanza kuingilia biashara ya mabati yanayofanana na ya kiwanda cha subash.

kuna wachina kama mia mbili hv nao mizigo yao iko kwenye hiyo ya huyu bwana so sad,kumbe na wao wanakwepa kodi

ukwepaji kodi huu wa Said,unajulikana wazi na kila mtu,hata serikalini,sijafahamu hasa kwann this time wameamua kumgeuka mwenzao! labda ndio yale maneno ya magufuli kuwa anaeweza kumtoa ni rais tu,maana huyu jamaa keshahamisha maafisa wa tra kama mia na hv!

my take:crime doesn't pay

Bado sijaona mtu wa "KUMFANYA KITU" huyu jamaa!
 
Jamani habari ya Said si ya uongo, kwani wafanyabiashara wote wa kariakoo polisi na TRA wakiwakamata na mzigo wakisema mzigo huu unatoka kwa Said wanaachiwa lakini wakisema vinginevyo sero ya msimbazi polisi ya kwako au utoe rushwa ndevu, manake wakubwa wote wanajuwa habari za said, kwa hiyo inawalazimu wafanyabiasha wote kariakoo kumtumia Said kutoa mizigo yao Bandarin ili kukwepa kodi, Pili kiwe kizingiti wakikatwa na polisi au TRA.Saidi alipoandaa sherehe mwaka juzi je ni mkubwa gani wa nchi hii hakuwepo? au kutuma mwakilishi? na kupokea bahasha nononono.... anayejua aseme, Said yupo juu ya sheria nashangaa kwanini wamemsaliti?
 
HSC wanakampuni kibao za Clearing bandarini pale, wafanyabiashara wanalazimika kuwatumia hawa jamaa kutokana na kuwa na mkono TRA na wakubwa wa wizara ya fedha. Ukijifanya unatumia kampuni nyingine kwa wafanyabiashara wa nguo, viatu, pazia na vinginevyo utapigwa ushuru wa kufa mtu. Ila ukitumia HSC container la nguo au kitenge unalipa mil.28 tunaambiwa jamaa yeye anacheza na wakubwa wa TRA anasema container lina Tooth pick au toilet paper yeye analipa TRA mil.7 dah kumbe zigo linathamani ya dola 170,000/= ishu ya Mwakyembe kuanza kukagua container imeanza kumuumbua bwana HSC na wakubwa wa TRA imesababisha taharuki kwa wafanya biashara k.koo mizigo imezuiliwa na biashara imesimama. Serikali imepoteza sana mapato juu ya hawa jamaa HSC wanakula pia na polisi wanasindikiza toilet paper kumbe nguo au vitenge au tv au friji.

TUWE MAKINI NA KINACHOENDELEA TATIZO SIO HOME SHOPPING CENTRE WADAU

Kiukweli inasikitisha sana kuona watu wachache wanaosaidia wanyonge wanachukiwa kwa misingi yao ya kibiashara
mimi ni CHADEMA FOR LIFE ila kwa hili CCM haihusiki na watendaji wanamtia aibu MH.Jakaya hapa kuna mambo matatu.
1.Kariakoo ilishakuwa Dubai ya nchi zote kongo, burundi, zambia, malawi, rwanda! Leo wanaenda uganda na kenya
2. Kodi itapungua, ajira itapungua, sisi hatujasoma tutaenda wapi
3. Nchi hii wabaya sio viongozi, wabaya watendaji! Na sisi tukiumia chuki zote kwa viongozi na ccm wao hata ikija chama kingine watabaki tu.

