Hivi Tanzania tulipoteza wanajeshi wangapi vita vya Tanzania na Uganda

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wadau JF.

Nimeangalia TBC kipindi cha matukio ya vita kati ya nchi yetu Tanzania dhidi ya Uganda!
Sehemu kubwa ya vita inaonekana jeshi la Tanzania likuwa linateka maeneo kiraisi upinzani ulikuwa hamna, hivi kuna kumbukumbu zozote zinaonyesha Tanzania ilipoteza Askari wa ngapi! Na Mateka walikuwa wangapi walipatikana na Askari wangapi walipata vilema vya maisha!
Na vita vilipiganwa muda gani, mwenye ufahamu wa masuala haya tunaomba hatufahamishe.
Nawakilisha
 
Nimeangalia hiyo documentary. Inasisimua sana. Kulingana na maelezo yake, vita ilipiganwa kuanzia Nov 78. Kampala ilitekwa 11 Apr 79. Baadaye waliendelea kusafishasafisha kwa miezi miwili hivi wakafika ktk mipaka ya Uganda na Zaire, na Uganda na Sudan maeneo ya Moyo na Arua. Then nadhani walirudi nyumbani ingawaje wengine wachache walibaki kwa makubaliano na Uganda.

Ni somo zuri la historia ya nchi yetu. Wakati ule Tz ilikuwa na umoja wa kufa mtu. Ng'ombe waliochangwa na wananchi kwa hiari kwa ajili ya kiitoweo cha wanajeshi ni zaidi ya 75,000. Wafanyakazi waliongeza muda wa kufanya kazi ili kutoa mchango wao wa vita. Kila mtu aliwajibika. Siasa ya vyama vyingi imetuharibia nchi. Kwa jinsi CCM ilivyoongoza vile vita,...Bora ingeachiwa iendelee kutawala milele.

Waliouawa/waliopotea haikuelezwa. Hata hivyo maiti waliorudishwa home walizikwa makaburi ya mashujaa kule Bukoba.
 
Kishongo,
Kilichotuharibia nchi si siasa za vyama vingi. Ni uroho wa viongozi wa CCM kutajirika upesi na kukosa moyo wa uzalendo. Siasa za vyama vingi hazijapelekea uongozi wa CCM kugawa madini yetu kwa chee, kugawa ardhi yetu kwa matapeli. Watanzania bado wana moyo wa uzalendo lakini hatuna hivi leo viongozi wa kutuhamasisha ndani ya CCM kwa sababu wako bize kujaza matumbo yao. Huo ndio ukweli.
 
Me pia nimejiuliza ni wanajesh wangapi wa tz walipoteza maisha. Halaf wengine walikuwa vijana wadogo sana walikusanywa na kupewa short time training wakaingia vitani . Kweli nch ilikuwa na uzalendo wa hali za juu.
 
Watu walikuwa wana uzalendo wa hali ya juu sana!kuna picha moja inasikitisha sana vijana wamekusanywa na kupewa mafunzo ukiangalia jinsi walivyokuwa wamevaa inasikitisha kuna wengine wamevaa viatu lakini vidole vya miguu vipo nje, suruali wamefunga na kamba za katani kama mkanda, wanaimba kwa uchungu
 
Me pia nimejiuliza ni wanajesh wangapi wa tz walipoteza maisha. Halaf wengine walikuwa vijana wadogo sana walikusanywa na kupewa short time training wakaingia vitani . Kweli nch ilikuwa na uzalendo wa hali za juu.

Nakumbuka katika hotuba ya mwalimu kuwakaribisha mashujaa nyumbani alisema 'Tumepoteza vijana wetu 400'. Nadhani ilikuwa ni round figure na idadi inaweza kuwa iliongezeka baada ya muda.
Hakueleza hali za wengine walioumia au kupoteza viungo.

Nakumbuka waliokuwa JKT waliunganisha juu kwa juu na wengine walikamatwa makazini. Jambo la kufurahisha kuhusu uzalendo, wapo waliodanganya hata umri nakumbuka kule mwanza na Musoma ilikuwa dili.

Mabasi yalikuwa yanakamtwa kupeleka askari mstari wa mbele, na likichukuliwa basi atakayesalimika ni utingo, dereva ni sehemu ya askari mbele kwa mbele. Walporudi walipokelewa kwa shangwe na furaha. Nakumbuka wimbo wa Zahiri Ali Zoro
'mashujaa wanarejea, tuwapokee kwa shangwe
hatuna cha kuwapaa, chakuwapa ni ahsante.......................

Nchi ilikuwa na viongozi waliounganisha watu na si chama. Ilikuwa Tanzania kama uliwahi kuishi nyakati hizo.
 
Mimi nilisikia alikufa mmoja tu, mtoto wa Nyerere, labda kama kuna mwenye taarifa zaidi atujuze
 
Katika vita propaganda ndio hutawala kuliko ukweli. Serikali ya Tanzania haiwezi kusema kuwa kuna watanzania wangapi wamekufa na idadi hiyo ikawa ya kweli. Kama kungekuwepo na Documentary ya Iddi Amini nayo ingeonesha idadi kubwa ya watanzania wakiuawa, ndio mchezo wenyewe huo.
 
Ile picha ya jana ilikuwa inasisimua sana, na kwa kweli watu walikuwa wazalendo sana! Nilitamani nirecord lakini sikuwa na empty VHS tape. Amin aliagiza aletewe bendera ya Tanzania, jamaa wakampelekea ya CCM. Nilitamani nchi ya Uganda ingeshikwa na rais Mtanzania mmoja walau hata kwa dakika tano, then tuwakabidhi wachaguane, nadhani ingekuwa historia kubwa duniani!
 
Nakumbuka katika hotuba ya mwalimu kuwakaribisha mashujaa nyumbani alisema 'Tumepoteza vijana wetu 400'. Nadhani ilikuwa ni round figure na idadi inaweza kuwa iliongezeka baada ya muda.Hakueleza hali za wengine walioumia au kupoteza viungo.Nakumbuka waliokuwa JKT waliunganisha juu kwa juu na wengine walikamatwa makazini. Jambo la kufurahisha kuhusu uzalendo, wapo waliodanganya hata umri nakumbuka kule mwanza na Musoma ilikuwa dili.Mabasi yalikuwa yanakamtwa kupeleka askari mstari wa mbele, na likichukuliwa basi atakayesalimika ni utingo, dereva ni sehemu ya askari mbele kwa mbele. Walporudi walipokelewa kwa shangwe na furaha. Nakumbuka wimbo wa Zahiri Ali Zoro 'mashujaa wanarejea, tuwapokee kwa shangwe hatuna cha kuwapaa, chakuwapa ni ahsante.......................Nchi ilikuwa na viongozi waliounganisha watu na si chama. Ilikuwa Tanzania kama uliwahi kuishi nyakati hizo.
Mkuu, kuna fidia zozote walilipwa familia za wanajeshi waliopoteza maisha vitani?
 
Wengi sana walikufa,maana kuna wale waliopelekwa bila mafunzo ya kutosha na kutupwa mstari wa mbele.Kama kawaida idadi kamili haiwezi kuwepo zaidi ya makadirio.
 
Nimeangalia hiyo documentary. Inasisimua sana. Kulingana na maelezo yake, vita ilipiganwa kuanzia Nov 78. Kampala ilitekwa 11 Apr 79. Baadaye waliendelea kusafishasafisha kwa miezi miwili hivi wakafika ktk mipaka ya Uganda na Zaire, na Uganda na Sudan maeneo ya Moyo na Arua. Then nadhani walirudi nyumbani ingawaje wengine wachache walibaki kwa makubaliano na Uganda.

Ni somo zuri la historia ya nchi yetu. Wakati ule Tz ilikuwa na umoja wa kufa mtu. Ng'ombe waliochangwa na wananchi kwa hiari kwa ajili ya kiitoweo cha wanajeshi ni zaidi ya 75,000. Wafanyakazi waliongeza muda wa kufanya kazi ili kutoa mchango wao wa vita. Kila mtu aliwajibika. Siasa ya vyama vyingi imetuharibia nchi. Kwa jinsi CCM ilivyoongoza vile vita,...Bora ingeachiwa iendelee kutawala milele.

Waliouawa/waliopotea haikuelezwa. Hata hivyo maiti waliorudishwa home walizikwa makaburi ya mashujaa kule Bukoba.

what??????????????????????????
 
Muulizeni BEN KIKO.......mtangazaji wa RTD. Alirudishwa kutoka vitani baada ya kusema " WATANZANIA WANAKUFA KAMA KUKU"!
 
Sheria inasemaje unaweza kufungua kesi ukaidai serikali fidia kutokana na kupoteza viungo vyako vya mwili wakati ukiwa vitani?
 
ule uzalendo niliouona jana kwenye ile vita sijui kama utarudi,..leo tz ikivamiwa afu uniambie niende mstari wa mbele sikubali,sanasana nitaside na maadui...
 
Muulizeni BEN KIKO.......mtangazaji wa RTD. Alirudishwa kutoka vitani baada ya kusema " WATANZANIA WANAKUFA KAMA KUKU"!
Siyo Ben Kiko! Kuna yule mwingine alikuwa anatangaza moja kwa moja toka huko enzi hiyo kwa jina amenitoka kidogo lakini nikikumbuka narudi hapa chap ila siyo Ben Kiko.
 
Nimeangalia hiyo documentary. Inasisimua sana. Kulingana na maelezo yake, vita ilipiganwa kuanzia Nov 78. Kampala ilitekwa 11 Apr 79. Baadaye waliendelea kusafishasafisha kwa miezi miwili hivi wakafika ktk mipaka ya Uganda na Zaire, na Uganda na Sudan maeneo ya Moyo na Arua. Then nadhani walirudi nyumbani ingawaje wengine wachache walibaki kwa makubaliano na Uganda.

Ni somo zuri la historia ya nchi yetu. Wakati ule Tz ilikuwa na umoja wa kufa mtu. Ng'ombe waliochangwa na wananchi kwa hiari kwa ajili ya kiitoweo cha wanajeshi ni zaidi ya 75,000. Wafanyakazi waliongeza muda wa kufanya kazi ili kutoa mchango wao wa vita. Kila mtu aliwajibika. Siasa ya vyama vyingi imetuharibia nchi. Kwa jinsi CCM ilivyoongoza vile vita,...Bora ingeachiwa iendelee kutawala milele.

Waliouawa/waliopotea haikuelezwa. Hata hivyo maiti waliorudishwa home walizikwa makaburi ya mashujaa kule Bukoba.

Sidhani kama umetumia Ubongo kufikiria hicho ulichokiandika hapo. Bila shaka Umetumia Uti wa Mgongo, kwa wale wanaoelewa biology kidogo. Napenda kujua elimu yako ni ya kiwango gani tafadhali!!?
 
Wanajeshi wa Tanzania pamoja na uzalendo walikuwa nao walivyofika Jinja walipora vitu vingi sana vya raia wa Uganda, pamoja na kuiba magari na vitu mbalimbali na kuja navyo Tanzania
 
Siyo Ben Kiko! Kuna yule mwingine alikuwa anatangaza moja kwa moja toka huko enzi hiyo kwa jina amenitoka kidogo lakini nikikumbuka narudi hapa chap ila siyo Ben Kiko.
Mkuu mimi nilikuwa na miezi kadhaa toka nimezaliwa lakini jamaa aliyetaja Ben Kiko yuko sahihi, Nilisikia ijumaa iliyopita TBC Taifa kulikuwa na hicho kipindi na jamaa kaweka saut ya Ben Kiko akielezea hiyo vita Mtukula sasa hapo siwezi kujua kama alirudishwa baadaye au aliendelea kuripoti.

Kuna thread moja humu kina mkuu Kichuguu wameelezea sana nikilogin kwenye computer nitaitafuta sahivi natumia simu, hata hivyo ukitaka kujua mengi ukimpata mtu kama Msuguri ingawa amezeeka anaweza asikumbuke mambo yote, au Tumainiel Kiwelu nadhan hata Ben Kiko mwenyewe atakuwa anajua mengi.
 
Benedict Kiloloma (Ben Kiko) home boy, ndio aliekuwa akitangaza vita vya Uganda, wakati mwingine alikuwa mtangazaji Seleiman Kumchaya pamoja na Dunstan Tido Mhando
 
Back
Top Bottom