Hivi kitchen party zina maana (+vely) kwa wanaoanza ndoa?

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,892
Wakuu nimekuwa nikisikia dada zangu wakifanyiwa kitchen party pale tu wanapokaribia kuolewa hata kwa yule aliyekwisha zaa anapofika hatua ya kubariki ndoa yake anafanyiwa kitchen party.Sasa swali Huyu ambaye alishaolewa bila harusi kitchen party ya nini?

Je kama kwenye kitchen party wanafundishwa maadili ya kumheshimu mume wake mbona wakiolewa wanayasahaho yote bila hata kuyafuata walioambiwa na waliowafanyia kitchen party?

Kitchen Party ni utamaduni wetu au umeigwa kwenye mitandao.

Wakuu nisaidieni maana yake naweza nisisfanyiwe kitchen party siku nikipata mwenza.
 
Mzee, kitchen party ni unyago mamboleo kwa wamama. Ni mafundisho ya jinsi ya kutunza mume na nyumba ya ndoa. Mafunzo haya yanaweza kurudiwa kwa vipindi kadha wa kadha kama refresher course. Ndo maana unakuta hata wale waliokwishaolewa wanaweza kurudi tena kukumbushwa au kufundwa mapya ambayo sayansi na teknolojia imeyavumbua.

Yapo mazuri mengi huko kwenye KP lakini pia kuna mikengeuko ya aina yake. Yategemea walimu wao kwani si wote ni wazuri.
 
Mzee, kitchen party ni unyago mamboleo kwa wamama. Ni mafundisho ya jinsi ya kutunza mume na nyumba ya ndoa. Mafunzo haya yanaweza kurudiwa kwa vipindi kadha wa kadha kama refresher course. Ndo maana unakuta hata wale waliokwishaolewa wanaweza kurudi tena kukumbushwa au kufundwa mapya ambayo sayansi na teknolojia imeyavumbua. Yapo mazuri mengi huko kwenye KP lakini pia kuna mikengeuko ya aina yake. Yategemea walimu wao kwani si wote ni wazuri.

Hivi Babuyao umemsoma vizuri Chaku?

Mi nadhani Chaku pia ni dada, maana kwenye msitari wa mwisho wa hoja yake anasema kuwa, (namnunkuu) "Wakuu nisaidieni maana yake naweza nisisfanyiwe kitchen party siku nikipata mwenza"

Kwa kuzingatia hilo, naomba usimwite mzee, kama nilivyokusoma kwenye hiyo nyekundu, usije ukamkosesha mchumba mwenzio buuuuuuure, mwaya!
 
Last edited:
Jamani nilikuwa najua siku zote Chaku ni mwanaume sorry for that chaku sasa nimeelewa.

Kwa kweli kitchen party ni ya muhimu sana na ndo maana ukienda kwenye hizo kitchen party unakutana na watu wenye umri mbalimbali,wasichana ambao hawajaolewa,mama zetu ambao wana miaka mingi kwenye ndoa zao,na wa umri wa kati pia,na lengo lao ni kufundisha/kumfunda yule ambae anenda kuolewa na pia hata wale wengine ambao wako pia kwenye ndoa kwa muda mrefu pia wanakumbushwa maana yapo ambayo wamesahau na mengine pia hawayajui.

kwa hiyo kitchen party ni za muhimu sana maana ukipata walimu wazuri utapata pia mambo mazuri ila kuna walimu wengine jamani mmmhhh,usipime yaani hayo mafundisho yao yanaweza kukuacha hoi,kwa ushauri mwingine siku ukialikwa mahali kwenye kitchen party hudhuria.
 
msitari wa mwisho wa hoja yake anasema kuwa, (namnunkuu) "Wakuu nisaidieni maana yake naweza nisisfanyiwe kitchen party siku nikipata mwenza"

Kwa kuzingatia hilo, naomba usimwite mzee, kama nilivyokusoma kwenye hiyo nyekundu, usije ukamkosesha mchumba mwenzio buuuuuuure, mwaya!

Nakushuru ndugu yangu, hii tabia ya kukurupuka kujibu bila ya kusoma kwa makini, inapelekea kupata majibu ya hovyo hovyo
 
sidhan kama ina umuhimu has kwa mtu aliyeolewa tayari, maana siku hizi madogo (wasichana wanyange) wanafanya kila liwezekanalo kujifunza haya mambo ya kikubwa hata kama umri wao ni mdogo.
utakuta kitoto cha miaka 15 kinajua mambo kuliko hata mama yake. looooh! si hatari hiyo?
evidence!
we siunacheki wazee wanavyopenda madogo?
 
