Hivi tunamuhitaji waziri mtendaji Tanzania?

wemma

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
230
164
Kwanza nianze kwa kumwelezea waziri ni nani? Kwa kadri ninavyofahamu mimi waziri ni Mwanasiasa. Waziri ni Kada wa chama chake. Waziri ni shabiki wa chama chake. Waziri ni MNAZI wa chama chake. Waziri ni mshauri wa kisiasa wa Rais. Waziri ni msimamizi wa SERA na AHADI za chama chake katika wizara husika. Kazi kuu ya waziri katika wizara ni kufuatilia manifesto ya chama chake, iliyowapa ushindi katika uchaguzi. Naomba hata hivyo nikiri kuwa mimi si 'mwanasiasa' [ingawa nashawishika kuamini kuwa kila mtu ni mwanasiasa] lakini pia si mtaalamu wa mambo ya Utawala bali mimi ni Social Worker kitaaluma.

Najua katika kila wizara kuna Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu pengine Manaibu Makatibu Wakuu wawili ama zaidi, lakini kuna Wakurugenzi kwa kila idara, Manaibu Wakurugenzi, Maafisa waandamizi na Maafisa wengine mbalimbali ambao ndio wataalamu na watendaji mahususi. Sasa Waziri anafanya nini tangu asubuhi saa 1.30 [kwa wengine watakao sifa] hadi saa 3 usiku. Napenda tuangalie kwa makini hapa; hivi tunamuhitaji kweli kweli waziri mtendaji? Kama pana waziri mtendaji wizarani, hawa Makatibu, Makamisna, Wakurugenzi na Maafisa mbalimbali wanafanya nini ambacho waziri anaweza kufanya lakini wao wanashindwa kufanya? Imetokea mara nyingi utaona Waziri akitaka kumfukuza mtumishi kazi, anamwambia [siyo kuamuru] Katibu Mkuu amfukuze mtumishi husika, kwa nini?

Kazi azifanyazo waziri si hizo hizo anazotakiwa kufanya Katibu Mkuu? Kwa kitendo cha waziri kufanya kazi za Katibu Mkuu na za Maafisa wengine si kumfanya Katibu Mkuu awe 'redundant?' Kwa utaratibu huu si tunamlipa Katibu Mkuu ambaye hafanyi kazi yote anayotakiwa kufanya? Kwa tabia hii ya Mawaziri kufanya kila kitu si anauza tu sura kwa watu 'kampeni' ili chama chake kionekane kinafanya kazi? Kwa nini kunakuwa na watu wawili wanaotakiwa kufanya kazi ile ile na bado wanalipwa mishahara na marupurupu kibao? Hayo si matumizi mabaya ya rasilimali za nchi?

Kwa mapendekezo yangu, waziri abakie kuwa mwanasiasa, mshauri wa Rais, kada wa chama, shabiki, n.k. ila aruhusiwe kwenda wizarani kufuatilia manifesto ya chama chake kama inatekelezwa kama walivyowaahidi wapiga kura. Sasa, kufanya kazi hiyo hahitaji magari wawili, mshahara mkuuuubwa na marupurupu kibaaaao! Namna nzuri ya waziri kufuatilia [siyo kusimamia] ahadi za chama chake ni kuwa na vikao vichahe, kwa mfano vikao vinne [quarterly] kwa mwaka vinatosha ili awape wataalamu nafasi ya kufanya kazi kwa uhuru naye apate taarifa ya quarter. Kama patakuwa na mapungufu atasawazisha. Kama Katibu mkuu hawezi kazi atamshauri Rais amfute kazi, basi. Waziri [wakati mwingine si mtaalamu] anawatisha tu watumishi wizarani [kwa uwepo wake] hivyo wizara zingine wanamwachia waziri afanye kila kitu! Makatibu wakuu wengi kwa kweli wanabembea tu kwenye vitu vyao ofisini.

Napenda nieleweke hata hivyo kuwa kuna mawaziri wanaochapa kazi vizuri tu lakini wanaweza kufanya hivyo kwa kuwa na vikao vya robo mwaka na kufuatilia kile walichokubaliana robo iliyopita. Ufuatiliaji kama huu unatosha kabisa kuona kuwa manifesto inatekelezeka kikamilifu. Maana kama kuwa wizarani masaa kumi na nne [14] ndiko kunakotoa tija, basi inabidi waziri awepo pia katika mamlaka zilizo chini ya wizara yake. Kwa mfano waziri Magufuri agawe muda kila siku awepo Wizarani, TANROADS, TAMESA, n.k. Waziri afanye kazi kama afanyavyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya. Inatosha kabisa hiyo na itapunguza matumizi, kisha waziri asiwe jikoni kabisa ili afuatilie sawasawa. Hivyo afanyavyo yeye anakuwa sehemu ya utekelezaji. Kwa mtindo huu ni makosa Mwakyembe kulaumu Bandari wanapoharibu. Ni makosa Magufuli kulaumu TANROADS, kwa sababu yeye naye ni sehemu ya utendaji!

