Hivi kwa nini tunaendekeza sana imani za kishirikina?

Tunaendekeza imani hizi kwa sababu,ushirikina hutoa majibu ya maswali magumu haraka (huku tukiwa tumejidanganya). Mfano; ili nipande cheo namloga bosi wangu basi , Biashara ngumu nakwenda Bagamoyo kwa babu; nataka kuchimba madini, namtafuta albino fulani basi nawahi mererani.
 
Nakumbuka nikiwa mtoto, mtaani kwetu kulikuwa na mzee mmoja na mkewe ambaye walisemekana kuwa ni wachawi. Basi sisi watoto (na baadhi ya wakubwa) tulikuwa tunawanazomea kila wakipita. Tulikuwa hatuwaogopi wala kuwatetemekea. Na hakukuwa na mtu yeyote aliyewahi kudhurika na 'mashambulizi' yao (kama yalikuwepo)

Sijaelewa vizuri, wewe ulikiona kitendo cha kuwazomea wazee wa watu ni kitu kizuri au kibaya?
 
Sijaelewa vizuri, wewe ulikiona kitendo cha kuwazomea wazee wa watu ni kitu kizuri au kibaya?

'maji hufuata mkondo'

...unapokuwa mtoto, matendo ya jamii inayokuzunguka yanakuathiri kwa namna moja au nyingine.

...iwapo wazazi walikuwa wacha mungu, si ajabu ukaishi maisha mfano na huo, lakini kama wazazi walikuwa "wanachungulia tobo", si ajabu imani ikakupelekea huko japo siku moja moja...
 
baada ya nchi yetu ya Tanzania kukisiri kwa mauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi ( malbino) je ? tuna kila sababu sasa kwa serikali kusimamisha leseni za wa waganga wa asili na kupiga vita waganga wa kienyeji?

kila siku mauaji ya maalbino yanaripotiwa katika vyombo vya habari lakini ndio kwanza yanazidi na uchunguzi umebaini kuwa waganga wa kienyeji na asili ndio wanaodanganya watu kuwa utajiri unapatikana kwenye viungo vya albino.

nadhani huduma zote zizotolewa na waganga hawa zisitishwe.
 
Sijaelewa vizuri, wewe ulikiona kitendo cha kuwazomea wazee wa watu ni kitu kizuri au kibaya?

Well, nilivyokuwa mtoto niliona tendo hilo la uzomeaji kuwa ni zuri. Isitoshe ukiwa mtoto, robo tatu ya matendo ufanyayo unayaona ni mazuri. Pia kuna kufuata mkumbo... Nafikiri nimejibu swali lako.
 
Sometimes mambo mengine ni kukosa akili tuu.
Wee unaenda kwa mganga eti upandishwe cheo while ndo mtu mvivu na mwenye majungu ofisini.
Ila sometimes hawa waganga aminia kama ile ya kumwona mwizi wako kwenye kioo imetulia na haina tofauti na kamera za bank-big up ila masharti yapungue.
Ntashukuru kama suala la kuruka na ungo litakuwa commercialised hasa ktk ulimwengu huu ambapo mafuta yanasumbua and time is of essense
 
Nimefikiri sana fikra za baadhi ya watanazania wakisema ili mauaji ya hawa binadamu wenzetu yaishe ni kutangaza kuwa waganga wote wa kienyeji ni dili, kisha wakasakwa na kujificha na baadae ishu ikawa ndio suluhu! I am tempted these guys might be very right! How 'bout you?
 
Sometimes mambo mengine ni kukosa akili tuu.
Wee unaenda kwa mganga eti upandishwe cheo while ndo mtu mvivu na mwenye majungu ofisini.
Ila sometimes hawa waganga aminia kama ile ya kumwona mwizi wako kwenye kioo imetulia na haina tofauti na kamera za bank-big up ila masharti yapungue.
Ntashukuru kama suala la kuruka na ungo litakuwa commercialised hasa ktk ulimwengu huu ambapo mafuta yanasumbua and time is of essense

Ushirikina haujawahi kuleta manufaa kwa jamii kwa ujumla wake....faida zake kama zipo ni short-lived na kwa mtu mmojammoja....
Tukumbuke kuwa ushirikina ni kitu kibaya na si kitu chema; ubaya ni kinyume cha uzuri.Ubaya mara zote huumiza wengi na kufurahisha wachache na kwa kipindi kifupi.
Ukiachilia mbali anecdotes za ushirikina ( k.m. kamera za kuonyesha mbaya wako n.k) ni wapi tumeona kwa mfano ushahidi wa jambo zuri lililofanywa na wachawi?
Kama kuna mwenye mifano hai hapa JF atuonyeshe.
 
