Modem za voda zimezidi wizi wa wazi

Msolopagazi

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
663
153
Jamani mie nashindwa kuelewa hawa mafisadi wa Vodacom yaani karibia miezi miwili sasa kila nikinunua bundle yaani baada ya dakika chache tu unaambiwa bundle yako imekwisha jaza hela tena.

Ukiweka ukianza kufungua Jamii forums hata hujafika kwenye topics unaambiwa your bundle is depleted. Hivi tatizo hili linawatokea hata nyinyi wana jamii au ni kwangu tu. Naomba mnijuze kibaya zaidi ukipiga simu customer care wanakwambia watatuma sms kwa kitengo cha ufundi, kibaya zaidi sijawahi kujibiwa hata siku moja.

Jamani huu si ni wizi wa mchana kweupe ndo maana nimeshindwa hata kupost kwa muda mrefu sana mpaka nafikiria kuuza modem yangu hata kuigawa ninue za mitandao mingine.
 
pole sana ndugu yangu....hili tatizo hata mimi lilinikuta tena nikaenda mpaka ofisini kwao wakaniambia hakuna shida watanirefund....mpaka leo sijawasikia miezi miwili sasa......nilichofanya....imenibidi nichakachue hiyo hiyo modem yao sasa natumia zangu airtel kwa raha zangu
 
Kwa nini ubanane kwenye ki-bittle wakati kuna Marcopollo! Mi nliwahama siku nyingi

Jamani mie nashindwa kuelewa hawa mafisadi wa vodacom yaani karibia miezi miwili sasa kila nikinunua bundle yaani baada ya dakika chache tu unaambiwa bundle yako imekwisha jaza hela tena ukiweka ukinza kufungua jamii forum hata ujafika kwenye topics unaambiwa your bunle is depleted hivi tatizo hili linawatokea hata nyinyi wana jamii au ni kwangu tu naomba mnijuze kibaya zaidi ukipiga simu customer care wanakwambia watatuma sms kwa kitengo cha ufund kibaya zaidi sijawahi kujibiwa hata siku moja jamani huu si ni wizi wa mchana kweupe ndo maana nimeshindwa hata kupost kwa muda mrefu sana mpaka nafikiria kuuza modem yangu hata kuigawa ninue za mitandao mingine
 
Du, nilifikiri peke yangu kumbe tuko wengi!. Labda mwenzetu aliyefanikiwa kuchakachua atufundishe nasi kama atapenda, maana wala hatuinjoi chochote kwa sasa. Binafsi nijaribu bundle 30 ikaliwa kama mchezo, nikajaribu kawaida ndio usiseme!.
 
hamieni zantel speed ni 3.1mbps ama airtel speed ni 236.8kbps in most cases. n they are relatively cheap. buy 500mb at 10,000 per month, 400mb at 2,500 per month respectively. cina experience na ttcl.
 
huwa nasikia sifa zao sana....bei zao unaweza kufahamu?

hapa natandaa na ttcl,30,000 kwa modem,..mi nimejiunga na huduma ya banjuka,..buku unabofya kwa masaa takribani matatu kwa usiku na speed ni ya ajabu,..atleast speed ipo juu and that what matters most to me
 
Tumia ttcl modem.unlmited download per month 45000/=,..au banjuka 1000/= per hour,..500/= kwa night
 
hamia airtel utaweza kupata ofa ya 200MB,dk 10 na message 100 kila mwanzo wa weekend (ijumaa hadi jumapili) ukiongeza salio kuanzia sh 1000 utakaloweza kulitumia saa nne usiku hadi majogoo
 
Jamani mie nashindwa kuelewa hawa mafisadi wa vodacom yaani karibia miezi miwili sasa kila nikinunua bundle yaani baada ya dakika chache tu unaambiwa bundle yako imekwisha jaza hela tena ukiweka ukinza kufungua jamii forum hata ujafika kwenye topics unaambiwa your bunle is depleted hivi tatizo hili linawatokea hata nyinyi wana jamii au ni kwangu tu naomba mnijuze kibaya zaidi ukipiga simu customer care wanakwambia watatuma sms kwa kitengo cha ufund kibaya zaidi sijawahi kujibiwa hata siku moja jamani huu si ni wizi wa mchana kweupe ndo maana nimeshindwa hata kupost kwa muda mrefu sana mpaka nafikiria kuuza modem yangu hata kuigawa ninue za mitandao mingine

Inakuaje??? I use Voda 24/7 and sina shida hio....
 
Labda mwenzetu utusaidie unafanyaje, maana yangu nimeamua kuiweka kwenye droo siiwezi!. Niliponunua walinishauri niingie kwenye bundle, nami baada ya kuingiza vocha tu nikachagua bundle ya elfu 10 ambayo ni 250mb. Ilikuwa kama saa 8 mchana sikuitumia sana nikaizima, kwenye saa 10 nikatoka kidogo nikamuacha kijana wangu. Niliporudi saa 2 usiku hamna kitu, nikafikiri labda alitumia nafasi hiyo kudown load vitu ndio maana. Baada ya siku 2 nikaweka tena elfu 10 kwa mtindo huo huo, ilikuwa saa 12 jioni nikatumia mpaka saa 2 usiku, kuja kesho yake kufungua hamna kitu. Nikajaribu kuweka bila ya kuingia kwenye bundle mambo yale yale, nikaona huu msala nimeiweka kwenye droo la kabati siiweziiiiiiiii!
 
Kweli hawa jamaa wamekuokota, pole sana!
 
hahah kaka 10,000/= VODA unapata UNLIMITED SERVICE for 7 DAYS. Soma tena products zxao ndugu yangu mimi natumia ya 25,000/= kwa mwezi unlimited na ipo njema tu kwani napata kwa siku zaidi ya 3GB.

Pia kumbuka kudisable AUTO UPDATE YA WINDOWS na ANTIVIRUS kwani hizo huwa zina kula tu kwa kwenda mbele. hasa hiyo ya AUTO UPDATE YA WINDOWS ndio kiboko!
 
Mi nafahamu kuwa kila kitu kina faida naa hasara zake thats y NATUMIA LINE YA MAZABE NAPATA FREE UNLIMITED internet...poleni sana na Kama hutakishida hamia SASATEL fungua web yao utapata ahueni.kuna unlimited day unaweka JERO unasurf hadi macho yanauma kuangalia POST ZA jamii forum.
 
Mkuu hiyo jero si kwa modem za sasatel bali ni kwa simu zao kuzitumia kama modem, speed yao ni kichefu chefu
 
Back
Top Bottom