Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
- Thread starter
- #161
Habari,ni Mara ya kwanza kukuona nimefurahi kwakuwa ktk watu wanaoongoza kwa kuota nahisi naongoza duniani:Nina maswali Mengi ambayo sijawahi kupata ufumbuzi:kwa Leo naomba nisaodie kutafsiri hii ndoto:kuna siku niliota nipo shule ya msingi ambayo nilisoma miaka mingi sana,nipo kwenye uwanja Fulani hv sasa ghafla nikamuona Simba dume nikaogopa sana,nikajitengenezea fensi zile za seng'enge haraka nikawa ndani ya fensi Simba nje,ghafla àkaja Mdogo wangu wa kiume ameshikilia bahasha ya kaki mkononi akaruka fensi akaingia ndani,nikashangaa amepitaje huko nje wkt kuna Simba?
Wkt nashangaa Mara nikamuona yule Simba nae kaingia ndani ya fensi bila kujua kapitia wapi,basi akaanza kutukimbiza tulikimbia sana huku namwambia Mdogo wangu akazane ni heri Simba anile Mimi lkn asimle yeye.nikashtuka ghafla.kuangalia saa ilikuwa SAA 8 usiku.je maana Yake nini hyo ndoto?
Hizi ndoto zenu wote zinaashiria kitu kimoja! Mapambano ya kiroho katika ulimwengu wa gizaMkuu Mshana Jr Heshima yako chief.
Nimeota usiku wa kuamkia majuzi (wiki hii hii),..Ni Mara ya tatu kama sio ya pili.
Nilianza kwenda na jamaa mahali (sura simfahamu) tukaelekea poroni kama vile kuna kitu tunaenda kukufuata tulikua na piki piki.Gafla likatokea basi Moja ivi likasimamishwa na wanajeshi wakasema Luna jambazi humo mpo chini ya linzi Mimi nilikua Katibu na basi hilo nikajitupia kwenye mitaro hii ya pembeni ya Barbara",.. Mmoja wa wale wanajeshi wakiwa wanatangisha basi akaniona akaanza kunilenga kwa risasi,.. nikainua mkono kuashiria sins kosa ila alizidi kunimiminia risasi hizo (nilikua sijeruhiki) hakuna aliyenitetea hata kwa kusikitika huku nafsi ikijawa na hofu na maumivu,..
Nikaona nisimame akanilenga za kichwa (bado nilikua sijeruhiki) Punde baada ya risasi hizo likatokea gari Moja likanibeba kunipeleka mbali (walionibeba hata siwafahamu) tukaenda mbali gafla wakatokea wengine wakimsaka mtu wao ila wakiniona mm wananitaka, kutokana na wale watu wakawa wananiacha,.. ivo ivo kwenye barrier zingine adi nikavuka nikaenda sehemu salama nikashuka nikiwa na furaha kwa kiasi chake.
Sijui itakua INA maana yoyote maana nimeota Mara ya tatu hivo hivo bila kubadilika kitu.
Hiyo ya shule ya msingi ni dalili kwamba mapambano hayo ni ya siku nyingi
Na hii ya ugenini ni kwamba tayari kuna kitu kibaya kilikuwa kinakuandama ndio maana hata mfanyakazi mwenzako akaota umekufa
Ndoto mara nyingi huwezi kupata tafsiri yake halisi bali ni kwa ujumla wake tu kutokana na viashiria vya ndoto husika
Hizi ndoto za kujirudia rudia ndio hizi tunazoita ndoto maono au taarifa, ni ufahamu wako unajaribu kukupa warning fulani...unaota unagongwa na gari lakini huumii ukifika kesho yake kazini unanusurika kuanguka kwenye ngazi nk
Ndoto za mapambano halafu huku unaibuka mshindi, ni mapambano na vita vya nguvu za giza lakini Zikiwa zinakushindwa hasa kama zikiendelea kujirudia kwamba mapambano hayo bado yanaendelea
Ni vema na ni muhimu ukiota ndoto za kujirudia rudia siku inayofuata ujaribu kuwa makini kwa kinachokutokea kisha linganisha na ndoto husika utagundua mengi ya kushangaza sana