Mimi ni mkristo na tangu awali nilijua kuwa ZK ni mwislam, nilimpenda sana kijana ZK hapo alipojitokeza kama kijana shujaa hadi hapo alipoanza kuyumba na kuonyesha tabia za kihuni katika CDM. Hata mleta hoja unajua kuwa zito kama ameonyesha udhaifu mkubwa huu akiwa ktk cheo cha unaibu katibu mkuu wa CDM na mbunge, hivi akiwa sasa ndo m/kiti wa chama mambo yatakuwaje!!!!! Na hapa tuondoe ushabiki wa kumchukia au kumpenda kijana ZK kwa namna yoyote ile.
Kijana wangu ZK ni nani aliye kuloga au umepatwa na nini? ulianza aktika kuaminika sana na unamalizia katika kutiliwa mashaka na umma mkubwa wa wapenda mageuzi. yanayojitokeza na yanayowekwa wazi juu yako yanatuhuzunisha sana kuwa sasa ZK umebadilika na umekuwa siye shujaa yule... angalia wapi umeanguka ukauacha upendo wa kwanza ukatubu na Mungu atakupa nguvu tena kama mwanzo na watanzania nikiwa mmoja wao huenda tutakuamini tena.
Safari ya mabadiliko mtoa hoja siyo ya nani awe m/kiti wa CDM ni zaidi ya hapo. Hata mimi naweza kuwa m/kti muhimu ni Watanzania kuelewa Haki zao na kuziendea kwa namna yoyote ile.
Kama wewe ni msomi kama unavyodai ebu mfanyie ZK na wewe menyewe SWOT analysis halafu uache kutaka nani ( au ZK) awe m/kti wa CDM maana siyo hoja kuu
Nimesikitishwa sana na mawazo finyu eti ndo ya great thinkers....!!!! ZK awe m/kti wa CDM!!!!
Suala siyo udini wala ukabila ni tamaa ya kutotaka kutulia na kujifunza na kujua kuwa kila jambo lina wakati wake chini ya jua.
Nikisoma vizuri between the lines naona kabisa husemi ukweli kuhusu ZT, unajidai tu..no evidence