Hivi kitchen party zina maana (+vely) kwa wanaoanza ndoa?

Kitchen Parties zimeshika kasi.....hata mashankupe, mashangingi, maveterani yanayojua A to Z and beyond eti yanafanyiwa kitchen party yakiwa yanaolewa!!! nafikiri imekaa kibiashara zaidi=kukusanya zawadi kwa binti/mama/muolewaji. nimejaribu kuhesabu ndoa za marafiki zangu za hivi karibuni...nimegundua zaidi ya nusu zimesambaratika====nafasi ya kitchen ipo wapi?
kuna mama mmoja maarufu sana wa kusherehesha hizo kitchen party Dar,yeye hajaolewa na ana watoto wawili kila mmoja na baba yake,i fail to imagine anafundisha nini kwa maneno na matendo kama si 'akikuzingua rudi nyumbani?'.
siku hizi kuna matangazo lukuki kwenye media yanayoitwa 'VUNJA UKIMYA', je sasa serikali ime-admit mafundisho ya ndoa hakuna hadi watu wa marekani wanatufunda? maana mwisho wa matangazo utasikia 'tangazo hili limewajia kwa hisani ya watu wa marekani'.

.................i submit...........

Kitchen parties zilikuwa zamani.. za sasa ni kufundisha how to be a professional *****!!
 
Inahitaji mjadala wa hali ya juu kuhusu hizi Kitcheni pati, maana zinaonekana zimekaa kibiashara zaidi.
 
Ni biashara ya sociolization na kupata faida materially!..zaidi sana mi niziite ni get-together parties tu!...lakini kwa habari ya ELIMU, hakuna kitu, sanasana hata binti aliyekuwa na maadili anakuwa spoiled kabisa pindi akifanyiwa sanaa hiyo!.

...Kuna kakaangu alimwambia mkewe kuwa hatomruhusu kwenda huko k/party hadi kwanza huyo mwanamke aanze kuyafanya yale yanayofundishwa kule k/party, chumbani kwao!..Maana inaonekana hawa akina mama wanafundisha mabinti zao mambo ambayo wao wenyewe hawayafanyi kwa waume zao!..huh!
 
Ni ujinga tu! Ikifa hii, watakuja na 'master bedroom party'! Mwanadada anatakiwa kuwa na 'hen party' na mwanaume 'bachelor/ stag party/ stag night kabla ya kuoa au kuolewa. Mwanadada anaongeza 'send-off' then ndoa. Wengine wanafanyiwa kitchen party hata kupika chakula cha mchana na usiku hawajui kabisa! Nasikia mafunzo mengine kama vile mara moja moja kwenda kinyume na maumbile - ushetani mtupu!
 
wapendwa, kuna dukuduku ambalo nimekua nalo kwa miaka sasa hasa inapofikia muda wa binti/mama kutaka kufunga harusi. Utakuta kwenye vikundi au kinamama wanalazimishana kuchangishana michango kisa wafanikishe kuwepo kwa kitchen party. Hii inakolea zaidi unapokuta watu waliokuwa wakiishi pamoja na sasa wanawatoto, wanaamua kufunga ndoa, mke (mama) anakomalia afanyiwe kitchen party kwa juhudi kubwa. majilani wanajibana kumchangia kwa kuepuka kutengwa. Sasa hebu nisaidieni, mantiki ya hii hasa ni nini?

Kama ni mafundisho, hivi huyu mama aliyeishi maisha yake yote anaweza kufundishika kwa masaa mawili au manne ya siku hii moja na akabadilika kuwa bora zaidi! Katika pekua pekua nimebahatika kuingia ndani ya mambo yanayotendeka tafadhali jionee mwenyewe kwa kubofya hapa
 
Last edited by a moderator:
Kama ni mafundisho, hivi huyu mama aliyeishi maisha yake yote anaweza kufundishika kwa masaa mawili au manne ya siku hii moja na akabadilika kuwa bora zaidi!

