NEGLIGIBLE
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 354
- 92
Jana usiku nilikuwa naangalia taarifa ya habari star tv,ambapo kulikuwa na habari ya mtoto michael lazaro ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi nyegezi b(mwanza) akimtafuta baba yake mzazi anayeishi iringa,kukimbia mateso ya mama wa kambo.kwa mujibu wa habari,mama mzazi wa michael alifariki.kwa maana michael hakuwa akiishi na baba mzazi ila alikuwa akiishi na mama wa kambo. Nijuavyo mimi ili kuwe na mama wa kambo lazima kuwe na baba mzazi,na ili kuwe na baba wa kambo lazima mama mzazi awepo.inawezekana mimi sijui vizuri maana ya mama wa kambo,vinginevyo mwandishi wa habari husika hakuwa makini wakati wa kuandaa habari.ili kuondoa wasiwasi naomba nieleweshwe maana halisi ya mama wa kambo.