Wahenga wanatwambia kama unaishi kwenye nyumba ya vioo usiwatupie maadui zako mawe. Ninapata shida sana kufuatilia hoja za wabunge wa ccm bungeni, kama kuna kitu wanafanikiwa ni kuwakejeli wabunge wa upinzani. Bahati mbaya kejeli hizi ni mafanikio kwa wapinzani.
Bajeti inayojadiliwa bungeni ni ile ya serikali ambayo wapinzani wanaipinga kwa hoja ambazo zimewasilishwa kupitia waziri kivuli na michango mingine ya wabunge inayoendelea bungeni sasa. Wabunge wa ccm kuivalia njuga hoja ya waziri kivuli ni kufirisika kimawazo. Hoja ya waziri kivuli ni mchango na mawazo ya upinzani. Utashanga ccm wameacha agenda na kuunda agenda yao. Mwisho wa siku ccm wote hawatakuwa wamemtendea haki waziri wa fedha maana hakuna cha maana anachopata kutoka kwao.
Wamepoteza wasikilizaji nje ya bunge wakiona wa ccm anasimama wanasema ni wale wale wa yaleyale.
Hakuna kitu kibaya katika siasa kama kupoteza mvuto na maana yake ni kukosa fursa ya kusikilizwa. Ukisifiwa na mke wako, watoto na ndugu zako wewe si kitu, maana unatekeleza yale wanayotegemea kutoka kwako. Ni vema ukafanya vizuri na kuvutia watu wengine nje ya wale ambao wanakuhusu.
Kwa hiyo kama watu wanadhani wabunge wetu wa ccm wanakijenga chama kwa kuwakejeli wa upinzani hii ni bahati mbaya sana tena sana kwani matokeo yake ni kinyume. Ccm inabomolewa na wabunge wake bungeni. Ccm inabomolewa na makada wake serikalini na ccm inabomolewa na wanasiasa wake uchwara majukwaani. Kama ingekuwa siasa ni mchezo wa pointi kama ngumi sasa hivi refa wa mpambano wa wapinzani na ccm alipaswa kusimamisha mpambano kwani ccm inatoka damu kila sehemu ya uso na majeraha yamekuwa makubwa mno.
Bondia wa namna hii anaweza kupandwa hasira na kushika silaha ya aina yoyote akaishia kuua nataahadharisha washabiki na bondia anayepambana nae kuchukua tahadhali mapema.