Washirikina ni wagonjwa....(adui wa tatu)..wana ugonjwa kushindwa kufikiri ( over and above ujinga)

Nakubaliana nawe WomenofSubstanc, mtu mshirikina ni
-zaidi ya ujinga,
-no analysis of self problem,
-matatizo ni lazima yanatokana na mtu mwingine
-mshirikina daima hana self confidence
Mtu mshirikina daima atafanya kile anachoelekezwa and he is not a driving force but a driven one.
Huu ni ugonjwa ulio ndani ya moyo mtu mwenyewe(sick minds) na unaweza tu kuondolewa na imani sahii ya kupambana na symptoms za hapo juu.
 
...
Ukiachilia mbali anecdotes za ushirikina ( k.m. kamera za kuonyesha mbaya wako n.k) ni wapi tumeona kwa mfano ushahidi wa jambo zuri lililofanywa na wachawi?
Kama kuna mwenye mifano hai hapa JF atuonyeshe.

...WoS ...mifano, faida na hasara za uchawi zitakubalika iwapo tu nawe unakubaliana na imani ya ushirikina, ...kinyume na hapo endelea tu na msimamo wako huo kuwa uchawi ni Ujinga katika nafsi ya mtu.
 
Aluta Continua…....

Tumezungumzia jinsi gani ushiriki wa kishirikina ulivyopotofu katika jamii yetu.

Hebu sasa tuangalie njia nyingine ya uendekezaji wa imani za kishirikina katika jamii. Njia hii, si ile ya kujishirikisha na shughuli za kishirikina, bali ni ile ya kutandwa na hofu ya imani za kishirikina.

Tukiangalia hizi scenario nne – ni hipi kati ya hizi ambayo wanajamii wanahaki ya kuhofia? Na kwa nini?

1) Siku hizi watoto kula kwa jirani ni mwiko. Kisa? Eti huwezi jua jirani ameweka nini kwenye chakula.

2) Siku hizi ni mwiko kwa mtu yoyote (isipokuwa ndugu wa karibu sana) kumfunga khanga kiunoni bibi harusi. Kisa? Eti kuna hofu kuwa wengine wanakuja na kanga zilizowekwa ‘mambo’ ya kufunga kizazi.

3) Siku hizi mwanamke akiwa mjamzito, anahakikisha ananunua khanga mpya kabisa, na kuacha kuzivaa zile za zamani. Kisa? Eti kunaweza kuna na khanga zilizofanyiwa ‘mambo’ kutaka kumdhuru mtoto ingali bado tumboni.

4) Siku hizi wafiwa wanahakikisha kwenye shughuli za uoshaji wa mwili wa marehemu ni lazima kuwe na mtu ambaye kazi yake ni kuhakikisha hakuna mwoshaji yoyote anayenyofoa kiungo cha marehemu. Kisa? Eti watu huwa wanatabia ya kunyofoa viungo vya marehemu na kupeleka wa wanganga wao au hata kwenda kuviuza.
 
Tukiangalia hizi scenario nne – ni hipi kati ya hizi ambayo wanajamii wanahaki ya kuhofia? Na kwa nini?

1) Siku hizi watoto kula kwa jirani ni mwiko. Kisa? Eti huwezi jua jirani ameweka nini kwenye chakula.

2) Siku hizi ni mwiko kwa mtu yoyote (isipokuwa ndugu wa karibu sana) kumfunga khanga kiunoni bibi harusi. Kisa? Eti kuna hofu kuwa wengine wanakuja na kanga zilizowekwa ‘mambo' ya kufunga kizazi.

3) Siku hizi mwanamke akiwa mjamzito, anahakikisha ananunua khanga mpya kabisa, na kuacha kuzivaa zile za zamani. Kisa? Eti kunaweza kuna na khanga zilizofanyiwa ‘mambo' kutaka kumdhuru mtoto ingali bado tumboni.

