Hivi kwanini wanawake wa kitanzania huwa hawapendi kula viporo?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,814
15,096
Kwema wakubwa?

Kuna hii ishu huwa inanishangaza sana, ni kuhusu wanawake wa kitanzania kutopenda kula msosi uliolala{kiporo}, hii ishu nimekua nikiiobserve toka kipindi nikiwa naishi nyumbani, dada zangu pamoja na mama walikuwa huwezi kuwalisha kiporo cha chakula chochote kile, mwanzo nikawa nahisi hawa labda wanaleta pozi coz wanajua vipo tu na wala hawajui mzee anavyohangaika kuvipata lakini mpaka leo wamekua watu wazima wanaojitegemea hawali kitu kinachoitwa kiporo kabisa.

Sasa nina mpenzi wangu nae naona anataka kunitia umasikini mchana kweupe coz nae ana tabia hizo, yani juzi kati kaja gheto kapika ubwabwa na tambi, sasa ule msosi uliobaki si tunatakiwa tuule asubuhi au mchana ya kesho yake coz tunakua tumeuhifadhi vizuri, mwenzangu yeye kaamka kaumwaga jalalani, kumuuliza ananijibu simple tu kuwa yeye halagi viporo hivyo akajua na mie silagi, pia wakati niko nasoma nilikuwa nasikia wadada wengi wakisema kuwa kwao ni mwiko kula viporo vya msosi wowote. Sasa nilitaka kujua hivi ni kwa nini hawa wanawake wa kitanzania hawalagi viporo?
 
Kwani huna fridge mkuu? Even without chakula kinalika bila tatizo labda mazoea ndio shida.
 
Sipo sure ila nakumbuka wakati nakua nilikua nasikia kiporo kinaleta kitambi, sasa nadhani unajua wadada na vitambi ambavyo hatupatani. Kiukweli hata mimi sikipendi kiporo na nahakikisha chakula cha usiku kinakua cha kutosha usiku tu, ili kuepuka dhambi ya kukimwaga
 
Akili zako na mawazo yako ndio yanawafikilia hivyo. Lakini wengi wanapenda na wamekulia viporo
 
Back
Top Bottom