Hivi ni kweli tunasamehe na kusahau?

mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
10,513
10,404
Jamani kila mara tunashauriwa kusamehe pale tunapokosewa na wenzi wetu. Tena tunaambiwa usamehe halafu usahau kabisa, then mnafungua ukurasa mpya na maisha yanaendelea!

Swali langu ni hivi, hiki tunachoshauriwa au kuaminishwa (kusamehe na kusahau) kinatekelezeka? I mean, is it realistic or we just pretend?
 
Mengi huwa nasamehe na kusahau kabisa ,mengine huwa nasamehe lakini huwa sisahau lakini hata siku moja huwa simkumbushi aliyenitenda na mara chache sana huwa nasamehe nusu na huwa namuambia/namkumbusha aliyenikosea mpaka wakati utakapofika moyo wangu ukubalishe huo msamaha.

tumetofautiana sana moto kuna watu hawajui kusamehe kabisa hata akikuambia tegemea maumivu.
 
mimi mpenzi wangu huwa namsamehe na kusahau pale anapokuwa mkweli.....na analijua hilo.....
zaidi ya hapo huwa sinaga msamaha na subiri kupokea kitu inauma......
 
vingine hata ukisamehe havisahauliki maana viaacha kumbukumbu ya maisha
 
mimi huwa nasamehe ..lakini kusahau ni ngumu kwa kweli....utasahauje sasa? huwezi kusahau
 
Nimependa hapo kwa red Chauro. Basi mi sisahaugi kitu kibaya nilichofanyiwa na mtu ye yote, sema tu huwa najitahidi kutomkumbushia
 
uko kama mimi Smile
nami niko-interested kujua kama kuna mtu anasahau kabisa, ngoja tuone kama yupo!
 
mimi mpenzi wangu huwa namsamehe na kusahau pale anapokuwa mkweli.....na analijua hilo.....
zaidi ya hapo huwa sinaga msamaha na subiri kupokea kitu inauma......

Preta niko-interested kujua zaidi hapo kwa red, ni kweli unasahau kabisa au una-pretend kusahau?
 
vingine hata ukisamehe havisahauliki maana viaacha kumbukumbu ya maisha

Nakubaliana na wewe Lady N, lakini ni kweli vipo ambayo vinasahaulika au tunajifanya tu kuvisahau?
 
Sasa huoni kama utakuwa unajipa shida tena mie mtu ambaye hayuko kivile akinikosea huwa namdharau hapo hapo na baada ya muda nasahau kabisa

Nimependa hapo kwa red Chauro. Basi mi sisahaugi kitu kibaya nilichofanyiwa na mtu ye yote, sema tu huwa najitahidi kutomkumbushia
 
Kusamehe yawezekana mziki unakuja kwenye kusahau na ili pezi liwe na afya ukishasamehe si vizuri kukumbusha jambo ambalo limeshapita ukiwa na tabia ya kukumbusha utaonekana unagumu si kwa mwanamke/mwanaume.
 
Kusamehe is deliberate and intentional lakini kusahau inategemea na magnitude ya kosa na limekuumiza kwa kiasi gani.the majority huwa tunaweza kusamehe lakini kusahau kwa wengi inakuwa ni pretence!
 
Sasa huoni kama utakuwa unajipa shida tena mie mtu ambaye hayuko kivile akinikosea huwa namdharau hapo hapo na baada ya muda nasahau kabisa

Ni kweli kwa haraka haraka inaonekana kama najipa shida vile, lakini kiukweli huwa sina nia ya kulipiza kisasi au kukata mahusiano au sijui nisimtendee mema au kumuondoa kwenye 'ufalme wangu' no siyo hivo. Nikishamsamehe tutaendelea na urafiki/mahusiano yetu kama kawaida, Ila tu ni kwamba siwezi poteza kumbukumbu ya kile alichonitendea!
 