Nafahamu waziri anaruhusiwa na katiba na sheria kufanya anayofanya, lakini hivi ni lazima Tanzania kufanya kazi kama Uingereza ama India? Napendekeza wataalamu waachwe wafanye kazi kwa uhuru lakini wafuatiliwe. Tujadiri.
 
RAIS wangu, Waziri mkuu wetu Mizengo Kayanza Peter Pinda alipoteuliwa kushika wadhifa huo kwa mara ya kwanza, Watanzania walimwita mtoto wa mkulima. Maskini na watoto wa maskini pamoja nao wenye mioyo yao iliyokuwa imepondekapondeka wakajazwa matumaini mapya. Wakauhisi uoto mpya.
Wakadhani wameiona nuru iamshayo uhai uliofifia! Wakamwona kama ni mtu aliyetumwa kuja kuwafuta machozi yao. Anapoamua naye kulia, nani wa kumfuta machozi?
Lakini loo! Wananchi walewale sasa, wanamzoea. Ni kitu gani kimeingia hapa katikati? Nani alaumiwe kwa hali hii kutokea? Kuna aliyekengeuka? Je, ni Waziri Mkuu au ni wananchi? Awe yeyote yule, hali hii haitufai. Aliyekengeuka lazima arudishwe kwenye mstari ili nchi ipate kusonga mbele.
Ndugu rais, mwangwi wa andiko lililopita ulikuwa mkubwa. Wanawema wengi walinitumia maoni yao. Hatuwezi kuyaandika yote kwa nafasi tuliyonayo, itoshe tu kuwashukuru wote waliochangia kwa njia mbalimbali. Hata hivyo, kuna baadhi tunaziweka hadharani ili wananchi wengine wazisome, Waziri Mkuu naye azisome na baba nawe uzisome.
Mwanamwema aliandika; "Mwalimu wangu ikifikia watu wanashindwa kuheshimu mamlaka iliyopo, jua tunakokwenda ni kubaya sana. Ni kitu kilicho wazi, waliomzomea Pinda ni vijana waliokuwa wameandaliwa kwa mbinu za hali ya juu. Unaposema uwanja wote walizomea ina maana hata wanaCCM waliokuwa pale uwanjani walizomea? Kuwa makini sana usipende makala zako zote kuwa zinaegemea kwenye kukosoa tu ya CCM na serikali yake."
Rais wangu, heshima ya serikali yoyote duniani haitoki kwa wananchi; hutoka kwenye serikali yenyewe. Kwa wananchi huenda kudunda tu na kisha kuirudia serikali yenyewe. Kutumia fedha ya serikali inayotokana na kodi ya wananchi wote kushabikia chama cha siasa chochote hakuwezi kuitwa ni kujiheshimu kwa serikali.
Kuna watu ambao hatujajiunga na chama chochote cha siasa, kiongozi yeyote anayetumia kodi yetu kwa kushabikia chama chake cha siasa tutamkosoa tu. Ambao hawana njia nyingine watamzomea. Na wale wenye vyama tofauti na anachoshabikia watampopoa kwa mawe! Asiyejiheshimu hastaili kudai aheshimiwe!
Alichokifanya Waziri Mkuu ndicho kilekile walichokuwa wanakifanya waliokuwa wanazomea. Waziri Mkuu na wazomeaji wote walikuwa wanashabikia vyama vyao vya siasa. Tumeandika mara nyingi kuwa kufanya ushabiki katika siasa ni kufanya jambo la kipuuzi. Hali kama ile haipendezi kwa sababu inaifanya jamii inayowatazama kuwaona wote kuwa ni wapuuzi watupu.
Kuendekeza upuuzi katika mambo yanayogusa maisha ya watu ni jambo la hatari kwa amani ya nchi. Ndiyo maana tulimkariri Ernest Hemingway aliyepata kusema kuwa miongoni mwa mambo yanayosababisha uvunjifu wa amani katika taifa ni ugumu wa maisha.
Alisema "alama ya kwanza ya utawala usio bora ni kuibuka kwa mfumuko wa bei, kitu cha pili kinachofuata ni kutokea kwa vita."
Kwa maneno haya ni kwamba kwa mfumuko wa bei tulionao ni uthibitisho kuwa utawala tulionao sio utawala bora. Yaliyotokea kwenye viwanja vya Sahara jijini Mwanza ndiyo mwanzo wa hatua ya pili, vita.
Maisha magumu hayana chama cha siasa. Mfumuko wa bei uliotokana na utawala usio bora (kulingana na kauli ya Ernest Hermingway) uliosababisha maisha kuwa magumu haukuwatenga wanaCCM waliokuwa pale katika viwanja vya Sahara, jijini Mwanza.
Shida walizonazo wananchi zitokanazo na utendaji usioridhisha wa serikali haziwabagui wananchi kufuatana na itikadi zao. Zinawakabili katika ujumla wao. Mwanamwema huyu atambue kuwa kuna wanaCCM waliopigika kuliko hata wasio na vyama au vyama vingine. Hawa wasizomee?
Rais wangu, kaulimbiu ya safu hii ni ‘nchi yangu kwanza'. Tuko wengi tusioamini katika ukombozi wa kuletewa tu kwa midomo ya wanasiasa. Ni mpaka pale tu Watanzania watakapoukubali ukweli kuwa mkombozi wao wa kweli ni wao wenyewe! Iweje mtu atake kukukomboa kwa sharti kuwa akutawale?