4) Siku hizi wafiwa wanahakikisha kwenye shughuli za uoshaji wa mwili wa marehemu ni lazima kuwe na mtu ambaye kazi yake ni kuhakikisha hakuna mwoshaji yoyote anayenyofoa kiungo cha marehemu. Kisa? Eti watu huwa wanatabia ya kunyofoa viungo vya marehemu na kupeleka wa wanganga wao au hata kwenda kuviuza.

...ebwanaaa eeeh! QM mbona yote yanatisha haya, huenda kuna kaukweli hapa, hata kama mtu huna imani ya ushirikina, unakuta jimama linang'ang'ana kumfunga kanga mamsapu, tena yenye maneno "kufuli langu", hata mimi nitarusha ngumi!

Shukran kwa kunifungua macho, duh!

Woman of Substance sijui ata comment lipi juu ya hayo manne, maana yanawagusa moja kwa moja wanawake...
 
Mbu
ukiacha hilo la kwanza la kula kwa jirani ambalo siyo la siku hizi tu bali lilikuwepo tangia zamani, hayo mengine wala sina la kusema maana binafsi sijaskia.

Kula kwa jirani, kwanini mtoto ukale kwa jirani? kwenu hamna chakula?

Umesahau pia kuna zongo - jicho baya, yaani mtu anaweza kumwangalia mwanao akapata maradhi! Hili pia sijui asili yake lakini watu wengi hasa wa pwani utawasikia wakizungumzia hiki kitu.

Kuna kupigwa kipapai - sijui ndo kutupiwa majini/mashetani... alimradi utitiri wa imani za kishirikina.Lakini kama nilivyochangia mwanzo - ujinga, umaskini na maradhi ya kushindwa kufikiri na kutumia akili na pia hali ya kukumbatia imani na tamaduni zisizo na maana!
 
Mimi naomba kuuliza yafuatayo:

1. Je ushirikina/uchawi upo? (i.e. Ni kweli kwa mfano mtu anaweza akoroga ufe na ukafa?). Mwenye experience atupatie.

2. Je ushirikina na uchawi ni kitu kimoja? Mchawi ni nani na Mshirikina ni nani?
Si unaona hata viongozi wetu haweshi kuvaa mapete na macheni ya ajabu-ajabu. Ushirikina mtupu!

3. Mazingaombwe ni tofauti na uchawi/ushirikina?

Kuna thread moja kulikuwa na discussion ya jinsi viongozi mbalimali wanavyovaa mapete and cheni na kwa kiasi kikubwa watu walihusiha uvaaji wake na ushirikina. Kama ni kweli basi vita dhidi ya ushirikina/uchawi itakuwa ngumu kweli.
 
Vita ya ushirikina ni ngumu sana kuizungumza jumla jumla hivi,kwa mfano utakapoona jirani yako/mtu unayemfahamu anafanya haya utasemaje: kanunua kiwanja cha kupima kwa hela zake/ mkopo toka kazini kwake,lakini siku ya kuanza kujenga anakwenda na fundi aka mganga wa kienyeji(tapeli) eti kuzindika msingi wake au shamba lake. Viwanja vimepimwa na jirani yako ajae humjui,hofu ya nini.Uvivu na mazingira tulimokulia vinachangia sana.

Ubaya wa ushirikina ni kwamba hauna tabaka. Si tajiri,si msomi, si mbumbumbu,hata viongozi wa dini wamo. Ushauri wangu ni huu; amini ktk maarifa sahihi,utalaamu uliothibitika, jitume ktk kazi zako,weka malengo,pata ushauri wa kutosha nk na kwa njia hii unaweza kupata mafanikio yako bila kutumia ushirikina.

Tuendelee kuchangia ili tuelimike.
 
Last edited:
Kula kwa jirani, kwanini mtoto ukale kwa jirani? kwenu hamna chakula?

Eh WOS! Si unajua wakati mwingine inabidi ku-compare menu ya 'home' na ya 'jirani.' Sasa unakuta maharage ya home yapoyapo tu, yameungwa kwa vitunguu na mafuta basi. Lakini maharage ya kwa jirani yananukia nazi, iliki, na pilipili mbuzi. Sasa hebu niambie, mtoto akipiga ana-ana-do lazima mkono uangukie kwa jirani. LOL

Mbu
ukiacha hilo la kwanza la kula kwa jirani ambalo siyo la siku hizi tu bali lilikuwepo tangia zamani, hayo mengine wala sina la kusema maana binafsi sijaskia.

