Hofu yatawala Siyoi Sumari kukatwa na CC-CCM

Meru ni tofauti na Masaini, kule Meru kuna utawala wa kifalme, kwao mbunge ni mfalme na akifa mwanae ndio anatawazwa mfalme.

Baada ya CC ya CCM kumpitisha Sioi leo, basi uchaguzi Arumeru utakuwa ndio umemalizika rasmi!. Kitakachoendelea ni kutimizwa tuu kwa matakwa ya kikatiba na kusubiri kumtangaza rasmi!.
Kwa hiyo Mkuu unataka kutuambia kwamba Marehemu Sumari alirithi ubunge toka kwa baba yake??
 
Siasa za tz bwana! Hv kuna mtu anataka kujua kuwa hawa watu wanasiasa za aina gani, uelekeo gani misimamo gani, malengo gani,
au hayo si muhimu?au maamuzi ya chama hayahitaji kushare na wananchi wengine misimamo ya wagombea wao?
 
Mnamuona Sioi tuu, mbona Adam Malima ni jimbo la baba yake, Dr. Mwinyi, Vita Kawawa etc, hata Fred akijenga political interest atarithishwa Monduli wakati Mzee akielekea Magogoni!.

Na sio Tanzania tuu, Mnajua Odinga alitokea wapi?, Uhuru Kenyata nae?. Mnaujua mpango wa Museveni?. Kama mlidhani ni Karume baba na Karume mtoto tuu, au ni Mwinyi baba na Mwinyi mtoto tuu!. Subirini mshuhudie atakayechukua fomu ya ubunge wa Bagamoyo 2015! ndipo muendelee kushangaa!.
 
taarifa za uhahika sumari jina lake kesho kukatwa. Mpaka sasa sumari si raia wa tanzania hivyo anakosa sifa za kugombea ubunge. alipofika miaka 18 alitakiwa aukane uraia mmoja (wa kenya). hata kama wazazi wake wote ni watanzania lakini hakuzaliwa katika ardhi ya tanzania si raia.

kama walijua si raia wa Tanzania then walishindwa nini kumtoa kwenye hatua za mwanzo? Tena na juzi wangefanya kumtoa na asirudie tena uchaguzi. Wasukuma wanasema senema iyeniyi.
 
Wana CDM wawaache CCM na mambo yao, CCM nao Wawaache CDM na mambo yao. Wakutane siku ya uchaguzi na tume ndiyo itatoa matokeo. Kukatwa Sioi hilo haliwezekani, nadhani CCM hawata rudia kumkata mtu aliyeshinda kura za maoni. Wanatambua kuwa hilo ni kosa kubwa kwao.
 
Wana JF
Hofu kubwa imetanda miongoni mwa makundi ndani ya chama tawala kuwa huenda kesho kamati kuu ikamkata mgombea aliyeshinda Arumeru Sioi Sumary na kumpitisha William Sarakikya. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Sumary hakubaliki na wajumbe wengi wa CC kutokana na kuwa kambi ya EL.

Pia Sumary anaweza kung'olewa kwa madai ya kundi lake kuhusishwa na rushwa katika ushindi alioupata kwani watu waliokamatwa na Takukuru Arusha na kuhojiwa ni kutoka katika kundi lake.

Hata hivyo uamuzi wa CC-CCM unaweza kuwa mgumu zaidi kwa kuleta madhara makubwa katika kampeni za chama hicho kwani wameru wamekuja na kaulimbiu kuwa YATIMA HADHULUMIWI wakimaanisha kuwa hawako tayari kuona Sumary anakatwa!

.

Acha walikate jina la asieoa na CHADEMA wachukue jimbo na hatimae nchi kwa ujumla. chama kikishakuwa na mpasuku ndani what do you expect? Napata raha sana kuona sisiem wakijizika wenyewe
 
Mnamuona Sioi tuu, mbona Adam Malima ni jimbo la baba yake, Dr. Mwinyi, Vita Kawawa etc, hata Fred akijenga political interest atarithishwa Monduli wakati Mzee akielekea Magogoni!.

Na sio Tanzania tuu, Mnajua Odinga alitokea wapi?, Uhuru Kenyata nae?. Mnaujua mpango wa Museveni?. Kama mlidhani ni Karume baba na Karume mtoto tuu, au ni Mwinyi baba na Mwinyi mtoto tuu!. Subirini mshuhudie atakayechukua fomu ya ubunge wa Bagamoyo 2015! ndipo muendelee kushangaa!.
UPOTOSHAJI JAZZ BAND.......

Hivi Adam malima amerithi jimbo hilo toka kwa babake??mzee malima unamjua kweli wewe?hebu tuambie alikua mbunge pale kwa mara ya mwisho lini labda?na baada ya kutoka yeye ni nani alimrithi?oterwise uache porojo zako!

Dr.mwinyi amerithi jimbo lipi au toka kwa babake?hebu tukumbushe na hapa pia;otherwise piga kimya.

Mzee kawawa alimrithisha jimbo Vita kweli mzee??una matatizo makubwa sana na unahitaji msaada wa haraka.

Mambo yako mengi ni ya kufikirika zaidi.Tunaposema ya sioi ni kama kurithishana ufalme ni kwa kuwa ni aghalabu kwa mtoto wa mfalme kuwa mfalme mara tu baada ya baba yake,hivyo mifano yako ni ya kitoto ili tu kuchanganya mambo, haina mashiko kwa tunachokijengea hoja,jipange uje kivingine ukiwa na ufafanuzi zaidi.
 
taarifa za uhahika sumari jina lake kesho kukatwa. Mpaka sasa sumari si raia wa tanzania hivyo anakosa sifa za kugombea ubunge. alipofika miaka 18 alitakiwa aukane uraia mmoja (wa kenya). hata kama wazazi wake wote ni watanzania lakini hakuzaliwa katika ardhi ya tanzania si raia.
Pamoja na hili la Uraia wake wa nchi mbili lipo pia la Rushwa iliyokithiri, Uwepo wake kwenye kundi la baba Fred linalopigwa vita ya urais wa 2015,na baya zaidi kushinda yote hayo ni jina lake. Kama ilivo hoja ya Uraia kwamba alitakiwa kuukana mmoja ule wa kuzaliwa nchini Kenya pia alitakiwa Kulikana jina lake alilokua nalo la SIOI siku alofunga ndoa ili asiendelee kuwa muongo wa kuitwa Sioi kumbe Kaoa tena binti wa Rais mtarajiwa.
 
Yaani kweli, mtoto wa nyoka ni nyoka. Hivi huyo mtoto mzee wake amefariki juzi juzi tu, badala ya kukaa atulie kwanza hapo hapo anang'ang'ania uongozi. Kama alikuwa na vision ya kuwa mwanasiasa ameshindwa nini kusubili agombee mwaka 2015 wakati hali ishatulia. Hivi hata hao makada wa ccm watamnadi vipi wakati washamkataa, mbona hata hastaili kushika uongozi. Ukiangalia upatikanaji wake umegubikwa na mizengwe kibao mpaka fisadi Lowasa ametia mkono. Jamani kwa karne hii, elimu watanzania waliyonayo, uelewa wa mambo ya kisiasa pamoja na changamoto zinazotukabili ni jambo la kushangaza kama wanameru watamchagua huyo mtoto wa Sumari, hivi nani atakubali uongozi wa kurithishana karne hii. Nawasihi wanameru wawe makini na mchezo mchafu unaofanywa na Lowasa, haiwezekani watu wawili watatu wakae waamue kuwa huyu ndo mbuge wa arumeru mashariki waanze kutumia pesa kuhakikisha anashinda huku ndio kubaka demokrasia.
 
Pamoja na hili la Uraia wake wa nchi mbili lipo pia la Rushwa iliyokithiri, Uwepo wake kwenye kundi la baba Fred linalopigwa vita ya urais wa 2015,na baya zaidi kushinda yote hayo ni jina lake. Kama ilivo hoja ya Uraia kwamba alitakiwa kuukana mmoja ule wa kuzaliwa nchini Kenya pia alitakiwa Kulikana jina lake alilokua nalo la SIOI siku alofunga ndoa ili asiendelee kuwa muongo wa kuitwa Sioi kumbe Kaoa tena binti wa Rais mtarajiwa.

haaa! Hiyo sioi kimeru inamaana nyingine.
 
Kwa hiyo Mkuu unataka kutuambia kwamba Marehemu Sumari alirithi ubunge toka kwa baba yake??

Bora mkuu umeliona ilo,huyu jamaha Pasco uwa ananiachaga hoi sana na post zake,na labda atupe mifano mitatu ya tawala za Meru zilizorithishana!
 
Endeleeni kuraruana nyie wagawa rushwa na ndivyo hukumu ya wana Arumeru Mashariki watakavyoadhibu kwenye huu uchaguzi,lichama gani hili limejaa mijizi na nawashangaa mnaoshabikia hili lichama nanyi pia ni sehemu ya haya Mafisadi,pambaf..
 
Yee Mura, sisi Wakurya tumesoma na tumeendelea sana, hebu angalia:

1. Tanzania Raisi wake ni Julius Kambarage Nyerere.
2. Uingereza Waziri Mkuu ni Margreth Chacha.
3. India Waziri wake Mkuu ni Indira Gathi.
4. Zimbabwe, Raisi wake ni Robert Magathi.

Mchaga akaja, Yesuu, sisi kwa muziki wa Reggae hamuoni? Hamuoni ndani kweli. Tuna Bob Malya, Peter Tesha, Rita Malya na sasa watoto wao wanapiga mziki pia, Steve Malya, Ziggy Malya, Endrew Tesha ..........
Mnamuona Sioi tuu, mbona Adam Malima ni jimbo la baba yake, Dr. Mwinyi, Vita Kawawa etc, hata Fred akijenga political interest atarithishwa Monduli wakati Mzee akielekea Magogoni!.

Na sio Tanzania tuu, Mnajua Odinga alitokea wapi?, Uhuru Kenyata nae?. Mnaujua mpango wa Museveni?. Kama mlidhani ni Karume baba na Karume mtoto tuu, au ni Mwinyi baba na Mwinyi mtoto tuu!. Subirini mshuhudie atakayechukua fomu ya ubunge wa Bagamoyo 2015! ndipo muendelee kushangaa!.
 
unajichanganya sana mkuu mpaka haueleweki unachomaanisha, mara ccm wahuni! mara tena lowassa mbarikiwa, nikuulize lowasa yeye si muhunpamoja na wenzake ccm?mkuu lowasa ni "muhuni" tu!
Mkuu bora umeniwahi sababu huyu Myisanzu hata simuelewi hata kidogo unamshabikia Lowassa wakati yeye ndie MuHUNI wa kuogopwa kabisa ndani ya CcM kwa hyo haeleweki kabisa
 
Back
Top Bottom