Wote waliopo na wajao wadaini mkataba siyo ahadi! Atakayekuja kutaka kuwakomboa akiwa na Azimio la Arusha mkononi, msikilizeni! La, atakayekuja akiwa amesimama juu ya Jukwaa la Mwalimu - Mwalimu Forum (MWAFO) mpokeeni. Wengine wote ni mashaka matupu!
Ndugu rais, hatuko hapa kumchukia mtu. Matendo yake aliyowafanyia wana wa nchi hii ndiyo yatamfanya achukiwe na sisi tutayatangaza. Wala hatuko hapa kumbeba mtu. Matendo yake aliyowafanyia wana wa nchi hii ndiyo yatakayomfanya akubalike na watu na sisi tutayatangaza. Kuwa nchi inataka mabadiliko siyo siasa ya chama chochote, hiyo ndiyo hali halisi.
Tulipoandika kuwa Waziri Mkuu asingoje mpaka aje azomewe Mbagala siyo kukosoa ni kumtahadharisha jambo linalopaswa kufanywa na kila raia mwema. Tulidhani kuwa kwa mwenye nia njema angeuchukulia kama ushauri na akaagiza vyombo vyake vifanye utafiti kwa lengo la kuwaondolea watu wake kero hii. Wananchi wamefikishwa pabaya.
Huyu aliandika: "Mwalimu Mkuu wa Watu, Bwana akubariki sana. Nimeguswa mno na unyama uliouandika kuhusu hii kamatakamata ya magari hapa Mbagala. Hata mimi majuzi ilinikumba ila namshukuru Mungu sikutembea na bastola yangu. Laiti kama ningekuwa nayo mimi ningejitoa mhanga kwa ajili ya wote walionyanyaswa kwa kufungiwa magari yao na hao wezi wakubwa wanaojiita askari wa manispaa.
Lakini napenda kukuambia kuwa ipo siku mama (…) atapata upinzani wa msafara wake toka kwa wananchi wenye uchungu na mateso wanayofanyiwa na serikali yao. Endelea kutulilia! Tulio nyuma yako ni wengi sana japo hatujui tu pa kuanzia!"
Hapa ndipo wananchi walipofikishwa. Kutaka hali hii irekebishwe hatuwezi kusema ni kuikosoa serikali au kumkosoa Waziri Mkuu. Kama siku hiyo huyu ndugu angetembea na bastola yake, Waziri Mkuu anadhani ni kitu gani kingetokea?
Mwingine akaandika: "Salaam Mwalimu Mkuu. Yaliyomtokea mzee ya kufungiwa gari yaliishanipata huku Sinza. Kwa sasa nafanya mchakato wa kupata silaha ya moto. Nitalipaki gari langu palepale walifunge. Nitakachokifanya itabaki historia. Nawahurumia watakaolifunga maana atakayesalia atakimbilia ulokole. Tushachoka. Najiandaa maana mpaka watu wafe kwanza ndiyo tujue kama kuna serikali."
Mwingine akaandika: "Mwalimu wa Watu si Mbagala tu, na huku kwetu Morogoro Road ni kero hiyo hiyo. Mbezi, Mlandizi hakuna vibao. Paaza sauti ya wanyonge. Vituo vya nini kama mtu huruhusiwi kuegesha gari!"
Kutoka Mwanza akaandika: "Uliyoongea leo (26-9-2012) hata huku Ziwa Victoria doria wa Fisheries hulazimisha kupewa pesa bila ya kutoa risiti. Mapato hayo huingia mfuko upi wa serikali? Hongera kufuatilia tukio la kuzomewa kwa Waziri Mkuu."
Kisarawe wanasema bima ya afya wanatakiwa kuchangia sh elfu moja, lakini wanachangishwa shilingi elfu tatu na hawapewi risiti.
Kuyaandika haya siyo kukosoa CCM na serikali yake. Lengo ni kuwaonyesha viongozi wetu kero zinazowakabili wananchi, ambazo nyingi zinatokana na udhaifu wa watendaji wakuu serikalini.
Haiwezekani nchi ikae kama vile hakuna serikali. Ninapoona watu wanajipanga kumsaka yule mwizi aliyetokomea na fedha ya mzee mstaafu ili wamshughulikie wenyewe, najiuliza, ni nani anayewalazimisha wananchi wajichukulie sheria mkononi? Watakapomkamata Waziri Mkuu anategemea wampeleke polisi? Naye anajua kuwa hivi sasa anasakwa?
Wakati wengine wanatafakari ya Ernest Hermingway ya kuingia vitani, Mwalimu mwema kutoka Tabata anaandika: "Tunakoelekea wameanza na kuua wananchi. Lakini kwa mujibu wa kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu mwisho wao watawageuzia bunduki wao watawala nao wataungana na wananchi."
Rais wangu, tulipoifikisha nchi panahitaji tafakuri pana. Tusimame kwanza tuangalie tulikotoka, yawezekana tunadhani tunakwenda mbele kumbe tunarudi tulikotoka. Maji ya dunia hii ni yaleyale! Yakiwa katika uso wa dunia huitwa mto, ziwa au bahari. Yanapopanda kwenda mbinguni huitwa mvuke. Kule juu huitwa mawingu. Yanaposhuka duniani tena huitwa mvua. Mzunguko unaendelea siku nenda siku rudi.
