Hivi ni kwanini tusinyonge hawa wanaofirisi nchi?

HORSE POWER

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
2,099
1,415
Habari wana JF,

Pengine nimetumia lugha kali kidogo lakini ndio hivyo ilivyo. Kuna hawa wanaoitwa mafisadi ambao kimsingi si mafisadi bali ni majambazi watumiao peni na karatasi kuibia umma. Malalamiko dhidi ya ufisadi ni mengi na kashfa za ufisadi ni nyingi mno. Hili liko wazi.

Hawa watu ni hatari kwa mustakabali wa nchi na kwa lugha nyingine hawa ndio waliotufikisha hapa. Wameiibia hii nchi vibaya sana na mpaka leo bado 'inaatangatanga' nyikani. Hoja yangu ni kwamba kwanini tusiwe na sheria ya kuwanyonga hawa watu.

Hawa mafisadi ni wauaji wakubwa kuliko wauaji wa albino.Kwa ufisadi wao wengi wamekufa kwa kukosa dawa, kwa ufisadi wao miradi mingi imekwama. Tuanze sasa kunyonga hawa 'majizi' kama wafanyavyo baadhi ya nchi vinginevyo wataendelea kuchezea hii nchi. Hebu angalia hii; ekari ya milioni 25 watu wamecheza 'rafu' mpaka milioni 800 kwa ekari, hivi ni kiasi cha pesa kimeangamia? Tumeibiwa sana.

Tumechekeana sana. Tumefanywa mabwege sana. Inatosha sana! Upelekwe muswada wa kunyonga hawa mafisadi. Na hapa nawaomba wale wanaojiita watetezi wa haki za binadamu wawe na subira kidogo ili tunyooshe nchi.

Nawasilisha.
 
Mpaka sasa hakuna aliyefilisi nchi,kila ulatakae tajwa anakingiwa kifua,mfano mzuri ni yule wa Richmond na timu yake mwanzo alikingiwa na serikali na sasa anakingiwa na chama chake,hata madili mengine km escrow na ndugu zake,wahusika wanalindwa na wengine waliahidiwa ulinzi na mkuu mwenyewe. Katika mazingira hayo utamnyonga nani?

Tutaishia kuwahukumu waliokwapua hela za madawati na watumishi hewa lakini huko unakoenda unatafuta ugomvi
 
Tatizo wanaoiba hua wanakula na kila mtu, hawali peke yao. Wanahakikisha kila anaeweza kuwaletea figisu figisu na yeye anapewa kamgao, hadi viongozi wa dini wenye influence huwa wanamigao yao. Cha msingi tu, ni kuwaelimisha hao mafisadi wawekeze nchini ili hizo pesa zilete 'trickle down' effect kwa mwananchi wa kawaida badala ya kupeleka zikaozee uswiss pasipo na haki ya kuzirithi
 
Anza kumnyonga anaesotesha vijana mtaani bila kazi, tena bila sababu ya msingi.....
 
Back
Top Bottom