Hivi mama wa kambo maana yake nini?

NEGLIGIBLE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
354
92
Jana usiku nilikuwa naangalia taarifa ya habari star tv,ambapo kulikuwa na habari ya mtoto michael lazaro ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi nyegezi b(mwanza) akimtafuta baba yake mzazi anayeishi iringa,kukimbia mateso ya mama wa kambo.kwa mujibu wa habari,mama mzazi wa michael alifariki.kwa maana michael hakuwa akiishi na baba mzazi ila alikuwa akiishi na mama wa kambo. Nijuavyo mimi ili kuwe na mama wa kambo lazima kuwe na baba mzazi,na ili kuwe na baba wa kambo lazima mama mzazi awepo.inawezekana mimi sijui vizuri maana ya mama wa kambo,vinginevyo mwandishi wa habari husika hakuwa makini wakati wa kuandaa habari.ili kuondoa wasiwasi naomba nieleweshwe maana halisi ya mama wa kambo.
 
Mama wa Kambo ni mke wa Baba, na mke wa Baba ni Mama. Hivyo basi Mama wa Kambo ni Mama.
 
mama wa kambo ni mke wa baba, na mke wa baba ni mama. Hivyo basi mama wa kambo ni mama.
mimi pia ninajua kuwa mama wa kambo ni mke wa baba,ukambo unaanza pale ambapo baba atamuacha mke wake na kuoa mke mwingine,watoto/mtoto wa baba na mama waliotengana atakuwa sasa anaishi na mama wa kambo,sio mama yake mzazi,au labda mama atafariki na baba kuoa mke mwingine ,kama mama aliyefariki aliacha mtoto/watoto, wale watoto/mtoto watakuwa wanaishi na mama wa kambo.hivyo hivyo pia kwa baba wa kambo.
 
Alaa, nilidhani hujui maana ya 'Mama wa Kambo'.
 
Mleta Mada alimaanisha kwamba ile taarifa ya Habari ilikuwa inakanganya.
Huenda haikuhaririwa . Yule mtoto anaishi na baba wa kambo, hivyo anamtafuta baba yake mzazi.
 
Back
Top Bottom