Hivi kitchen party zina maana (+vely) kwa wanaoanza ndoa?

Hapo kwenye red unamaanisha nini haswa? Au ni namna ya kufanya wizi na kuficha siri?
hakuna hata siku moja mwanamke mwenye busara atamfunza binti wizi kwenye ndoa, ukiona hivyo ujue ni tabia ya mtu binafsi tu
 
Kicheni party sizipendi ni wizi mtupu kwa kweli...mchango utoe na zawadi upeleke.......halafu zingine utasikia kichefu chefu manake wazee wazima wanakata viuno hadi wanavua nguo..loh ndio kufundwa gani huko!
pole mwaya, ulienda zipi hizo?!!
nenda zile zinazofanana na jina lako
 
1) ni party kama zilivyo nyingine i.e birthday , anniversary n.k
2) hiyo kuchangishana ni utaratibu waliojiwekea kina mama kila inapotekea shughuli kama hiyo, kwajili ya vyombo vya binti kuanzia maisha
3) sio wanawake wote wanaopata bahat ya kufunga ndoa, siku hii unafurahi pamoja na wanawake wenzio kwa kuwa legally announced Mrs some one,
4) huwa sio mafundisho in such, ni kushare experience na wanawake wenzio ya maisha ya ndoa na wanawake wenio.
NOTE sio wote wanaofunga ndoa ni wenyeji katika hii, wengine huwa ni wageni kabisa na that day inakuwa ni kwaajili ya kufundishwa kweli.

hivi huoni zimekuwa kero, kama mnataka sherehe, send-off haitoshi! Sherehe kama sherehe zingine, kwa nini basi yeye mwenye sherehe asigharamie mwenyewe alafu awaarike ninyi ndio mje kumpa zawadi! badala yake anawalazimisha mumfanyie bila kujua mmekuwa mkia ugali maharage kwa mwezi mzima ili ku'save ada ya mtoto! tena unakuja na kiwango kabila, SH 20,000/ 30,000! mna dhambi ninyi, Mungu anawaona!
 
Wee Msikonge, unategemea watoto wetu waliojitunza wapate wapi vyombo vya kuanzia? Hujui kwamba sasa hivi harusi ni gharama? Wacha uchokozi
 
wanawake wote wastaarabu huwa hawafagilii kitchen party! Nafurahi kujua kumbe kuna watu wengi tu huwa wana kerwa na hili!
 
Wee Msikonge, unategemea watoto wetu waliojitunza wapate wapi vyombo vya kuanzia? Hujui kwamba sasa hivi harusi ni gharama? Wacha uchokozi

kama ni hivyo, kwenye send-off punguzeni vinywaji, muwanunulie vyombo vya kuanzia maisha! hata hivyo, harusi huwa si kitu cha kukurupuka, wanapaswa kuwa wamejiandaa kabla ya kufikilia kuoana, sasa ukitegemea vyombo upate kutokana na zawadi uteletewa vikombe tupu au glasi tupu uanze kulaumu, wakati waswahili walishasema zawadi ni zawadi!
harusi siyo gharama ki hivyo, just arrange a simple wedding, tatizo linakuja pale manapofanya sherehe kwa ajili ya kujionyesha wakati uwezo ni mdogo!
sio uchokozi, deep down ukiamua kufikiri utauona ukweli wa haya!
 
hivi huoni zimekuwa kero, kama mnataka sherehe, send-off haitoshi! Sherehe kama sherehe zingine, kwa nini basi yeye mwenye sherehe asigharamie mwenyewe alafu awaarike ninyi ndio mje kumpa zawadi! badala yake anawalazimisha mumfanyie bila kujua mmekuwa mkia ugali maharage kwa mwezi mzima ili ku'save ada ya mtoto! tena unakuja na kiwango kabila, SH 20,000/ 30,000! mna dhambi ninyi, Mungu anawaona!
ukishatoa hela ya mchango ndo hiyo hiyo inatumika kununulia zawadi, ukija na nyingine ni mapenzi yako binafsi. by the way wanaoletaga zawadi za maana ni wale ndugu na marafiki wa karibu sana the rest ni vibakuli vya plastic na tukanga twepesi my dia
 
Wee Msikonge, unategemea watoto wetu waliojitunza wapate wapi vyombo vya kuanzia? Hujui kwamba sasa hivi harusi ni gharama? Wacha uchokozi

kama hawana vyombo vya kuanzia, then hawako tayari kwa ndoa. Ndoa siyo kitu cha kukurupuka, kinahitaji maandalizi ya kutosha! Unaweze letewa saa za ukutani tupu kama zawadi na hao jamaa zako, sijui utazikataa, kwani zawadi ni zawadi tu!
Just do a simple wedding (send-off), kisha u'save for vyombos, tatizo ni pale mnapotaka harusi za kifahari wakati uwezo hauruhusu!
I'm sure if u allow your brain to think critically, u 'll surely realise that there nothing but the truth to what I'm pre-empting!!!
 