Ndugu rais, kung'atuka kwa Abdulrahman Kinana kutoka kwenye siasa za CCM hakuwezi kuchukuliwa kama jambo lililopangwa. Yawezekana ikawa ni ajali nyingine ya kisiasa. Nini kimemsukuma kufanya hivyo? Nilipomuuliza mzee wangu wa CCM kulikoni hata Kinana ang'atuke! Alinijibu kifupi tu kuwa, "na huyo ndiye alikuwa amebaki peke yake!" Alikuwa amebaki peke yake? Wapi? Tusubiri tuone.
Nilipomsoma mwanamwema wa Maswali Magumu nilikuta mahali ameandika, "hata ndani ya chama chake (Mwenyekiti Kikwete) wanamwona hivyo. Wapo wanaosema atakabidhi chama kwa watu walewale anaowakataa sasa kwa kuwa hana uwezo wa kuwashinda katika mikikimikiki na vitimbi vya uchaguzi wa ndani ya CCM."
Mwanamwema Juvenalis na wazo lake jepesi akaandika: "Na CCM wenyewe wanalifahamu hilo fika. Ndiyo maana wakaja na kelele za kuvua magamba. Magamba hawakuyavua na sasa hawana ujanja zaidi ya kutangaza kwamba wako hai na hawafi."
Vyombo vya habari vilimripoti Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa akizungumza kuhusu Lowassa na kashfa ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond iliyosababisha kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008.
Dk. Slaa alisema kiongozi huyo (Edward Lowassa) alilazimika kujiuzulu kama sehemu ya kuwajibika, lakini ameshindwa hadi leo kumtaja mhusika hasa wa kampuni hiyo.
Kauli ya Dk. Slaa ikanikumbusha hotuba ya dakika saba aliyoitoa Edward katika kikao cha NEC chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Mrisho Kikwete.
Alisema: "Mwenyekiti ni kitu gani nilichokifanya kuhusu Richmond ambacho wewe hukunituma au ulikuwa hukijui? Tulipotindikiwa si ulinituma nimtafute mtu aje atusaidie? Nilipolitaja jina la Rostam Aziz si ulisema huyo huyo ndiyo aje atusaidie! Mwenyekiti Rostam Aziz si ndiye alituletea Dowans?" Sijui walitaka wamtaje kwa jina lake la utoto!
Ukiyaunganisha haya matatu huja yakawa ndiyo kiini cha kung'atuka kwa Abdulrahman Kinana. Hataki kufa katika ndege inayoanguka ikiwa imetanguliza pua yake chini. Kushindwa kurejesha mrejesho wa ziara nzito aliyoifanya katika Mkoa wa Dar es Salaam kunaweza kumfanya mtu yeyote anayetaka kulinda heshima yake kung'atuka.
Kwetu kuna watu wanaitwa ‘Mkoma Chifwile'. Kuna watu kazi yao ni kuua kilichokwisha kufa.
Nilipoandika kuwa Rais wangu Kikwete walipe Dowans mapema tuepuke gharama zaidi, wengine waliniuliza Mwalimu Mkuu vipi? Niliwaambia Dowans ije mvua, lije jua lazima italipwa, hivyo ni bora ikalipwa sasa kupunguza gharama. Nikatoa sababu mbili. Kwanza ni amri ya mahakama lazima iheshimiwe. Pili ni utashi wa walipaji. Kwakuwa wanaolipa ndio wanaolipwa lazima Dowans italipwa tu.
Imeripotiwa kuwa Dowans imeibwaga tena TANESCO mahakamani, hivyo lazima walipwe. Ni gharama kiasi gani imeongezeka mpaka sasa kwa kuwasikiliza wahuni wachache?
Watu wako kimya. Ngoja uchaguzi ndani ya CCM uwaendee vibaya, Dowans wataifanya ni mauaji mapya. Wako wapi wale wakoma chifwile waliopambana na ufisadi mpaka mwisho? Kila mtu kajifungia kwenye kiyoyozi chake. Maskini wametumbukizwa katika kilindi. Ndiyo, wajinga ndiyo waliwao!
Wanasema kuna mtu ‘fyatu', hakuna mtu fyatu mbele ya njaa. Kalipuliwa na bomu la kivita raia asiye na hatia, mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, ni fyatu gani alifyatuka? Ni mwanamke gani jasiri alifungua mdomo wake? Wanamtandao waliozidiwa akili na wenzao nao wakadhani wangewazidi akili wananchi wote muda wote; wakawaangukia wananchi kwa kujifanya wanawahurumia. Unafiki mtupu!
Rais wangu, Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu wetu hakuwa mmoja wao wanamtandao! Na kwa sababu hiyo nimesema mwanzo kuwa kuteuliwa kwake kuliwajaza Watanzania matumaini mapya! Yampasa atambue kuwa watakapoamua kurudi kama walivyokuja hawatamjumuisha katika kundi lao. Afahamu upande unaomhusu sasa. Hizi kero tunazokuandikia simama uziondoe. Usiwe mkoma chifwile. Kama siyo Waziri Mkuu nani atawafuta machozi maskini wa nchi hii?
 
zamani nilikua naonaga waziri mkuu ni cheo kikubwa na kinastahili mtu jemedari atakayeweza kuongoza serikali bungeni na pia kusimamia watendaji wa serikali kama wakati wa kina sokoine, warioba, lowassa lakini mpaka na pinda nae kapewa hicho cheo sidhani kama kina thamani tena
 
zamani nilikua naonaga waziri mkuu ni cheo kikubwa na kinastahili mtu jemedari atakayeweza kuongoza serikali bungeni na pia kusimamia watendaji wa serikali kama wakati wa kina sokoine, warioba, lowassa lakini mpaka na pinda nae kapewa hicho cheo sidhani kama kina thamani tena
wewe mtoto wa mjini una wanyanyapaa watu wa kijijini.kwahiyo huyu alitakiwa kuwa shamba boy??
 
kimsingi wajibu wa waziri ni kutunga sera (police making) katika wizara husika, wajibu mwingine ni kushiriki katika vikao vya baraza la mawaziri ili kujadili na kufanya maamuzi mbalimbali ingawa kwa tanzania baraza la mawaziri linamshauri rais(halifanyi maamuzi)kutokana na kua rais-mfalme. kimsingi waziri hahusiki katika utendaji, kama wanafanya hivyo basi ni ultra vires
 
Mawaziri wakuu pekee walioweza kuvivaa viatu vya uwaziri mkuu kikamilifu ni Sokoine na Lowassa tu. Wengine wote walichemka!
 
wewe mtoto wa mjini una wanyanyapaa watu wa kijijini.kwahiyo huyu alitakiwa kuwa shamba boy??

ye mwenyewe alijiita mtoto wa mkulima..lakini utendaji wake wa kazi sio kama wakulima wafanyavyo kazi sijui tumuite ni mtoto wa nani
 
Back
Top Bottom