Tuna matatizo makubwa katika kutumia elimu na ujuzi tulionao. Hii imetokana na kuwa na fikra za kuazima au tegemezi.Siyo umeme tu hata maji ni shida maeneo mengi yaliyopitiwa na mradi wa maji wa ziwa Victoria.
Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Wanaoitwa wasomi hutumika kusababisha shida zaidi kwa wananchi badala ya kuwa msaada. Kunaanzishwa mamlaka za kudhibiti mabonde, maji, nishati, ... wakati huo huo hata uzalishaji bado kutosheleza (matumizi mabaya ya akili na elimu).
Wananchi wanaoishi kando ya ziwa au mto hawana maji ya mabomba majumbani (kisa matumizi mabaya ya akili na elimu kuwazuia kutumia pump kwa mahitaji yao).
Wananchi nao wanakuwa wajinga kukubali huo upuuzi.
Hawa wasomi wanatakiwa watumike kuwasaidia wananchi kupata maji kwa matumizi bora, salama na endelevu.
Hata taasisi za za kudhibiti ubora zinatakiwa zianzishwe baada ya uzalishaji mkubwa na ubunifu wa bidhaa zisizo na ubora ili kuwainua wananchi wabunifu (kwa mambo yasiyohusu afya).
Hata hivyo, changamoto ni viongozi kutokujua hali halisi ya wananchi mitaani na vijijini.
Hali itakuwa mbaya zaidi huko tuendako kwa sababu watachaguliwa na kuteuliwa watoto wa vigogo.
Maendeleo ya kweli na endelevu yatafanywa na wananchi wa kawaida, na ndiyo sababu ya migongano, misuguano na Mapinduzi katika njia ya kuelekea kwenye maendeleo.