Msikonge umenena..Wanawake na familia za wastaarabu hawafanyi huu upuuzi. Kitchen party is 4 uncivilized people period.
What do they learn out of it kwani ndoa nyingi baada ya hapo hazidumu. How to handle your man or woman in the house
hakufundishwi jamani tumia akili uliyopewa na muumba wako acheni huu uswahili usioleta maendeleo. Kitchen party zina
changia uharibifu mwingi katika sekta nyingi.........
 
kitchen party nyingi sasa wafundaji unakuta wameachika kwenye ndoa zao, watafundisha nini?ndoa haina formula!!
To me iko zaidi kimapato yani zawadi za jikoni+chumbani mana waalikwa hawatoi zawadi nyingi kama ilivyokuwa harusi nyingi zamani zaidi ya kula+kunywa..
 
Kama mtoa mada alivyogusia, kitchen party za siku hizi kwa kweli zimebadilisha kabisa maana ya hiyo sherehe. Kwa sisi ambao tumeolewa zamani, hiyo haikuwa sherehe kama hizi za siku hizi (ukumbini, mziki mnene, zawadi za kifahari, n.k). Nakumbuka wakati nataka kuolewa, mama yangu aliwaita wamama walikuwa kama 10 hivi, pia kulikuwa na mama zangu wakubwa na mashangazi kwa hiyo idadi ilikuwa kama 20 hivi. waliandaa chakula na vinywaji kidogo, wakaniita chumbani (Sio siting room) ni chumbani. Wakaanza kuongea.
Nilifundishwa mambo mengi sana ambayo kwa asilimia kubwa sana naamini yananisaidia sana katika ndoa yangu, maana nayakumbuka mpaka sasa. Na kwa kusema kweli, nimehudhuria kitchen party nyingi sana za siku hizi, sijawahi kupata mafundisho kama yale niliyoyapata siku ya kitchen party yangu.
Mi naona hizi kitchen party za siku hizi tuzitafutie jina jingine.
 
Hongera mtoa mada; kwa hakika mada hii ibebainisha ukweli wa hizi kitchen party hazina maadili mema kwa muolewa na ndizo kwa kiasi zinachangia ndoa za leo kutodumu.Maana halisi ya hii sherehe imepotoshwa kwa kiasi kikubwa na kukosa umaana wake. Kitchen party(sherehe ya kumufunda mwali) ilikuwa ni ya kina mama tu waliokuwa na uelewa wa kufunda(kufundisha) mambo mema ya ndoa kwa muolewa; wamaume na watoto hawakuruhusiwa kabisa kuwepo; sasa leo sherehe inahusisha paka wanaume na watoto; pia imekuwa si yakufundisha mambo muhimu ya ndoa bali ni matusi tupu.Nafikili sasa jamii inahitaji kukumbushwa turudie utamaduni wetu.
 
wapendwa, kuna dukuduku ambalo nimekua nalo kwa miaka sasa hasa inapofikia muda wa binti/mama kutaka kufunga harusi. Utakuta kwenye vikundi au kinamama wanalazimishana kuchangishana michango kisa wafanikishe kuwepo kwa kitchen party. Hii inakolea zaidi unapokuta watu waliokuwa wakiishi pamoja na sasa wanawatoto, wanaamua kufunga ndoa, mke (mama) anakomalia afanyiwe kitchen party kwa juhudi kubwa. majilani wanajibana kumchangia kwa kuepuka kutengwa. Sasa hebu nisaidieni, mantiki ya hii hasa ni nini?
Kama ni mafundisho, hivi huyu mama aliyeishi maisha yake yote anaweza kufundishika kwa masaa mawili au manne ya siku hii moja na akabadilika kuwa bora zaidi! Katika pekua pekua nimebahatika kuingia ndani ya mambo yanayotendeka tafadhali jionee mwenyewe kwa kubofya hapa
: YouTube - NICHAKO MOYEWE KIKATE -HOT KIUNO..

Kwanza huyo anayekata kioni ana huhakika kuwa huyo mlengwa anamzidi? Halafu mafunzo hayo si ya vitendo kwani huyo mkatikaji alitakiwa kila style anayoonyesha iwe live kwa maana ya kwamba awe amebana original shaft. Na hili sherehe isichukue muda mrefu basi kama kuna style 20 basi itabidi kuwe na pair 20 - original shaft 10 na original samosa za nyama ya kusaga 10. Kukata kiono namna hiyo si kwanza ni mzuri kwenye futi 6!!