Kusamehe is deliberate and intentional lakini kusahau inategemea na magnitude ya kosa na limekuumiza kwa kiasi gani.the majority huwa tunaweza kusamehe lakini kusahau kwa wengi inakuwa ni pretence!

Baba V umeeleza vizuri kabisa, lakini hebu malizia kuweka sawa hapo kwa red. Je, unamaanisha in real sense wapo kweli (hata kama ni wachache) wanaoweza kusahau kabisaaaa? yaani kabisaa without pretence?
 
Kusamehe yawezekana mziki unakuja kwenye kusahau na ili pezi liwe na afya ukishasamehe si vizuri kukumbusha jambo ambalo limeshapita ukiwa na tabia ya kukumbusha utaonekana unagumu si kwa mwanamke/mwanaume.

Mkuu kapistrano nimependa ulivyoweka hiyo hapo kwa red, kifupi wewe uko kama mimi ktk hili. Ila naomba nikuulize swali kidogo, je unaamini yupo ambaye anaweza kusahau kabisa?
 
Kusahau kabisa hapana yapo mambo ya kusahau lkn mengine utasahau for short period the ipo siku utakumbuka tu.
 
me huwa nasamehe bt % kubwa huwa sisahau bali naignore tu. mf. miaka ileee ya kipindi kileee nliwah kumfumania bf wangu live bt baada ya km wiki 2 kupita nkasahau sahau tukarudiana na mapenz yakanoga kuliko mwanzo simply b-cos alikubali kosa na kuomba msamaha. kiukweli me mtu akikubali kosa na ku-apologise huwa namsamehe na kuyaacha tu kwa kweli huwa hayasahauliki
 
me huwa nasamehe bt % kubwa huwa sisahau bali naignore tu. mf. miaka ileee ya kipindi kileee nliwahi kumfumania bf wangu live bt baada ya km wiki 2 kupita nkasahau sahau tukarudiana na mapenz yakanoga kuliko mwanzo simply b-cos alikubali kosa na kuomba msamaha. kiukweli me mtu akikubali kosa na ku-apologise huwa namsamehe na kuyaacha tu kwa kweli huwa hayasahauliki

charminglady nashawishika kuamini kuwa ulichokieleza (in blue) ndo kinatokea realistically, lakini hii dhana ya kusahau nadhani haipo, sema tu tuna-ignore and sometimes tuna-pretend kusahau

Ila nimependa mfano wako. Mi huwa naamini anayeweza kusamehe kosa la cheating basi hakuna kosa jingine la kumfanya ashindwe kusamehe, na in most cases watu kama wewe mnakuwaga wavumilivu kupita maelezo
 
Jamani kila mara tunashauriwa kusamehe pale tunapokosewa na wenzi wetu. Tena tunaambiwa usamehe halafu usahau kabisa, then mnafungua ukurasa mpya na maisha yanaendelea!

Swali langu ni hivi, hiki tunachoshauriwa au kuaminishwa (kusamehe na kusahau) kinatekelezeka? I mean, is it realistic or we just pretend?

Binafsi nafikiri kuna makosa ambayo ukitendewa unaweza kusamehe na kusahau na kuna mengine unaweza kusamehe ila hautaweza kusahau (Kama mwanamke kubakwa) na mengine makubwa zaidi unaweza usisamehe wala kusahau (Kama ndugu yako kuuwawa kwa kuonewa au kusingiziwa).

Kiimani unashauiwa hivyo, kusamehe na kusahau na imani hiyo ndiyo inayotulazimisha kupretend kuwa tumesamehe na kusahau ila inapotokea kama mtu amekukosea na ukamsamehe, akirudia tena ni rahisi kukumbuka uliyokutenda mwanzo na kujikuta dhana nzima ya kusahau isiwepo tena.

Kwa kifupi naweza kusema huwa tunajitahidi kusamehe lakini zoezi la kusahau ni kama tuna-pretend tu!
 
Nadhani conclusion yako (in red) ndio realistic situation ktk maisha ya kawaida ya mwanadamu, thanks mkuu
 
Back
Top Bottom