Next time ukialikwa kwenye harusi, nenda na khanga, halafu jaribu kwenda kumvisha bibi harusi (wakati wa kutoa zawadi). Wallahi hautaweza kumfikia bibi harusi. Utaona jinsi utakavyopigwa bonge la stop na 'shangazi-mpenda-shari.' Na ukifanikiwa kumvalisha, hiyo khanga itavulia in a blink of an eye. hautajua hata nani kaivua, kwa jinsi itavyovuliwa haraka.

Kwa nini usijaribu?...halafu uje utupe feedback

Umesahau pia kuna zongo - jicho baya, yaani mtu anaweza kumwangalia mwanao akapata maradhi! Hili pia sijui asili yake lakini watu wengi hasa wa pwani utawasikia wakizungumzia hiki kitu.

Kuna kupigwa kipapai - sijui ndo kutupiwa majini/mashetani... alimradi utitiri wa imani za kishirikina.Lakini kama nilivyochangia mwanzo - ujinga, umaskini na maradhi ya kushindwa kufikiri na kutumia akili na pia hali ya kukumbatia imani na tamaduni zisizo na maana!

Hivi jicho baya nayo ni sehemu ya imani za kishirikina? Na kuna ile ya 'mdomo mbaya' pia.
 
Mimi naomba kuuliza yafuatayo:

1. Je ushirikina/uchawi upo? (i.e. Ni kweli kwa mfano mtu anaweza akoroga ufe na ukafa?). Mwenye experience atupatie.

Uchawi upo. Uchawi ni tawi la sayansi.

Kuamini uchawi upo na kuendekeza uchawi ni vitu viwili tofauti. Binafsi ninaamini uchawi upo, lakini siuendekezi wala kuogopa. Ninaamini kuwa anayekumbwa na dharuba la kichawi ni lazima na yeye awe anajihusisha na imani hizo kwa njia moja au nyingine. Ninaamini kuwa ukikaa mbali na imani hizi, basi hautadhurika....hata kama ukashindiwe makaburini mwaka mzima.

2. Je ushirikina na uchawi ni kitu kimoja? Mchawi ni nani na Mshirikina ni nani?
Si unaona hata viongozi wetu haweshi kuvaa mapete na macheni ya ajabu-ajabu. Ushirikina mtupu!

Kwa mtazamo wangu, ushirikina ni mfupisho wa "ushiriki wa imani za kichawi." Hivyo basi, mshirikina sio lazima awe mchawi. Hata yule anayeendekeza imani hizi kwa kuhusisha kila tukio na imani za kichawi ni mshirikina. Mfano, ndugu wanaokataa bibi harusi wao asivalishwe khanga na wasio ndugu kwa kuhofia kuwa hizo khanga zinaweza kuwa zimewekwa 'mambo' ya kufunga kizazi ni washirikina. Mchawi ni mshirikina.

3. Mazingaombwe ni tofauti na uchawi/ushirikina?

Mazingaombwe ni sayansi itumiayo mbinu za kichawi. Kwa maneno mengine, mazingaombwe utumia mbinu za kichawi.
 
Mbu
ukiacha hilo la kwanza la kula kwa jirani ambalo siyo la siku hizi tu bali lilikuwepo tangia zamani, hayo mengine wala sina la kusema maana binafsi sijaskia.

Kula kwa jirani, kwanini mtoto ukale kwa jirani? kwenu hamna chakula?

Eh WOS! Si unajua wakati mwingine inabidi ku-compare menu ya 'home' na ya 'jirani.' Sasa unakuta maharage ya home yapoyapo tu, yameungwa kwa vitunguu na mafuta basi. Lakini maharage ya kwa jirani yananukia nazi, iliki, na pilipili mbuzi. Sasa hebu niambie, mtoto akipiga ana-ana-do lazima mkono uangukie kwa jirani. LOL

...ha ha ha... haki ya mungu hata mie chakula cha jirani kilikuwa kinanitoa mate kila siku ...sijui ilikuwa ni utoto? lakini hata wazungu wana msemo "the grass looks greener on the other side!"

...tukirudi kwenye sayansi ya mwafrika; ...na ile ya wale watoto wanaovimba vitumbo halafu unaambiwa "kalambishwa", au "kabemendwa" nayo imekaaje?
 