Faida yake ni kumwambia mtarajiwa kuwa kuna maana mbili za kitchen - chumbani na jikoni kwenyewe - hii ni slang ya wanawake wetu kwani hufananisha jiko na chumbani - kule kuna kuchambua, kupika, kupakuwa na kula vile vile. Hasara ni kwamba mengine ni ushetani kama kwenda kinyume na maumbile mara moja moja. RC wanasemina za ndoa, ni nzuri mno kuliko hiyo kitchen party maanake kuna somo la reproduction na explore sensitive parts of the sex organs and how to make preparations and the like!

Kama mwanamke ni RC, na amehudhuria semina ya ndoa, basi kitchen party haitakiwi; kama ni hizo zawadi si wampelekee siku ya send off na reception!!!!
 
Nakubaliana nayo, hayo mafundisho ya ndoa ktk sehemu zetu za ibada yanajitosheleza, huko kwenye kitchen party ni upuuzi mtupu wanaoufuata!
 
Hongera mtoa mada; kwa hakika mada hii ibebainisha ukweli wa hizi kitchen party hazina maadili mema kwa muolewa na ndizo kwa kiasi zinachangia ndoa za leo kutodumu.Maana halisi ya hii sherehe imepotoshwa kwa kiasi kikubwa na kukosa umaana wake. Kitchen party(sherehe ya kumufunda mwali) ilikuwa ni ya kina mama tu waliokuwa na uelewa wa kufunda(kufundisha) mambo mema ya ndoa kwa muolewa; wamaume na watoto hawakuruhusiwa kabisa kuwepo; sasa leo sherehe inahusisha paka wanaume na watoto; pia imekuwa si yakufundisha mambo muhimu ya ndoa bali ni matusi tupu.Nafikili sasa jamii inahitaji kukumbushwa turudie utamaduni wetu.

Nafarijika kuona kumbe ni wengi tunakerwa na vurugu hizi za kitchen party, PAKAWA yeye ndio ameenda mbali zaidi, your msg is loud and clear, n I think our feeling is mutual!
Sasa, nafikiri umefika muda tuanzishe kampeni ya ku'barn' huu upuuzi, or else, warejee kwenye maana halisi ya wale wazee wetu waliojaa hekima na busara mpaka walipofikia kuanzisha ufundaji huu, hapo ndo tuyaruhusu kuendelea!
Nakubaliana na wachangia maada kama mwanamayu, Belinda, Fixedpt, Hero, Mkandya, 1st lady, Antibiotix, nk kuwa jamii yetu sasa inabidi irudie misaafu yake katika imani zao, & they 'd stick to their mafundisho.
Na kwa wale ambao Kitchen party is a MUST issue, kama Lady N, Mentee nk,basi they 'd review the puporse of its existence ili maana halisi na heshima yake irudi, ili hata inapotokea tunaaga home kwenda kwenye shughuli hizo basi jamii ituheshimu na kututhamini!
Thank you very much for giving me courage by letting me know that there is a lot of my fellow citzens that feel the same about this mada & they are ready to positively impact our motherland!
I salute you all!!!!
 
Binafsi huwa nakereka nikisikiliza baadhi ya mambo wanayofunzwa wanandoa wa kike watarajiwa katika kitchen parties. Hata hivyo, nakubali kuwa kuna Kitchen Party nyingine wanandoa watarajiwa hufunzwa mambo muhimu ya kuwawezesha kudumisha ndoa zao.

Kitchen parties zinazonikera ni zile zinazotia mkazo zaidi katika ngono tu. Binti atafundishwa jinsi ya kulala kwenye godoro, mara jinsi ya 'kula koni', mara jinsi ya kutumia kidole, mara mafiga matatu,.........

Sikatai kuwa ngono ni jambo muhimu na kiunganishi katika ndoa; lakini napinga kulifanya ndilo pekee linaloweza kudumisha ndoa.

Naomba mawazo yenu.
 
usizubaike na kitchen party kaka yangu watu wanafanya ili kujiburudisha tu na kupata zawadi mafunzo huwa hayatolewi hadharani vile, vinavyofanyika pale vyote ni kujifurahisha tu
 
Ndugu zangu ninaomba kuuliza zaman kulikuwa na unyago hii ilikuwa ina2mika sana kwa ajili ya kuwafunza wanawake ila kutokana na maendeleo ndo kunaki2 kikaja kinaitwa kichen part nilikuwa ninauliza mana hz kichen part ukiwa nje hayo maneno wanayo2mia kumuelekeza mwanamke yan huwa hayana nadhaa mana dah! Hebu 2saidiane mm ninaona wanamwalibu mwanamke labda anachopata ni vyombo 2uu ila wanamtia kibur 2uu au mnaonaje?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom