mito
JF-Expert Member
- Jun 20, 2011
- 10,513
- 10,404
Tabai ya kwenda Club na bar ndiyo iliyosababisha mchumba wake wa awali amuache.
Tabia ya kwenda bar au club si uhuni, ila jamii inachukulia ni uhuni kwani mwisho wa starehe huko bar au club ni matendo ya kihuni.
Upande wa pili hii ni tabia tegemezi, ukianzasha tu kwenda club ni vigumu kuacha tabia hii. Hata kama utakosa pesa, utatafuta tu ili weekend uende club.
Kwa sababu hiyo hapo kwa red, ndo maana utakuta wanaume wengi hawaoi wanawake wanaoenda nao club au bar. Watapeana tu kampani huko lakini mwisho wa siku mwanaume anaingia mitini, anatafuta mwanamke mwingine wa kuoa.
Binafsi huwa nawashauri wanawake/wasichana wanaotaka kuolewa waepuke kwenda maeneo hayo, unless umeishakata tamaa ya kuolewa. Otherwise, ni vizuri kwenda na mumeo kama ni obi yako.