Hoja za Uislam ni hoja binafsi,tunachotaka bandari yetu isiuzwe,full stop.

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,872
Kwa hakika hoja za Uarabu, Uislamu na Ukristo zilizotolewa katika suala la mkataba danganyifu wa bandari ni hoja binafsi ambazo hazina mashiko katika suala la uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Pia Uzanzibari, Utanganyika ni hoja binafsi, tunachotaka bandari yetu isiuzwe,full stop kama itathibitika mahakamani wapo watu walidhamiria kuiuza bandari yetu basi washtakiwe kwa mujibu wa sheria.
 
Wamishemishe za bandarini naona mmekomaa, kitumbua kinaingia mchanga
Wapi wameandika inauzwa?
 
hoja za Uarabu, Uislamu na Ukristo zilizotolewa katika suala la mkataba danganyifu wa bandari ni hoja binafsi
Ila la Uarabu lina mashiko. A spade is a Spade. piga ua, lina mashiko...documented!
uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Pia Uzanzibari, Utanganyika ni hoja binafsi
Ipo siku watasema wenyewe. Kibinafsi. Uzanzibari na Utanganyika ni hoja halali
hazina mashiko katika suala la uwekezaji
Kitu ambacho sijasikia ni tafsiri ya "Mwekezaji'" katika mijadala hii....hatahivyo, inaashiria mtu wa nje, Mzungu, Mwarabu, mhindi, mchina, n.k Hivi Mwafrika sio mwekezaji? ......
tunachotaka bandari yetu isiuzwe,full stop
Isigawiwe, kuuzwa ninkitu kingine, isigawiwe na hata ikiuzwa(msithubutu) tulipane mumuhumu Tanzania!
walidhamiria kuiuza bandari yetu basi washtakiwe kwa mujibu wa sheria.
Yani Shika, kamata, garagaza, peleka mahakamani, funga, fukuza! Ikibidi Rudia mpaka kieleweke

Pana taka hizo!
 
Kwa hakika hoja za Uarabu, Uislamu na Ukristo zilizotolewa katika suala la mkataba danganyifu wa bandari ni hoja binafsi ambazo hazina mashiko katika suala la uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Pia Uzanzibari, Utanganyika ni hoja binafsi, tunachotaka bandari yetu isiuzwe,full stop kama itathibitika mahakamani wapo watu walidhamiria kuiuza bandari yetu basi washtakiwe kwa mujibu wa sheria.
Asilimia kubwa ya wanaopinga mkataba (IGA) Hawapingi mkataba (IGA) wa bandari, kwakua ili kupinga mkataba, ni lazima uanze na sheria zitakazo ongoza mkataba kwanza, kabla ya yaliyomo, kwakua yaliyomo ni lazima yafuate sheria. Hii ni kama tu unataka kupinga kwa nia njema ya taifa. Usipofanya hivyo nisawa na kuchukua maneno, na mistari miwili kwenye vitabu vitakatifu ili iendane na haja zako. Waingereza wanaita hali kama hiyo “ulterior motives”

Kuna msukumo mkubwa kwa wanaopinga lengo Lao kuu ni wanapinga Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 🇹🇿 kuwa HURU kimapato kwa mara ya kwanza. Usione ajabu, Kaskazini wanakua na mtazamo tofauti wa mambo na sio dhambi. Hata Mangi Mkuu Mangi Marialle alipingana na Mwl kuhusu Tz kupata uhuru 09 Dec 1961, aliona muda haijafika kwanza, hatuna uwezo wa kujiongoza Bado.

Lakini Uhuru uliletwa na TANU, ambayo leo inaitwa CCM, baada ya kuugana na Afro Shirazi (ambacho likua na wapini Znz) 1977, na Kila mtu amefaidika kutokana na hilo.

unaweza kuiangalia South Africa 🇿🇦 Kijuju ukadhania bora tungechelewa kidogo kupata uhuru kama ulivyokua mtazamo wa Mangi Mkuu Mangi Marialle, japo alikua hapatani na mmoja wa mangi wadogo, mangi Shangali.
Laking Uhuru ni sasa, alisisitiza Mwl, na njia aliyofanikisha kutupitisha ndio tunaendelea nayo Leo.

Hili Jambo ni kubwa kiasi kwamba haliwezi kuwa na mkataba (IGA) mmoja wenye kurasa 38 tu, lazima iwepo mengine, pia ya kupenda na na makubaliano kati ya Tanzania 🇹🇿 na Dubai. Kuku, mbuzi, nguruwe, ngombe, ni nyama, kama vile IGA, HGA, na PA(s) yote ni mikataba, lakini nyama zote ziko Sawa? Mikataba yote iko Sawa?
Watu wanajua tofauti Za nyama, ila kutokana na shughuli zao Za Kila siku sio wote wanajua tofauti ya tofauti ya IGA, HGA, na PA(s).
Kutokua kwao usikutumie kwa faida yako kama wewe ni kiongozi wa kweli.

ukiiangalia kipengele cha 21, kipengele pekee pekee kinachoelezea sheria zitakazo ongoza mkataba, kwakua yaliyomo yote lazima yaendane na sheria.

Kimsingi tafsiri ya mkataba ni makubaliano yanayoweza kulazimishwa na sheria.

Sheria gani sasa zinaweza kulazimisha hayo makubaliano?

Jibu liko kipengele cha 21, kwamba IGA itafuata sheria Za uingereza ambazo tunazifuata tayari, zinafanana na Sheria zetu, kwakua tumezirithi kutoka serikali iliyokuwepo kabla ya 09 Dec 1961. Kipengele cha 21 pia kinasema HGA na makubaliano ya mradi yatafuata sheria Za Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Na sheria Za Tanzania tunaweza kuzibadilisha tunavyotaka bila na mkataba (IGA) inatambua hilo, na kukiri hilo. Hii inakua muhimu kwenye mapato. Ndio maana mapato hayamo kwenye IGA, yatakuwepo kwenye HGA ili yafuate sheria Za Tanzania, na hapo ndipo Prof Mbarawa, wanalinda maslahi, ya wa Tanzania, kwamba mapato yangekuwepo kwenye IGA, tusingekua na control nayo. Badala ya kufurahia hilo wanaliruka, hakuna anayepinga anaweza kukataa ukweli huu.
 
Back
Top Bottom