Honestly huwa sioni umuhimu wake labda wanawake watujuze maana wao ndio wahusika zaidi kwenye hili halafu kwenye red hapo najaribu kufikiria ratio ya muda uliyoitaja sijui kama kwa masaa manne anakuwa bora zaidi:confused2: ni mtazamo tu
 
Sikonge naomba nijangie kesho sasa hivi baada ya kazi ngumu na kutukanwa na boss nahitaji VIP:confused2:
 
Honestly huwa sioni umuhimu wake labda wanawake watujuze maana wao ndio wahusika zaidi kwenye hili halafu kwenye red hapo najaribu kufikiria ratio ya muda uliyoitaja sijui kama kwa masaa manne anakuwa bora zaidi:confused2: ni mtazamo tu
The finest, nataka kuamini Msikonge ametaja huo muda akiwa ana 'refer' muda unaochuka kufanyika party tangu kufungua hadi kufunga party! Ki-msingi ni muda mfupi sana too short to imact any noticiable behavioral changes! All in all, ni utumiaji mbaya wa resources, na kama alivyogusia, kuongeza wigo wa zawadi, na pengine 'ufahari'!
 
Haswaa Hero!
 
:thinking::thinking::thinking::thinking:
Utakuta huyo binti/ mama ana ndugu na jamaa haohao, anawakamua kwa kitchen party, anarudi tena kuwa kamua kwa send-off, na kama huyo jamaa (mume mtarajiwa) bado ni wa maeneo hayohayo atawafuata awakamue tena kwa reception! Ole wake atakae shindwa, atamchukia huyo!
 
Lengo kuu la kitchen party ni zawadi. Lengo la pili, tena kwa mbali ndio mafunzo. Hilo la pili kwa hakika halina manufaa makubwa kwa vile samaki alikwishakunjwa angali mbichi. Kaishakauka anapofanyiwa hiyo chicken party.
 
1) ni party kama zilivyo nyingine i.e birthday , anniversary n.k
2) hiyo kuchangishana ni utaratibu waliojiwekea kina mama kila inapotekea shughuli kama hiyo, kwajili ya vyombo vya binti kuanzia maisha
3) sio wanawake wote wanaopata bahat ya kufunga ndoa, siku hii unafurahi pamoja na wanawake wenzio kwa kuwa legally announced Mrs some one,
4) huwa sio mafundisho in such, ni kushare experience na wanawake wenzio ya maisha ya ndoa na wanawake wenio.

NOTE: Sio wote wanaofunga ndoa ni wenyeji katika hii, wengine huwa ni wageni kabisa na that day inakuwa ni kwaajili ya kufundishwa kweli.
 
1) ni party kama zilivyo nyingine i.e birthday , anniversary n.k
2) hiyo kuchangishana ni utaratibu waliojiwekea kina mama kila inapotekea shughuli kama hiyo, kwajili ya vyombo vya binti kuanzia maisha
3) sio wanawake wote wanaopata bahat ya kufunga ndoa, siku hii unafurahi pamoja na wanawake wenzio kwa kuwa legally announced Mrs some one,
4) huwa sio mafundisho in such, ni kushare experience na wanawake wenzio ya maisha ya ndoa na wanawake wenio.
NOTE sio wote wanaofunga ndoa ni wenyeji katika hii, wengine huwa ni wageni kabisa na that day inakuwa ni kwaajili ya kufundishwa kweli.

Hapo kwenye red unamaanisha nini haswa? Au ni namna ya kufanya wizi na kuficha siri?
 
Hapa kwenye kitchen party hakuna la maana linalofanyika ila ni starehe za kibongo zisizo na maana yoyote na utumiaji mbovu wa rasilimali.

Hapo kama ana mtoto shuleni ada wakati mwingine mtu hajamaliza lakini utakuta anafuatwa atoe mchango wa kitchen party.

Cha ajabu ni ukiona yanayofanyika huko hutakaa umheshimu mtu(mmama) kwa heshima uliyokuwa unamheshmu pale mwanzoni.
 
Kicheni party sizipendi ni wizi mtupu kwa kweli...mchango utoe na zawadi upeleke.......halafu zingine utasikia kichefu chefu manake wazee wazima wanakata viuno hadi wanavua nguo..loh ndio kufundwa gani huko!
 
Hapa kwenye kitchen party hakuna la maana linalofanyika ila ni starehe za kibongo zisizo na maana yoyote na utumiaji mbovu wa rasilimali.
Hapo kama ana mtoto shuleni ada wakati mwingine mtu hajamaliza lakini utakuta anafuatwa atoe mchango wa kitchen party.
Cha ajabu ni ukiona yanayofanyika huko hutakaa umheshimu mtu(mmama) kwa heshima uliyokuwa unamheshmu pale mwanzoni.
my self nimefanyiwa hiyo, hakuna jambo baya linalofanyika hapo wala nini! ni mazungumzo ya kawaida tuu
 
Back
Top Bottom