Hivi ni kweli? Cal. Gaddafi anaongea lugha ya KISWAHILI nzuri isiyo na mawimbiii???

Gaddafi, Rest In Hell, alikuwa hajui kiswahili,
ila kuna maneno ya kiarabu yanafanana na kiswahili, hivyo akitamka utadhani anaongea kiswazi
mf. Shukran, dini, timam, maskin, mushkeli, marhaba, magharib, salaam, na kadha wa kadha
 
Mi naona tumuulize mwenyewe anajiteteaje!!!!! Maswali mengine hayana maana kujadili
 
Jamaa anataka kufahamu,kwan watu weng hupata kuelmika kupitia mitandao ya jamii kama hii.Suala la mabishano linatokea wapi?

Mkubwa! Humu jamvini cku hz wa2 wanaropoka utafikiri hawajaona class,cha kushangaza hata mtu mwenyewe anayeropoka naye hata hajui chochote kuhusu swali tajwa lakini utamshangaa anaangusha lugha mbovu na hata hakuna siku anaelimisha. ONYO: Wenye tabia hii waache mara moja.
 
Toeni hoja zenye nguvu,vile vile tusiwe wakosoaji kwa mtu aliye omba kufahamu kitu au jambo fulani,
tuelimshane,na kama haufahamu kuhusu hoja ama swala alilo ongelea mwingine,sidhani kama ni busara kuvuruga lengo la mhusika.
Kuhusiana na gadaf kuongea lugha ya kiswahili!hakuna ukweli ndani yake.
 
Gadafi alikua anaongea kiswahili mimi nimewahi kukutana nae na tulizungumza kiswahili
 
hata kama aliongea kiswazi wewe inakusaidia nini, jamaa ni marehemu kwa sasa, malipo ni duniani, mbinguni ni kuimba haleluya tu kwa wale wateule wa bwana.

Kama hujui si unyamaze kimya kuna haja gani ya kumrushia mtu makombora ambaye ameuliza ili kutaka kujua?
 
Gaddafi, Rest In Hell, alikuwa hajui kiswahili,
ila kuna maneno ya kiarabu yanafanana na kiswahili, hivyo akitamka utadhani anaongea kiswazi
mf. Shukran, dini, timam, maskin, mushkeli, marhaba, magharib, salaam, na kadha wa kadha

na mudhahara, adhama, nidhamu, tawfiki, tawafu, tasnifu, makala na kadhalika
 
Na sisi watanzania tumezidi mno kujadili vitu visivyokuwa na tija.

Hivi hivi hata bungeni 'Namtambulisha mke wangu.' Hivi tuliwatuma huko kwenda kutambulisha wake zenu?

Kiswahili ni lugha tu, ajue ama asijue haikusaidii chochote. Mbona Rais Kabila anajua na hijakusaidia kitu. Kikwete ndo usiseme, lakini wapi UCHUMI ndo unaporomoka pamoja na kiswahili chake cha PWANI.

Umenena excellently my brother...Kwa kweli Watanzania wengi tunapenda kujali mambo duni na yasiyosaidia...wakati tuna tons of serious and critical issues that need our attention....ndio maana maendeleo yetu duni...
 
inawezekana...moja kati ya maneno yake ya mwisho kabla yajafa alisema "haram" kazi kwako,
 
Gadafi alikua anaongea kiswahili mimi nimewahi kukutana nae na tulizungumza kiswahili

Mkubwa! Duh! Bila shaka wewe ni anga nyingine,mpaka ulishakutana na mkabonga kiswahili sahihi kweli. Ama ni ile kishwahili ya wale ndg zetua pale "MWEMBE TAYARI MOMBASA" ndiyo anakiweza sana. Hebu tujuze Kamanda we2!
 
... na ndipo nikakataa katu katu na ndipo nikasema nipate uhakika humu. NAWAKILISHA KWA Wana JF!
Umekataa kata kata. Sasa umeleta hapa upate uhakika gani tena? Una maana ulikuwa unakataa kata kata huku ukiwa hauna uhakika?
 
Umekataa kata kata. Sasa umeleta hapa upate uhakika gani tena? Una maana ulikuwa unakataa kata kata huku ukiwa hauna uhakika?

Mkubwa! Kwa kuwa naiamini wadau humu jamvini niliamua kuleta huku nipate ukweli kwa yeyote yule mwenye uwelewa wake zaidi maana naamini tunao. Tu pamoja Kamanda!!!!
 
Wakati hbr ya mazishi ya Marehemu Cal. Mohamad Gaddafi pamoja na Mwane na waziri wake ikifanyika jangwani kusiko julikana,Kuna mabishano yanipata baada ya wadau niliokuwa nao wakisema ya kwa Gaddafi ni msemaji mzuri wa Kiswahili, na ndipo nikakataa katu katu na ndipo nikasema nipate uhakika humu. NAWAKILISHA KWA Wana JF!
Gaddafi ameshakufa na wewe mwenyewe unakiri kwamba amezikwa jangwani, iweje sasa unasema "ANAONGEA KISWAHILI......". Kama alishakufa ataongeaje kiswahili? Nadhani unaoongea kiswahili utakuwa labda ni mzimu wake na si yeye!!!
 
Kama mshikaji amepotea ktk alama ya nyakati c tuelimishane tu? Milolongo ya nini? We mzigo tu humu jamvini!! Sijui MODS yuko wapi asikupe BAN!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom