Elections 2010 Hivi mbali na askari polisi huyu ni mwana usalama gani kwenye uchaguzi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Sheria ya taifa ya uchaguzi iliyotolewa 30 Juni 2010 chini ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, F. M. Werema, ibara/ vifungu 63 (2) (l); 72 (1) (e); na 80 (6) (f) vinasema kuwa moja ya watu wanaoruhusiwa kuingia kwenye kituo cha kupigia kura ni "askari polisi au mtu mwingine yeyote anayehusika na usalama katika kituo cha kupigia kura".

Jamani naomba msaada hapa, je huyu mwingine ndio usalama wa taifa, Green Guard, JWTZ, askari magereza, Knight Support, au nani huyu? Tutamtambuaje kuwa yeye ni mwanausalama kama tunavyomtambua polisi kwa magwanda yake? Je, huu ni ushahidi tosha kwa Dr. Slaa kusema kuhusu usalama wa taifa kuvuruga uchaguzi mkuu?
 
Back
Top Bottom