Hodi waungwana wa jamii forum

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Kwa muda mrefu nilifikiri nina kila kitu muhimu kwa maisha yangu mpaka nilipochungulia kurasa za Jamii Forum. Kumbe nilikuwa naishi na njaa kali ya maarifa ilhali JF imejaa mapochopocho niliyoyaonja leo tarehe 20/12/2011.Nipeni pole sana kwa kuchelewa kiasi hiki kwani nimeona waungwana wengi walijiunga zama za zama, baadhi mwaka 2006 na wengi mwaka 2010. Jama ndo nimeingia hivyo na nimefurahishwa na yote niliyoyakuta huku.Mambo mengi ntakayochangia yatakuwa kwenye lugha, siasa kwa mbali sana, muziki,na mambo ya jamii.Bila shaka hodi yangu imekidhi masharti ya mtandao huu maana naogopa kupigiwa filimbi siku ya mwanzo.Asante na ninawapenda sana!
 
Back
Top Bottom