Mkutano ulioitishwa na waziri kuhusiana na kukwama mizigo bandarini ni kutokana na bidhaa kuwekewa kodi kubwa sana ambazo hazilipiki mizigo iliyokwama sio ya HSC ni wafanyabiashara mbalimbali na mkutano uliwahusu hao wadau wote hali ni mbaya...
tuliyoyashuhudia katika mkutano huu ni kama yafuatayo nilihudhulia kama mfanyabiashara niliyeadhirika na hili
A. Sisi wafanyabiashara ndio tunaoumia na kulipa kodi kwa mizigo inayoingia nchini lakini ajabu kubwa ya kutoa maoni walipewa mawakala wa forodha kuongea badala ya sisi wafanyabiashara ambao ndio waadhirika wakubwa wa ucheleweshwaji huu, ambao kwa kiasi kikubwa pia unawaadhiri wafanyabiashara wadogo na wananchi wa kawaida ambo bidhaa zetu ni kariakoo sehemu ambayo hao makamishna na mawaziri hawaji kununua chochote mambo yao ni ulaya na maduka makubwa huko posta kariakoo yetu hawaijui.
B. Mawakala wa forodha katika mkutano huu badala ya kujikita kujadiri sababu za msingi zinazosababisha mizigo ichelewe kutoka bandarini wao walitumia muda mwingi kushambuliana wao kwa wao kuhusu nani anapata kazi nyingi (vita ya kibiashara) jambo ambalo halikuwa lengo la mkutano huu na wala hatudhani mizigo kuchelewa kutokana na kampuni moja kupata kazi nyingi kuliko nyingine bali ni matatizo ya kiutendaji kwa hili Mh.waziri hakuambiwa ukweli kabisa mi naomba afike kariakoo ajioneee mwenyeweee.\

NB: Kilio chetu kama wafanyabiashara kuhusu ucheleweshaji wa mizigo ni suala la uthaminishaji mizigo (valuation) ambao maafisa wa TRA wanaweka bei kubwa sana kuliko ukweli kusababisha kodiinayotolewa kuwa kubwa kiwango ambacho hakilipiki.
 
Jamaa hawa wanafaidi nchi kwa kukwepa kodi wakitoa mzigo wanakuletea wao wenyewe mpaka mlangoni

Dunia ya sasa hata ukienda nchi za wenzetu hawahangaiki kuna service inaitwa Door to Door delivery hata bongo ipo na waanzilishi walikuwa home shopping centre wakaja furniture centre leo hii hata pizza unaletewa mlangoni hivi hapa kunatatizo gani kama mtu kaamua kuwajali wateja wake na hapa ndio watanzania wanachemka wengi hawana customer care wala si wabunifu hata kidogo. BIG UP HOME SHOPPING CENTRE... WADAU DONT HATE THESE GUYS WANAENDELEA KWASABABU WANACHAPA KAZI WE ALL HAVE 24HOUR SO DONT HATE THEM tufanye kazi....
 
Baada ya kuiona hii habari kwenye source ya kuaminika kama ITV na kulinganisha na tangazo la mkutano wa Waziri wa Fedha Dr. Mgimwa naanza kuamini kuwa hapa hakuna uzushi.
Halafu hapa sio mambo ya kuishia kwenye mikutano sijui na waziri au nani maana hawa jamaa nasikia wameshajenga mtandao mpaka ndani ya taasisi kama TRA kuna hadi mameneja wanawatumikia wao, kampuni za meli nasikia wanachukua meli nzima kwa hiyo hata wizarani huenda wana mtu wa kuwasimamia.
Kwa maana hiyo wale wasiopenda mchezo wao wasidhani itakuwa kazi rahisi kuuvunja huu mtandao lakini kama kweli nia ipo itafanikiwa.
Kampuni ambayo ilitoa msaada wa kujenga shule ya waanga wa Mabwepande kwa 800m na mkuu wa mkoa ananyenyekea huwezi jua mkono unaowalinda unaanzia wapi.


