Hofu yatawala Siyoi Sumari kukatwa na CC-CCM

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Wana JF
Hofu kubwa imetanda miongoni mwa makundi ndani ya chama tawala kuwa huenda kesho kamati kuu ikamkata mgombea aliyeshinda Arumeru Sioi Sumary na kumpitisha William Sarakikya. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Sumary hakubaliki na wajumbe wengi wa CC kutokana na kuwa kambi ya EL.

Pia Sumary anaweza kung'olewa kwa madai ya kundi lake kuhusishwa na rushwa katika ushindi alioupata kwani watu waliokamatwa na Takukuru Arusha na kuhojiwa ni kutoka katika kundi lake.

Hata hivyo uamuzi wa CC-CCM unaweza kuwa mgumu zaidi kwa kuleta madhara makubwa katika kampeni za chama hicho kwani wameru wamekuja na kaulimbiu kuwa YATIMA HADHULUMIWI wakimaanisha kuwa hawako tayari kuona Sumary anakatwa!

.
 
Yatima hadhulumiwi kwa kuwa alipatikana kwa rushwa? Na hao waliokosa hiyo nafasi kwa ajili ya chapaa chafu ya lowasa hawkudhulumiwa? Acheni ujinga, huyu mtu kapatikana kwa rushwa inabidi akae kule bungeni kama ndondocha aliyempeleka huko kwa chapaa ya ajabu
 
taarifa za uhahika sumari jina lake kesho kukatwa. Mpaka sasa sumari si raia wa tanzania hivyo anakosa sifa za kugombea ubunge. alipofika miaka 18 alitakiwa aukane uraia mmoja (wa kenya). hata kama wazazi wake wote ni watanzania lakini hakuzaliwa katika ardhi ya tanzania si raia.
 
yote sawa,wakate wasikate sisi tunajua Nassary ndiye mbunge wetu.tunajua hizo ni propaganda za kumtangaza mgombea wao ccm.
 
Mleta mada acha majungu yasiyo kichwa wala miguu.

Mkubwa!

Ni kwamba mleta heading hajasomeka ama una lako?
Nakwambia hili jimbo safari hii itawasambaratisha chichiem na habari ndiyo hiyo!

Ingependa sana wangetengana hawa majambazi wakubwa!
 
taarifa za uhahika sumari jina lake kesho kukatwa. Mpaka sasa sumari si raia wa tanzania hivyo anakosa sifa za kugombea ubunge. alipofika miaka 18 alitakiwa aukane uraia mmoja (wa kenya). hata kama wazazi wake wote ni watanzania lakini hakuzaliwa katika ardhi ya tanzania si raia.

Haitakuwa ajabu hiyo ikitokea. Ila ili hili la uraia litokee ndani ya CC itabidi mjumbe mmoja apendekeze lirudishwe katika mjadala. Tayari Chiligati aliliingiza na likakataliwa kuwa halina uzito. Je, nani atasimama tena na kupingana na CC ya wiki jana? Mjumbe gani wa CC anataka kununua hii kesi na kwa faida ya nani?

Msekwa na Chiligati walikuwa ni wa wasimamizi wa uchaguzi wa marudio na wazungumzaji, na kama hawakulisema kwenye Mkutano Mkuu wa Wilaya Arumeru, ili wakimbilie kulisema tena kwenye CC basi watakuwa na chuki binafsi na Siyoi na wala siyo suala la uraia tena.

Na pia sidhani kama Sarakikya atapenda kubebwa hivyo kama kiwete. Sarakikya ana msimamo wake, na ni wazi ataaibika sana kama atakubali kubebwa kiasi hicho. Labda wampitishe mtu mwingine na siyo Sarakikya ambaye mara mbili ameshindwa kupata hata kura 400, pamoja na kupigiwa chapuo na vigogo wa Chama Taifa.

Maoni yangu ni kuwa Siyoi atapitishwa, ila CCM watajifanya kama hamnazo vile na watamuacha mwenyewe ahangaike na kampeni zake kama walivyofanya kwa Raza - Uzini.
 
taarifa za uhahika sumari jina lake kesho kukatwa. Mpaka sasa sumari si raia wa tanzania hivyo anakosa sifa za kugombea ubunge. alipofika miaka 18 alitakiwa aukane uraia mmoja (wa kenya). hata kama wazazi wake wote ni watanzania lakini hakuzaliwa katika ardhi ya tanzania si raia.
Kamati kuu ilishasema hakuna tatizo na uraia wake wenyewe watafutetafute kwenye mafaili yao wanaweza kupata sababu nyingine.
 
Wana JF
Hofu kubwa imetanda miongoni mwa makundi ndani ya chama tawala kuwa huenda kesho kamati kuu ikamkata mgombea aliyeshinda Arumeru Sioi Sumary na kumpitisha William Sarakikya. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Sumary hakubaliki na wajumbe wengi wa CC kutokana na kuwa kambi ya EL.

Pia Sumary anaweza kung'olewa kwa madai ya kundi lake kuhusishwa na rushwa katika ushindi alioupata kwani watu waliokamatwa na Takukuru Arusha na kuhojiwa ni kutoka katika kundi lake.

Hata hivyo uamuzi wa CC-CCM unaweza kuwa mgumu zaidi kwa kuleta madhara makubwa katika kampeni za chama hicho kwani wameru wamekuja na kaulimbiu kuwa YATIMA HADHULUMIWI wakimaanisha kuwa hawako tayari kuona Sumary anakatwa!

Kwa kujionea zaidi mgawanyiko na hofu hii, nenda katika TANURU LA FIKRA ukajionee

Nawasilisha.

Kichwa cha habari na habari yenyewe tofauti nahisi unaugonjwa wa FISADIOROENLmg 2015 pole sana.
 
hawawezi kukata jina lake..mjiandae kupigwa chini mara hii tena..najua tayari mmeshaandaa excuses
 
yote sawa,wakate wasikate sisi tunajua Nassary ndiye mbunge wetu.tunajua hizo ni propaganda za kumtangaza mgombea wao ccm.
Mgombea wao yupi maana hadi sasa hawajapata mgombea, labda cha kuwakumbusha tu waangalie muda wa mwisho kurudisha fomu unaweza kupita wakingali wanahangaika kutafuta mgombea.
 
Back
Top Bottom