Hivi kwa nini tunaendekeza sana imani za kishirikina?

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
128
Hivi kwa nini tunaendekeza sana imani za kishirikina?
  • Umefukuzwa kazi kwa sababu ya uzembe - unamtafuta mchawi wako
  • Mmejaribu kwa miaka kadhaa kupata mtoto bila ya mafanikio - lazima kutakuwa na mtu kawafunga kizazi.
  • Mwanao alikuwa anafanya vizuri darasani, lakini ghafla performance imeshuka – kuna mtu amemroga.
  • Biashara yako imedorora, lakini ya jirani yako imechanganya – jirani mchawi
  • Jamaa kakolea ile mbaya kwa mpenzi/mke wake – si bure, kawekewa limbwata au kaendewa kwa mganga
  • Unataka utajiri wa haraka haraka – tafuta kiungo cha Albino
  • Na kadhalika, na kadhalika

Yaani imefikia hali ambayo hatuwezi kufanya chochote au kukubali matokeo yoyote bila kuhusisha imani za kishirikina. Maneno uchawi na ushirikina yametukaa sana midomoni mwetu. Haipiti siku bila kujikuta kwenye maongezi yahusuyo imani za kishirikina (uwe ni mshiriki wa maongezi au mpita njia tu mwenye masikio makubwa).

Nakumbuka miaka ya utoto wangu, ilikuwa ni kawaida kuvizia chakula kwa jirani. Ukijua ratiba ya nyumbani ni ugali maharage, basi unasogea kwa jirani kutaka kujua ratiba ya msosi ya kwao. Kama ya kwao ni mzuri, basi siku mzima utashinda kwao. Siku hizi watoto kula kwa jirani ni mwiko. Well, hata zamani ilikuwa ni mwiko. Lakini sababu ya zamani ilikuwa ni "tabia mbaya kula kwa watu." Siku hizi sababu ni "huwezi jua jirani ameweka nini kwenye chakula." Majirani hawaaminiki tena.

Siku hizi ni mwiko kwa mtu yoyote (isipokuwa ndugu wa karibu sana) kumfunga khanga kiunoni bibi harusi. Kisa? Eti kuna hofu kuwa wengine wanakuja na kanga zilizowekwa ‘mambo' ya kufunga kizazi. Mke wa rafiki yangu mmoja alipokuwa mjamzito, mama yake alihakikisha anamnunulia khanga mpya kabisa, na kumkataza asizivae zile khanga za zamani. Kisa? Eti kunaweza kuna na khanga zilizofanyiwa ‘mambo' kutaka kumdhuru mtoto ingali bado tumboni.

Siku hizi wafiwa wanahakikisha kwenye shughuli za uoshaji wa mwili wa marehemu ni lazima kuwe na mtu ambaye kazi yake ni kuhakikisha hakuna mwoshaji yoyote anayenyofoa kiungo cha marehemu. Kisa? Eti watu huwa wanatabia ya kunyofoa viungo vya marehemu na kupeleka wa wanganga wao au hata kwenda kuviuza.

Yaani tunaendekeza na kuogopa ushirikina kiasi kwamba hatuwezi tena kuwa huru kufanya chochote tukiwa na amani moyoni. Siku hizi hakuna matokeo mabaya yasiyohusishwa na imani za kishirikina. Inasikitisha. Nahisi hata hao ‘waitwao washirikina' wamefikia wakati hata hawapotezi ‘resources' zao tena. Wanachofanya ni "kubwaka tu…..bila ya kung'ata." I mean, kama ukitishia unapishwa njia, kwa nini utumie raslimali zako pasipo sababu?
 
Last edited by a moderator:
Ahsante Painkiller kwa msaada.

Mada iendelee....
 
qm,
Sidhani kama dhana ya uchawi na ulozi ni za siku hizi, vinginevo kusingekuwa na misemo kama kutafuta mchawi au witch-hunting.Watu waliposhindwa kuelewa au kutoa maelezo au sababu ya mambo yaliyokuwa yanatokea waliingiza imani za ushirikina au kuyahusisha na nguvu za ziada zisizoonekana.Tukumbuke pia kuwa uchawi au imani za giza zilikuwepo kama sehemu ya utamaduni si wa waafrika tu bali hata wazungu, waasia n.k.Imani za kidini kwa kiasi kikubwa zilisaidia katika kuwafanya watu wapunguze kama si kuacha kuamini au kushiri ushirikina.