Jamani nilikuwa najua siku zote Chaku ni mwanaume sorry for that chaku sasa nimeelewa.

Nadhani na Avatar pia inaweza kuchangia kumislead kama mtu hayupo makini kuangalia vizuri pointers zote za gender. Kama huna uhakika na gender ya member pengine inaweza kuwa vizuri kuepuka kuchangia on a gender specific basis.
 
Wakuu nimekuwa nikisikia dada zangu wakifanyiwa kitchen party pale tu wanapokaribia kuolewa hata kwa yule aliyekwisha zaa anapofika hatua ya kubariki ndoa yake anafanyiwa kitchen party.Sasa swali Huyu ambaye alishaolewa bila harusi kitchen party ya nini?

Je kama kwenye kitchen party wanafundishwa maadili ya kumheshimu mume wake mbona wakiolewa wanayasahaho yote bila hata kuyafuata walioambiwa na waliowafanyia kitchen party?

Kitchen Party ni utamaduni wetu au umeigwa kwenye mitandao.

Wakuu nisaidieni maana yake naweza nisisfanyiwe kitchen party siku nikipata mwenza.

kwani Chaku ungependa kufanyiwa iyo kitu, kuna kitu hukijui?
 
wadada wanafundwa namna ya kutunza familia lakini lengo hasa ni kuchangishana samani na zawadi za kum support mwezao pindi akijiandaa kuolewa.
 
Kitchen Parties zimeshika kasi.....hata mashankupe, mashangingi, maveterani yanayojua A to Z and beyond eti yanafanyiwa kitchen party yakiwa yanaolewa!!! nafikiri imekaa kibiashara zaidi=kukusanya zawadi kwa binti/mama/muolewaji. nimejaribu kuhesabu ndoa za marafiki zangu za hivi karibuni...nimegundua zaidi ya nusu zimesambaratika====nafasi ya kitchen ipo wapi?

kuna mama mmoja maarufu sana wa kusherehesha hizo kitchen party Dar,yeye hajaolewa na ana watoto wawili kila mmoja na baba yake,i fail to imagine anafundisha nini kwa maneno na matendo kama si 'akikuzingua rudi nyumbani?'.

siku hizi kuna matangazo lukuki kwenye media yanayoitwa 'VUNJA UKIMYA', je sasa serikali ime-admit mafundisho ya ndoa hakuna hadi watu wa marekani wanatufunda? maana mwisho wa matangazo utasikia 'tangazo hili limewajia kwa hisani ya watu wa marekani'.

.................i submit...........
 
i dont see any problem with it, as long as i go there to have fun and share some light jokes with my woman folks and celebrate my girlfriend's step to marriage, also its a chance to get kitchen valuables and furthermore.

...there are lots and tons of religious themed kitchen parties.. its correct that we can learn everything that day, but its also important that woman have their own gathering to dance and celebrate together, i really do think mama mzazi should give their daughters home guidance prior to sherehe ya vyombo vya jikoni
 
Kitchen Parties zimeshika kasi.....hata mashankupe, mashangingi, maveterani yanayojua A to Z and beyond eti yanafanyiwa kitchen party yakiwa yanaolewa!!! nafikiri imekaa kibiashara zaidi=kukusanya zawadi kwa binti/mama/muolewaji. nimejaribu kuhesabu ndoa za marafiki zangu za hivi karibuni...nimegundua zaidi ya nusu zimesambaratika====nafasi ya kitchen ipo wapi?
kuna mama mmoja maarufu sana wa kusherehesha hizo kitchen party Dar,yeye hajaolewa na ana watoto wawili kila mmoja na baba yake,i fail to imagine anafundisha nini kwa maneno na matendo kama si 'akikuzingua rudi nyumbani?'.
siku hizi kuna matangazo lukuki kwenye media yanayoitwa 'VUNJA UKIMYA', je sasa serikali ime-admit mafundisho ya ndoa hakuna hadi watu wa marekani wanatufunda? maana mwisho wa matangazo utasikia 'tangazo hili limewajia kwa hisani ya watu wa marekani'.

.................i submit...........

elimu haina mwisho..........................
 
mwingine anafanya hiyo sijui ndo sherehe ya jikoni, then haolewi wala nini, kibiashara zaidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom