Hivi ni kweli wabunge wote wa CCM wanaitetea serikali?

Lastname

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
921
296
Najiuliza sana hivi ni ,kweli wabunge wa CCM wote wanaitetea serikali kwa dhati? Hawayaoni ambayo serikali inachemsha sana. Na hawasomi dalili zozote zile mbele? Bora mbunge wangu huwa anapiga kimya yeye ni wa CCM, kuliko wale wanaosema sema sana. Ila nitachunguza kama hata kupiga meza huwa anapiga kimya.
 
SIo wote wanaoitetea ila ni wote wanaoiunga mkono ,si unaona bajeti za serikali zote zinapita ,hata huko upinzani nako mwisho wa siku wanaunga mkono.
 
Asante mwiba, je ni kweli wote akili zao za kufikiri ndo zimeishia hapo? Au wanapelekwa pelekwa na kuonekana hamnazo?
 
Asante mwiba, je ni kweli wote akili zao za kufikiri ndo zimeishia hapo? Au wanapelekwa pelekwa na kuonekana hamnazo?

Akili zao za kufikiri sio zinaishia hapo ni kubwa na zina uwezo wa hali ya juu wa kupanga na kupangua mambo ,ila haziruhusiwi kutumika bungeni ,unajua kuna msemo usemao ukifika sehemu watu wanachongo na wewe ziba lako jicho ,au sivyo ?

SO pale bungeni unawasikia akina Mnyika Lisu wa Pemba na wengine hofoka sana ,ila mwisho wa siku wote huziba jicho na kuwa chongo !
 
Mwiba, ondoa neno wapinzani, kuna kitu umesahau kuhusu kanuni za bunge, WENGI... NDIYO HUSHINDA, (ccm)
 
Back
Top Bottom