Luali
Senior Member
- Jan 1, 2013
- 101
- 11
Nimekuwa nikifuatilia kwa kina dhidi ya issamichuzi.blogspot.com na sijawahi kuona hata mara moja ikizungumza lolote juu ya maslahi ya wananchi, wala tashuwishi mbali mbali kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu katika sekta mbali mbali za maendeleo. Hivyo ina maana hayaoni yanayotendeka au analinda ugali wake? Mawazo yangu nimefikiria ikiwa yeye ni blogger wa muda mrefu kama inavyojulikana hivyo kwa nini asichukue fursa hiyo kugombea haki za wananchi? Au anajivunia tu kwamba yeye ni blogger wa muda mrefu ila hajali wananchi wanavyoonewa,wanavyoteseka, wanavyodhulumiwa haki zao na serikali kupotosha taarifa za ukweli kwenye vyombo mbali mbali vya habari? Au anasubiria wengine ndio waandike baadae apite kwenye daraja la jasho la muhanga la waandishi wa habari majasiri? Au wadau nyinyi mnaonaje!!!