Zanzibar 2020 Namba 17: Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Khamis Mussa Omar achukua fomu kuwania Urais wa Zanzibar kupitia CCM

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar Amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi

photo_2020-06-22_10-09-24.jpg

KHAMIS MUSSA OMAR- TUMAINI JIPYA

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Ndugu Khamis Mussa Omar, mtoto wa mkulima na mkwezi aliyezaliwa Desemba 28 mwaka 1965 Visiwani Zanzibar.

Ni msomi mwenye elimu ya Chuo Kikuu akihitimu Shahada ya Pili katika fani ya Sayansi katika Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Glasgow nchini Uningereza mwaka 2009 ambapo mwaka 1996 alihitimu Stashahada ya uzamili ya Utawala katika Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham nchini Uingereza.

Akiwa Chuo Kikuu cha Glasgow, Khamis Mussa kutokana na uwezo wake aliwavutia walimu wake kiasi cha kumshawishi kubakia Chuoni kama Mwalimu baada ya kuhitimu masomo yake, amekuwa mwanafunzi bora na aliyepata kiwango cha juu katika alama za masomo yake akiwashinda wanafunzi kadhaa wa Mataifa mbalimbali.

Khamis Mussa Omar mwenye kipaji , mwerevu na muhubiri mkubwa wa Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na, ni Mzalendo wa kweli wa Kiafrika na ni mwanasiasa mwenye siasa za kati.

Ni Kada shupavu wa CCM, hodari na makini, mbali ya nafasi ya Ukatibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Khamis Mussa amebahatika kufanyakazi katika Serikali zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-Zanzibar (1997-2002.

Mwaka 2005 – 2006, Khamis Mussa aliteuliwa na Rais wa awamu ya sita wa Zanzibar, Dkt Amani Abeid Karume kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Ukuzaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA).

Nyota yake katika utendaji wa Serikali ilizidi kung’ara pale mwaka 2006 – hadi hivi sasa alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha akifanyakazi na Marais wawili, Rais wa awamu ya sita wa Zanzibar , Dkt Amani Abeid Karume na Rais wa awamu ya saba, Dkt Ali Mohamed Shein.

Khamis Mussa, sio tu amepata uzoefu katika Serikali, pia amewahi kufanyakazi katika sekta binafsi akiwa mwanzilishi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo akiwa Katibu Mkuu wa Kwanza wa Jumuuiya hiyo hapa Zanzibar.

Amekuwa katika Bodi mbalimbali nitazitaja chache ,kwa sasa ni Mkurugenzi (asiye mtendaji) wa Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania na nyenginezo.

Hadi anakwenda kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Juni 22 mwaka huu, hakuna anayefahamu kwa undani ni kitu gani kimekuwa kikitokea katika siasa za Zanzibar kiasi cha Khamis Mussa alipohusishwa na mbio za Urais.

Ni vigumu kwa wakati ule kuweza kubaini ni nini hasa kilichowafanya baadhi ya watu na hata wachambuzi wa kisiasa kumtaja katika mbio za Urais hasa ikizingatiwa kuwa ndani ya Baraza la Mapinduzi na kwa Makatibu Wakuu wapo mawaziri ambao aghalab baadhi yao walionekana kuwa na uzoefu wa muda mrefu katika uongozi katika ngazi za kisiasa na kiserikali tofauti na yeye.

Je ni hulka yake ya kujichanganya na watu wa rika tofauti? Ni haiba yake ya ujana aliyodumu nayo kwa miaka takriban 20 katika nafasi ya Ukatibu Mkuu Wizara ya Fedha ?

Ni upofu wa mashabiki zake? Ni upeo wake mkubwa wa kuona mambo? Ni hoja zake za kisasa? Ni uzalendo wake? Ni mapungufu waliyonayo washindani wake? Ni kitu gani hasa? Wazanzibari wanawajibika kukiangalia na kukitafutia jawabu zake.

Kinachomtofautisha Mwanauchumi huyo na baadhi ya wagombea wengine ni kwamba, ugeni wake (Khamis Mussa ) katika siasa za ndani ya CCM haitakuwa kikwazo kikubwa kwake kwani tayari alishakuwa kwa kipindi kirefu katika nyadhifa za kiserikali,lakini pia uwezo wake kiutendaji.

Licha ya majina makubwa kujitokeza kuchukua fomu ya urais wa Zanzibar bado jina moja kubwa linaonekana kuwa na mvuto wa kipekee nalo ni la Khamis Mussa Omar.

Ukiacha uzoefu wa kisiasa na utumishi Serikalini, Khamis Mussa anaonekana kuwa na sifa nyingine ambayo pengine wengine hawana, sifa ambayo kimsingi ndiyo inayomfanya awe mgombea maarufu zaidi kuliko wengine wote ndani ya kapu la CCM.

Ni jambo la wazi kuwa , wanasiasa ambao wanamuunga mkono Khamis Mussa katika mbio za kuteuliwa na CCM, wamekuwa wakimuona kama mgombea anayewakilisha mawazo ya kizazi kipya cha Wazanzibari na mtu anayeweza akawa kiungo cha wanasiasa wastaafu na damu changa ya vijana.

Khamis Mussa , kada wa CCM, mwenye dhamira ya kulivusha jahazi la Chama katika bahari iliyosheheni kila aina ya dhoruba, bila shaka kwa kutumia nguvu ya vijana yenye kuhitaji mabadiliko wanayoyaamini, ataweza kutufikisha salama katika Uchaguzi Mkuu kwa kukipatia CCM ushindi mkubwa.

Changamoto kubwa ambayo inamkabili, Khamis Mussa ni ujana wake. Wapo watakaompima kwa ujana wake wakiona ni kigezo cha kutomuunga mkono, lakini hoja hiyo ni dhaifu mno isiyokuwa na nafasi katika zama hizi za ‘vijana na Utawala’ kwani kwa sehemu kubwa tumaini la vijana ni kupata Kiongozi anayejuwa mahitaji yao kwa maana atokana na vijana wenyewe.

Khamis Mussa, Kada wa CCM, anajuwa shida, dhiki, na ni mtu aliyekulia katika mazingira ya kimasikini, kwa ujumla katika kipindi cha utumishi wake ndani ya Serikali na nje amejifunza mengi ambayo akitumia na sera za Chama chake ataweza kuwafikisha Wazanzibari katika hatua ambayo inatarajiwa na kila mmoja wetu.

Akiwa Chuo Kikuu cha Glasgow, Khamis Mussa kutokana na uwezo wake aliwavutia walimu wake kiasi cha kumshawishi kubakia Chuoni kama Mwalimu baada ya kuhitimu masomo yake, amekuwa mwanafunzi bora na aliyepata kiwango cha juu katika alama za masomo yake akiwashinda wanafunzi kadhaa wa Mataifa mbalimbali.

Hakuwa katika lile kundi la ‘Kayumba’ daima alitoa mwanafunzi bora, kwa kuwa yeye ni Mzalendo wa kweli, hakuweza kubaki katika viunga vya Chuo Kikuu cha Glasgow, akaamua kurejea nyumbani kuitumikia nchi.

Khamis Mussa, ana uwezo wa kujenga hoja katika vikao, mikutano ya ndani ya Nchi na ile ya Kimataifa. Yeye si Kasuku, anasoma kwa makini vitini vya mkutano na anajenga hoja bila papara, bila hofu, bila jazba. Anatulia wakati wa kuzungumza na anayozungumza ni yale yenye mantiki wala hasemi maneno ya kukirihisha wenzake.

Katika vikao vya majadiliano na mijadala, ameonesha uwezo mkubwa wa kupanga maneno, kushawishi upande wa pili kukubaliana na hoja zake. uzoefu alioupata serikalini akichanganya na uwezo wake na uhodari wa utendaji kazi ambao mtu yeyote makini anayemfahamu hawezi akautilia shaka hata kidogo uwezo wake katika nafasi ya Urais.

Baadhi ya watu wanaweza kusema mambo hayo ndo yanatosha kumfanya awe kiongozi mwenye kutakiwa na umma? Kwa hakika kama ningeamua kuorodhesha mambo aliyoyafanya akiwa mtumishi Serikalini utajaza vitabu.

Gwiji wa ushahiri,Mzee Haji Gora Haji katika kitabu chake cha Kimbunga kuna shairi linasema;

Najibu mimi najibu, kuimba naweza

Jina ulonita Mduruma, mie Peremu limenipendeza

Sishindwi na kushona tanga, na wala kuiunga heza

Kama unahodha kazi yangu, hakuna moja litalonizoza

Naam! Khamis Mussa hashindwi kuongoza Serikali, uwezo wa kufanyakazi hiyo anao na hakuna mwenye shaka kwa hilo. Hata hivyo, Khamis Mussa atalazimika kufanya kazi ya ziada kuyashinda majina makubwa yaliyochukua fomu kuomba ridhaa ya CCM kuteuliwa kuwa mgombea wake.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar Amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi

Hii ni fomu au ni mkoba.Kwa vyovyote vile majina ya vijana wapya kama hawa huenda ikawa ndio jibu la raisi atakayemrithi dkt Ali Mohammed Sheni
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar Amechukua fomu ya kuwania kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi

Tanganyika wameshafika wangapi?
Inafikirisha sana Hili swala

MÊmENtO HoMO
Aisee Baba angu Sisi wa TII ELO PII tunamuunga mkono Mgombea kutoka Chama Cha Mapinduzi eti! 🙄
Mnajua nini? Chukua chukua form Zanzibar ni ujanja wa ccm kuwahadaa wananchi kwamba kuna demokrasia na pia kuficha aibu ya watu kuzuiliwa kushindana na jiwe. Kuweni macho na udikteta katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom