Hivi yule mchungaji Isack Ndodi yupo wapi?

Mandown

JF-Expert Member
Apr 8, 2012
1,665
503
ati nauliza wadau yule mchungaji wa tiba kwa kutumia chakula mch Isack Ndodi kafunga biashara ama kabadilisha staili ya kuhudumu.... manake si muoni kwa runing yangu siku hizi!!!:rolleyez:
 
Aisee hata mimi simuoni nilkua namsoma EATV jumapili(1330) na StarTv Jummane(2200) sijui kaishia labda kafua.
 
what did you expect? mlimsema sanaaa, mkawafumbua macho wateja wake wakamkimbia..
what next? kaingia chimbo..
 
kuna jamaa yupo kimara stopo over ana zahanati yake inaitwa Eden huyu ndo kamfunika Ndodi inaaminika ndie aliyekuwa akimuuzia Ndodi dawa wateja wote wa Ndodi wamekimbilia kwa huyu jamaa
 
Ndodi yupo anakariri kitabu chake muhimu 'MAHALi PASIPO NA DAKTARI' huwa nacheka sana jamaa anaporejea kitabu hicho cha zamani!
 
watu wamemshtukia alikuwa anatumia elimu yake ya sayansi kimu kutibu huku akijifanya mchungaji!!! Huyu ni miongoni mwa wanaochafua sifa za wachungaji.
 
hahahaaa.... ujue kila jambo lina mwanzo na mwisho wake........... amevuna kile kiasi alichotaka sasa kaamua atulie. Beside that, dawa zake zilikuwa ghali sana. ila kuna tetesi kahamishia biashara Nairobi. kuna wadau wanamwona sana kule
 
kwani babu mwenzangu wa loliondo kapotelea wapi!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
kwani babu mwenzangu wa loliondo kapotelea wapi!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

....yule yupa, kasema kaoteshwa dawanyingine ila mungu bado hajamuambia akauze wapi kunusuru watanzania, kwahiyo turubirie mungu aongee naye kisha atatujuza!
 
ati nauliza wadau yule mchungaji wa tiba kwa kutumia chakula mch Isack Ndodi kafunga biashara ama kabadilisha staili ya kuhudumu.... manake si muoni kwa runing yangu siku hizi!!!:rolleyez:

Hajawahi kusema kuwa yeye ni mchungaji..Yeye ni muumini tu wa kanisa la kisabato
 
yupo bana maeneo ya mwembechai kafulia mbaya.alikuwa ana ofisi pale itumbi hotel maeneo ya magomeni mwembechai now kafukuzwa kashindwa kulipa pango now yupo tu hana jipya
 
Anadumu Mungu tuu (If you believe in Him), wengine wote wanapita na kuondoka. . .Kama

alivyokuja babu wa loliondo, sheikh Yahya, Ndodi, wote kapu moja na watapita tuu
 
Back
Top Bottom