me huwa nasamehe bt % kubwa huwa sisahau bali naignore tu. mf. miaka ileee ya kipindi kileee nliwah kumfumania bf wangu live bt baada ya km wiki 2 kupita nkasahau sahau tukarudiana na mapenz yakanoga kuliko mwanzo simply b-cos alikubali kosa na kuomba msamaha. kiukweli me mtu akikubali kosa na ku-apologise huwa namsamehe na kuyaacha tu kwa kweli huwa hayasahauliki
Katika kusamehe na kusahau aisee yapo makosa mengine ambayo hayasahauliki! Kwangu mimi kwa hali yangu ya ubinadamu naweza kumsamehe mtu akinikosea kosa lolote lile ila yapo engine ambayo huwa ni vigumu kuyasahau. Cha muhimu huwa namwomba Mungu wangu anisaide niyasahau kabisa yale nilokosewa au hata nikiyakumbuka yasinifanye niumie au nimchukie aliyenitendea huo ubaya.
Kusahau si kupoteza kumbukumbu....................Kama uzito wa kile ulichotendewa ni mkubwa (kwako mwenyewe) unaweza kusamehe na kusahau (kwa maana ya kutorejesha moyoni maumivu uliotendewa)
Lakini pia unaweza kusamehe na usisahau kwa maana ya kwamba kumbukumbu mbaya juu ya lile ulilotendewa inakurudia kwa nguvu na kwa sababu inasukumwa emotions unashindwa kuzuia.
Lakini unaweza usisamehe wakati huo na ukasahau baada ya kipindi fulani na usiwe na kinyongo kabisa.
Muhimu kuzingatia: Kusahau si kupoteza kumbukumbu
yap, vipo ambavyo vinasahaulika kama tu mkosaji hatarudia tena, lkn akirudia anakumbusha yale ya nyumaNakubaliana na wewe Lady N, lakini ni kweli vipo ambayo vinasahaulika au tunajifanya tu kuvisahau?