Uchawi upo. Uchawi ni tawi la sayansi.

Kuamini uchawi upo na kuendekeza uchawi ni vitu viwili tofauti. Binafsi ninaamini uchawi upo, lakini siuendekezi wala kuogopa. Ninaamini kuwa anayekumbwa na dharuba la kichawi ni lazima na yeye awe anajihusisha na imani hizo kwa njia moja au nyingine. Ninaamini kuwa ukikaa mbali na imani hizi, basi hautadhurika....hata kama ukashindiwe makaburini mwaka mzima.

Nina mashaka kidogo kama kweli uchawi ni tawi la sayansi.

Je kuna uwezekano wa kumroga mtu asiyeamini ushirikina na mtu huyo akadhurika? Kwa mfano mtoto mchanga.

Lakini kama kweli uchawi upo (mtu anaweza kukuroga ufe ukafa) then huoni pengine watu wanayo sababu ya kuchukua tahadhari. Kwa mfano kama uaamini kuna wizi/ujambazi ni lazima utafunga milango, utaweka walinzi nk. Isnt this automatic?

Je kuna ushirikina makanisani/misikitini nk? Wachungaji wanaokemea mapepo nao ni washirikina? Mtu hawezi kuzaa, wanasema mapepo! Anaumwa malaria wanasema mapepo!

Binafsi napata shida kuamini kwamba uchawi upo.
 
Nina mashaka kidogo kama kweli uchawi ni tawi la sayansi.

Well, naweza kuwa nimekosea kuhusisha uchawi kama sehemu ya sayansi. Pengine labda wachangiaji wengine wanaweza kusaidia kuelea hasa uchawi ni nini.

Je kuna uwezekano wa kumroga mtu asiyeamini ushirikina na mtu huyo akadhurika? Kwa mfano mtoto mchanga.

Kiujumla, siamini kuwa mtu asiyeendekeza uchawi anaweza kurogeka. Sasa, mtu asiyeamini uchawi hawezi kuwa anaendekeza uchawi. Kwa hiyo jibu langu ni kama la sentensi ya kwanza.

Kwa mtazamo wangu, imani ya mtoto mchanga inaangukia kwa wazazi wake moja kwa moja. Hivyo basi, kama wazazi wanaendekeza imani za kichawi, basi mtoto anaweza kudhurika.

Lakini kama kweli uchawi upo (mtu anaweza kukuroga ufe ukafa) then huoni pengine watu wanayo sababu ya kuchukua tahadhari. Kwa mfano kama uaamini kuna wizi/ujambazi ni lazima utafunga milango, utaweka walinzi nk. Isnt this automatic?

Tofauti na ujambazi, uchawi unategemea sana 'ushiriki wa imani hiyo.' Kwa hiyo, bado nasisitiza kuwa mtu ambaye hashiriki kwenye imani hizi hawezi dhurika na matendo ya kichawi. Kwa mara nyingine tena, huu ni mtazamo wangu.

Je kuna ushirikina makanisani/misikitini nk?

Ushirikina unahusisha watu. Mashehe na wachungaji ni watu. Sasa kama msikitini na makanisani kuna ushirikina, basi wahusika wa hayo 'majumba' ni washirikina.

Wachungaji wanaokemea mapepo nao ni washirikina? Mtu hawezi kuzaa, wanasema mapepo! Anaumwa malaria wanasema mapepo!

Tricky!

Sidhani kama mapepo yanatokana na uchawi. Katika miongozo ya kidini, mapepo ni aina ya viumbe ambavyo vinauwezo wa kuishi ndani ya mtu. Mapepo wako kwenye kundi la mashetani na majini (kama sio kitu hicho hicho). Uchawi ni imani ambayo inafanya mambo kwa kutumia nguvu za giza. (hapa naweza kuwa nimejichanganya mwenyewe....!!)

Sasa basi, mchungaji anayekemea mapepo si mshirikina. Lakini mchungaji anayeamini kuwa kuna watu walikufa na wakazikwa, halafu ( anaendelea kuamini) kumbe walichukuliwa kichawi na kufanywa misikule, basi huyo ni mshirikina.

Binafsi napata shida kuamini kwamba uchawi upo.

Well, ni imani kama imani nyingine. Wewe huamini kuna uchawi. Kuna watu wengine hawaamini kuna Mungu. Ni imani tu.
 
Back
Top Bottom