KWELI TUNAKURUPUKA
Mimi kama mdau katika hili naomba nichangie
tunachallenge kubwa sana hapa wafanyabiashara wanatumia makampuni mbalimbali na tunajua kampuni zote hapo nyuma bei za kodi zilikuwa sawa tu hakuna kampuni iliyokuwa ikitozwa eti zaidi kuliko nyingine, hii ni kumdanganya waziri kwa nia ya ushindani wa kibiashara kama kweli kuna kamouni yenye nyaraka zinazoonyesha kulipa kodi kubwa kuliko nyingine si wazitoe kwa bidhaa zilezile TRA siku zote ilikuwa ikitoa bei sawa.
na wanachokilalamikia wafanyabiashara wa kariakoo ambao wengi ni wanyonge ni mizigo yao na si HSC kwa sababu wengi wanatumia makampuni kibao tofauti 1. Watu wamefikisika na wengi wamekufa, benki zinatudai, pride marejesho yanatubana.Yuko mfanyabiashara amaekufa kwa madeni kajirusha ghorofani, yupo..... Kafa kwa presha, yupo ........... kafa!

Watu wanafanya utani wanaita vikao kwenye viyoyozi wanamdanganya waziri sisi tunakufa juani kariakoo viongozi fanyeni kazi zenu ushindani wa kibiashara waachie wao mkiingilia kwa maslahi yenu hilo silo lililowapeleka hapo kama hamuwezi pisha wenye akili zao waingie wafanye kazi nendeni kariakoo mkajioneee kama mnandugu waulizeni maana nyie kariakoo hampajui shopping zenu ulaya mnatuona hatufai sisi..
 
ujambazi hautokwisha chini ya serikali ya ccm. sakata hili muhusika mkuu ni jk, mtoto wa jk ndio kiungo mkubwa wa biashara haramu za hawa wa yemeni chotara, jk na mtoto wake walivyo na akili ndogo wamemchagua mmiliki wa kampuni hii kuwa balozi wa tanzania uchina,wakati kuna akina mangi meli pale wana sifa kedekede wameachwa. ujinga huu hautokowisha hadi ccm iondoke madarakani. chadema kwanza hakuna msafi ccm
 
tra ndo wamewashtukia hsc na kuanzia mwezi huu container zote zinakaguliwa (physical verification) na hih si kazi ya wizara ya uchukuzi, ni kazi ya tra wenye dhamana ya kukusanya kodi na ieleweke tra wapo chini ya wizara ya fedha, na kamishana wa tra amekvwa akilalamikia sana swala la hsc kupewa direct release ya container toka wizara ya fedha(serikali kuu).
Ni hivi majuzi tu hsc wamekamatwa kwa kwa kukwepa kodi zaidi ya 800M
Na hii si kwa hsc tu wafanyabiashara wengi wa kariakoo kama si wote wanatabia ya kudeclare vitu tofauti na walivyobeba au pungufu ili kukwepa kodi.
Takwimu zinaonyesha kuwa vitu vinavyokuwa declared tra sivyo vivivyopo sokoni.
Nenda idara ya forodha inayohusika na utoaji wa takwimu za bidhaa zinazoingia nchini uolinganishe na kiwango cha bidhaa yilizopo sokoni!
Na hii ndiyo sababu ya kufungua makasha (container)
 
kinacho lalamikiwa na wafanya biashara k/koo nini na tunacho jadili ni nini? sipati picha ya hili jambo?
wafanya biashara wao wana dai mizigo kucheleweshwa au wanadai ushuru mkubwa au wana mlalamikia hsc?
wakiandamana kesho wata andamana kudai kupunguziwa ushuru au wataandamana hsc ifungiwe ?
tutafakari kabla ya kuchukuwa hatuwa sipati picha ya hili suala ninaomba kujulishwa madai ya wafanya biashara wa kariakoo ni nini?
 
HSC wanatumia frusa waliopewa na Serikali ya ccm,kukwepa kodi.

ccm ndio inayofuga ujinga huu, je tungekua na serikali makini mtendaji gani wa Serikali angekula rushwa.?

Tatizo serikalini hakuna mwadilifu, ndio maana mtu badala ya kuwajibishwa tunaambiwa ni upepo utapita.

Dawa ni kuikataa ccm kwa nguvu zote.!!
 
Back
Top Bottom