Ronn M
JF-Expert Member
- May 2, 2012
- 1,279
- 683
Tumedanganywa mengi. Kwanza walikuja na Tanzania yenye neema kwa kila mmoja inawezekana. Wakatupigisha wimbo wa maisha bora kwa kila mtanzania! Wakatudanganya kuhusu EPA, DOWANS NA RICHMOND! Mpaka leo tunadanganywa kuhusu meremeta! Naam, wakatudanganya kiwira. Wakatudanganya kuwa matatizo ya nchi yetu yanasababishwa na kuyumba kwa uchumi wa dunia. Mara ni kupanda kwa bei ya mafuta. Tena mkulu akatudanganya kuwa hajui kwanini sisi ni maskini. Akatudanganya na kilimo kwanza. Akatudanganya kwa mbwembwe za mpango wa miaka mitano. Loh, mengi kweli! Hata kigoma kuwa Dubai ya Afrika tumedanganywa! Na sasa hii sinema ya Kova na Joshua wake! Loh! Kweli dhaifu! Sasa tatizo si la wadanganyaji bali wadanganywaji! Hata lini itakuwa hivi? Chukua hatua, liwalo na liwe!