Pamoja na hayo, uchawi ni kitu kipo japo haishauriwi kuishi kwa hofu ya imani hizi hasa kama unaamini Mungu.
 
Jana niliona kipindi hicho kwa sehemu. Muigizaji huyo alisema kwa kuwa,watu hutafuta viungo vya binadamu wenzao (kucha,ngozi,vichwa,viganja) kwa maelekezo ya waganga wa jadi,basi ili kukomesha hili jamii kwa mtindo ule ule wa hear say,ivumishe kuwa viungo vya waganga wa kienyeji dili sana ktk biashara. Hapo mtaona moto wake.

Jf mpo hapo,mathalani iwe ukipata macho ya mganga wa kienyeji utakuwa na uwezo wa kuona madini yalipo bila taabu,kama yeye aonavyo.

Hapo ngoma inakuwa droo mwanawane
 
qm,
Sidhani kama dhana ya uchawi na ulozi ni za siku hizi, vinginevo kusingekuwa na misemo kama kutafuta mchawi au witch-hunting.Watu waliposhindwa kuelewa au kutoa maelezo au sababu ya mambo yaliyokuwa yanatokea waliingiza imani za ushirikina au kuyahusisha na nguvu za ziada zisizoonekana.Tukumbuke pia kuwa uchawi au imani za giza zilikuwepo kama sehemu ya utamaduni si wa waafrika tu bali hata wazungu, waasia n.k.Imani za kidini kwa kiasi kikubwa zilisaidia katika kuwafanya watu wapunguze kama si kuacha kuamini au kushiri ushirikina.

Pamoja na hayo, uchawi ni kitu kipo japo haishauriwi kuishi kwa hofu ya imani hizi hasa kama unaamini Mungu.

Ni kweli hizi shughuli hazijaanza jana wala leo. Lakini tatizo ni kwamba, wakati tunapaswa kusonga mbele na kuachana nazo, ndio mwanzo tunazidi kuzikumbatia. Hiyo mifano niliyoiweka inaainisha jinsi tunavyozidi kuuendekeza huu utamaduni kadri siku zinavyokwenda.
 
...QM, ushirikina hutumika kutoa majibu ya hapo kwa papo,... mfano; mtu akikuibia huna haja ya kusubiri eti mpaka afe ndio akauone moto, ..."unamtengeneza" hapa hapa duniani :)
 
Ni katika kutapatapa pale ambapo mtu anataka kulazimisha mambo.Mfano mwanasiasa ambaye anajua kabisa hakubaliki atajitahidi kulazimisha kukubalika kwa kuongezea nguvu ya ziada.Mtu ambaye biashara zake hazichanganyi kwa sababu aidha hatumii mbinu za kisayansi kufanikisha basi ataenda kwa karumanzila ambako ataambiwa utajiri utaupata kwa kuleta viungo va albino! Mtu ambaye haamini kabisa kuwa mapenzi yamekwisha atalazimisha kwa kutafuta dawa.Kadhalika mtu mvivu na mzembe ambaye mambo yake yameharibika, hataki kukubali kwamba kayaharibu mwenyewe, shurti atafute kisababishi - karogwa!
Kwa kifupi ni ujinga ndio unaofanya watu waendekeza ushirikina!
 
...QM, ushirikina hutumika kutoa majibu ya hapo kwa papo,... mfano; mtu akikuibia huna haja ya kusubiri eti mpaka afe ndio akauone moto, ..."unamtengeneza" hapa hapa duniani :)

LOL

Sasa kwa nini huo moto asione kwa kumburuza mahakamani? Kwani mpaka ukamshindie makaburi usiku kucha ndio akione cha moto?
 
Ni katika kutapatapa pale ambapo mtu anataka kulazimisha mambo.Mfano mwanasiasa ambaye anajua kabisa hakubaliki atajitahidi kulazimisha kukubalika kwa kuongezea nguvu ya ziada.Mtu ambaye biashara zake hazichanganyi kwa sababu aidha hatumii mbinu za kisayansi kufanikisha basi ataenda kwa karumanzila ambako ataambiwa utajiri utaupata kwa kuleta viungo va albino! Mtu ambaye haamini kabisa kuwa mapenzi yamekwisha atalazimisha kwa kutafuta dawa.Kadhalika mtu mvivu na mzembe ambaye mambo yake yameharibika, hataki kukubali kwamba kayaharibu mwenyewe, shurti atafute kisababishi - karogwa!
Kwa kifupi ni ujinga ndio unaofanya watu waendekeza ushirikina!

Pamoja na ujinga, lazima kutakuwa na la zaidi. Kwani haihitaji wezevu wa hali ya juu kuona kwamba uendekezaji wa imani za kishirikina unamfanya mtu awe na fikira duni. Watanzania tunatapatapa sana. Sijui ndio maradhi ya umasikini au basi tu!
 
Enzi za mwalimu....tulitambua maadui watatu wa kupambana nao:
Ujinga
Umaskini na........................
jazia
 
Washirikina ni wagonjwa....(adui wa tatu)..wana ugonjwa kushindwa kufikiri ( over and above ujinga)

Wanaojihusisha na ushirikina ni upande mmoja wa tatizo hili.

Upande mwingine una wale wanaouendekeza kwa kuingiza kwenye mazungumzo yao ya kila siku. Hawa wanaweza kuwa hawashiriki kwenye utamaduni huu, bali wanahuofia kwa kuonyesha nidhamu ya woga kwa kila anasemekana anajihusisha na shughuli za ushirikina.

Nakumbuka nikiwa mtoto, mtaani kwetu kulikuwa na mzee mmoja na mkewe ambaye walisemekana kuwa ni wachawi. Basi sisi watoto (na baadhi ya wakubwa) tulikuwa tunawanazomea kila wakipita. Tulikuwa hatuwaogopi wala kuwatetemekea. Na hakukuwa na mtu yeyote aliyewahi kudhurika na 'mashambulizi' yao (kama yalikuwepo)
 
Jamani ninahitaji viungo vya mganga wa kienyeji, awe mweusi kutoka East Africa. Ukimpata Mtanzania bei ni nzuri zaidi. Kwa kuwa huku West and South Africa wanaamini waganga wa Tanzania ni deal hivyo viungo vyao vitafanikisha mambo yao.

Ukimleta laive utalipwa pension ya maisha.

kwa haraka bei ya viungo vya mganga wa kienyeji ni kama ifuatavyo:

kichwa Tsh 5,000,000
jicho Tsh 1,000,000
mguu Tsh 2,000,000
mkono Tsh 2,000,000
kucha Tsh 2,000,000

Bei itazidi ukimleta mganga maarufu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nami sirini

Duh!
Counter attack au ndio utatuzi wenyewe?
Maana,inawezekana mauaji ya albino yakakomeshwa kwa kuwandoa hawa watu (waganga wa kienyeji).
 
LOL

Sasa kwa nini huo moto asione kwa kumburuza mahakamani? Kwani mpaka ukamshindie makaburi usiku kucha ndio akione cha moto?

...QM, mahakamani kuna mengi, mpaka watafutwe mashahidi, mwendesha mashtaka afungue jalada la kesi, hakimu asiahirishe kesi... yote ya nini hayo. Mtu kakuibia baiskeli, unapuliza pampu tu yeye huko aliko tumbo linaumuka! mambo hapo kwa papo
 
Tatizo ndio litazidi, manake utajuaje kuwa hivi viungo ni vya mganga wa kienyeji. Wauaji wataua yoyote na kusema alikuwa mganga wa kienyeji.
 
Wakubwa tatizo la uchawi kwa Mwafrika ni culture,Uchawi ni moja ya culture yetu na kawaida culture hizi zisizo na msingi hupotea pale jamii inapoelimika.Na kuelimika si lazima ufike chuo kikuu ndio maana tunao wengi waliosoma lakini bado wanaendekeza culture hizi za kipumbavu,wamesoma lakini hawakuelimika ndio maana before their education kwanza wanaiamini tunguli halafu degree zao kiasi hata before exam wanampelekea bibi salamu kijijini afanye mambo.then mfano wa culture kama hizo ni baadhi ya wenzetu wamasai wanapuyanga mijini na mashuka na mikuki,na kule kusini wenzetu wanajitoboa mashikio na midomo,kwanza kumtoboa mtoto ni child abuse no question,kinachotakiwa wajengewe shule na iwekwe sheria ya kuwashitaki hawa wazee wanaowatoboa watoto kule kwa fisadi Mkapa.
 
Back
Top Bottom