Salaam,Shalom!!
Twende haraka kwenye mada, biashara ya Michezo ya kubahatisha Kwa sasa imetapakaa Nchi nzima Hadi vijijini, na sijawahi kushuhudia wahusika wakifunga biashara hizo Kwa kufilisika,
Betting haihitaji gharama kubwa katika uwekezaji, akishanunua mashine na kujenga ofisi hapo hapo anaanza kukamua maziwa 24/7.
Michezo ya Bahati nasibu inapata pesa Kutoka sekta zote, inaingiliana karibu na sekta zote za kiuchumi mfano;
1. BODABODA ( SEKTA YA USAFIRI).
Inakadiriwa nchini, bodaboda za miguu miwili, mitatu za kubeba Abiria na mizigo ni zaidi ya milioni 18, watu Hawa Kwa zaidi ya 75% wanabet, Kila jioni kabla ya kupeleka marejesho Kwa mabosi wao, huwasilisha kwanza rejesho kwenye betting, achukue mikeka kadhaa ndipo Afanye mengine, na mtu mmoja anaweza kuchukua Hadi mikeka 5, na ni jambo la Kila siku. Wako radhi wasipeleke rejesho Kwa tajiri ila betting lazima.
2. SEKTA YA MICHEZO.
Hapa ni UKWELI usiopingika kuwa, washabiki wa Simba na Yanga pekee, ukiwajumlisha, idadi Yao ni kubwa kuliko wanachama wa CCM na CHADEMA.
Watu Hawa Kwa zaidi ya 85% wanabet, yaani, wanabahatisha. Cha kushangaza ni kuwa, wakati wao wakibahatisha, kampuni za betting na Serikali, wao hawabahatishi, Yale ni mapato direct ya HAKIKA kabisa Kila siku. Na wabahatishaji hawajawahi kustukia mchezo huu, ni silent.
3. SIASA NA WANASIASA.
Betting Haina ubaguzi wa Vyama, CCM na CHADEMA wanaunganishwa vizuri kabisa Kwa mahusiano haya ya biashara fake ya kubahatisha vizuri kabisa, na tofauti zao za kisiasa, Huwa zinawekwa kando Ili watumie fursa zao na Uchumi wao katika kubahatisha.
Wanachama wa kawaida Kwa viongozi hubet, na wengine hawaingii Ofisini kuchukua mikeka, wanatumia simu kubeti hata wakiwa katika ofisi za Serikali, betting inaendelea vizuri kabisa.
3. SEKTA YA ELIMU.( MSINGI, SEKONDARI NA VYUO).
Vyuoni, wanafunzi VYUO vikuu, wanatumia boom kubeti, wasichana Kwa wavulana, sekondari Hadi shule za msingi hawaachwi nyuma, wanabet Hadi mitaani Kwa kutumbukiza sarafu Hadi mia na hamsini wapewazo na wazazi wao, Yuko radhi ashinde njaa lakini apate pesa ya kubeti.
4. SEKTA YA UCHUMI NA MABENKI.
Bankers wanabeti, wa mpesa wanabeti, wizara ya Fedha watumishi wanabeti,nk nk
5. SEKTA YA UTALII.
Huko kote, kampuni za kubahatisha inakusanya pesa Kila uchwao. Na hayupo anayestuka.
6. SEKTA YA BIASHARA.
Kuanzia, manufacturer, retailers, Hadi wachuuzi wanabeti, mangi na ubahiri wake, anachukua mkeka Kila siku na hastuki, usisahau Waha, pia nao wanabeti vizuri kabisa. Kampuni za betting, hazichagui, hazibagui.
7. SEKTA YA UVUVI, MADINI,KILIMO, MAWASILIANO, NK NK, NK.
Kampuni za betting zinakusanya pesa huko kote, na Kwa ufupi, hawabagui, hawachagui.
USHAURI: Ikiwa Serikali imeridhika kuwa kampuni hizi za Michezo ya kubahatisha kuwa ni sekta inayotoa ajira na kusababisha mzunguko mkubwa wa Uchumi, wanaonaje wakitoka hadharani na kuzitangaza na kuzipa TUZO sekta hizi machachari Kwa kutengeneza ajira Rasmi na zisizo rasmi?
Karibuni 🙏 Kwa maoni na ushauri kuhusiana na sekta hii Mahiri ya UCHUMI WA KUBAHATISHA.
KARIBUNI 🙏.