Hivi modem za voda zina tatizo la kiufundi au huu ni wizi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Mimi ni mteja wa kampuni ya voda na ninatumia modem ya voda.Hata hivyo, hivyo nashindwa kuelewa hizi modem zina tatizo gani.Kwa mfano ninaweza kuweka bundle sh 700 nikatumia karibu masaa 24 kwa kuperuzu tu ila cha ajabu siku nyingine naweza weka hiyo hiyo bundle sh 700 na nikwa na peruzi tu lakini bundle hiyo inakiwishi chini ya muda wa saa moja au mawili tu.Matumizi yangu ni yale yale tu just kuperuzi lakini kifurushi kinavyokwisha nashindwa kuelewa.

Kitu kingine kinachonishangaza ni kuwa naweza kununua kifurushi kwa kuweka line kwenye simu alafu baadae nikahamishia line kwenye modem.Cha ajabu, nikitaka kukonect kwenye internet inagoma mpaka tena nitoe modem kwenye copmuter alafu nichomoe line niweke kwenye simu ala niulize salio la kifurushi kupitia simu ndio tena nirudishe line kwenye modem alafu niweke tena kwenye computer ndio nikikonect kwenye net inakubali.Sasa huu si usumbufu na ni mara kwa mara inatokea.

Naomba mnaojua mnisaidie tatizo ni nini.
 
Kwa tatizo la kwanza naweza nikakushauri.
Check kwenye computer yako kama ume'enable automatic update ya window na antivirus.
kama ipo On ni lazma kila ukiweka connection ya internet nayo ina update na tatizo la update ya window inafanyika katika background yaani huioni wakati ina'update ila bundles zinaliwa kama kawa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom