hivi inawezekana ama ni kwangu tu?

sijawah hata kumuona zaid ya tulivykutana kwenye gari basi. Hapa mimi najiuliza kwanini hali kama hii itokee? mbona mume wangu hanijali jamani ama nilikosea kupenda? nimesali sana kaka na nimelia sana tena mpaka nimesema silii tena lakini mume wangu hanionyeshi hata wema ambao wengine wananionyesha.

siyo mwanaume wa kwanza kunitaka huyu huwa naruka viunz sana tu lakni kwanini mume wangu hanion kama n wa thamani kam wengne wanavyoniona?

kaka yangu hebu jiulize wewe kama mkaka hata siku moja mkeo haja kusifia kwa jambo lolote lakin kila siku wanawake unaokutana nao wanakusifu tena kwa vitu ambavyo vipo wazi utajiskiaje?
Hiyo hali huwa inajitokez ndio mrembo, ila unajipa moyo tu, ni mambo ya mpito kwenye ndoa, jaribu kufikiria mazuri aliyokufanyia, coz, kati ya hayo mabaya unayoyaona kwake lazima kuna mazuri, hakuna binadamu perfect,na uspende kumfananisha mumeo na wanaume wengine kila mtu ni unique in their own way, wanaume wengine wana upendo wa kweli mioyoni mwao lakini hawana mzuka wa kuiga mambo ya kizungu ya kufunguliana milango na mengineyo....but usiwe na wasiwasi itapita wewe ni binadamu na hiyo ni hali ya kawaida
 
Wapenzi wana mmu najitokeza mara ya kwanza hapa jukwaani nikiwa kama memba baada ta kuingia kama mgeni ka siku nyingi sana.

leo hii kilichonifanya nitamani kuingia humu ni hiki hapa, niko safarini naenda msibani Arusha wifi yangu kafiwa na mumewe. cha ajabu wk nzima iliyopita ndani kwangu hakukaliki, kila saa ugomvi tu amani hakuna wala raha hakuna nimejikuta kama naona ndoa ni chungu. sasa jana wakati niko ndani ya basi la mtei niligbahatika kukaa siti moja na baba mmoja siyo mzee ila siyo kijana ni kama wa miaka 45. Tulipokuwa maeneo ya king'atit basi liliharibika na kwakua huyu baba ni mwenyeji wa arusha akasema usiwe na tabu kwasababu wewe ni mgeni miye nitakusindikiza hadi huko. kweli aliita gari na nikapata lift, kwakweli care za huyu baba, zilinipagawisha sana, nikakuta kule kunifungulia mlango na kufunga, kule kunibebea kipochi changu, kunikaribisha tu kasupu b4 sijafika eneo la tukio kulinifanya nimuone mtu mwema sana nikajikuta naanza kumfananisha na hubby ambaye hivyo hafanyi kabisa.

kibaya zaid hapa msibani kaja kuniulia hali na kasalimiana na wifi vizuri, na kisha baada ya mazishi nikamsindikiza kwenye gari, jamani amenionyesha upendo ambao sijawah kuupata kwenye ndoa sasa amekwisha ondoka ila najiuliza hali hii imewah kukuta? yaani inafika mahali mtu unasema natamani ningeolewaga na huyu au ni kwangu tu? imagine kaniambia kesho atakuja kunichukua anipeleke stendi jamani nifanyeje mbona kama nataka kuanguka dhambini? Siyo kwamba simpendi mr ila tu maudhi ya ndani ndio yananifanya nianze kumcompea

Nakuhakikishia kuwa hizo ni sifa za shetani tu na si vinginevyo!Kavuruga amani wiki nzima nyumbani kwako halafu kakukutanisha na huyo mbaba ili uchanganyikiwe na uisaliti ndoa yako.
Chonde chonde, hangaikia ndoa yako, delete uyo mwanaume kwenye kichwa yako mapemaa ili umshinde shetani na pindi mawazo yako yakielekea kwake kemea!
 
Ulichonacho ni cha thamani zaidi kuliko huyo uliyekutana naye kwenye gari.Shika sana ulichonacho.
Vunja ukimya sema na mume wako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ukweli Ni Kwamba' Usimjaji Mtu Kwa Jinsi Anavyoonekana Au Anavyokutendea Kwa Siku Moja Tu. Kumfaham Mtu Vizuri Inachukua Time Sana May Be Utakapokuwa Naye Karibu Mara Nyingi Zaidi. Mume Wako Ni Mtu Wa Muhimu Sana Coz Una Noleji Kubwa Juu Yake, Unafahamu Mapungufu Na Mazuri Yake Hivyo Una Uwezo Mkubwa Wa Kuyabalansi Kwa Kadiri Iwezekanavyo. So Deal With Your Husband Pliz! Tunapendezwa na wengi sana barabarani, je hao wote ndo tuwe nao? tutakuwa na wangapi? Hebu Jiulize Umeshapendezwa Na Wangapi Katika Maisha Yako. HAYA BWANA!!!
 
nina miaka 35, kuoa sijaoa ila sasa sina ujanja itabidi nioe kukamilisha ratiba, sababu ni uwezo wa kufikiri wa nyie wapendwa wetu, mfanyie mwanamke mema mengi muudhi mara moja atokee mtu amfurahishe mara moja huyo wa mara moja atapeta. ndio maana kwa muda wote nilikuwa opputunist nikiutumia udhaifu na nilifanikiwa ila haramu itabaki kuwa haramu na halali itabaki kuwa halali.
 
Hakuna mkamilifu! Una muona ana kujali sababu ajakuweka ndani! Najua hata kabla hauja olewa mmewako uliona ana kujali sana! Usiache mbachao kwa::::::::::::::::::::::::::::::::

na hapa wanawake wengi ndipo huwa sehemu ya kuwapata, akisha umizwa tu, yan ana kuwa mwepesi ningekuwa huyo mzee ninge akikisha unaingia kwenye mtego alaf baadae na kuongoza toba.
 
Hebu nijibu maswali haya;
- Jee unayajuwa mabaya ya huyu bwana mgeni? Naam unayajuwa ya Mr/
- Jee huyu bwana angekuwa alimasi kama unavyomuona jee wangapi anao waliovutwa na wema wake?
- Mr alipokuaproach mara ya kwanza unakumbuka mema aliyokufanyia, lakini kabadilika jee huyu yeye itakuwaje?
- Jee gharama aliyotumia huyu bwana kukuteka moyo inalingana kiasi gani na anayoendelea kutowa huyo Mr.
-Jee Mr nae akitokea mwanamke nae akiwa tayari kujidai mbele yake ana haki ya kuhisi kama wewe?

Mlani shetani kwani huyo katumwa na shetani basi.

kaka nakushukuru na pia samahani kwa kuwa mbaali na mtandao na naomba nikujibu ifuatavyo:-
-siyajui mema wala mabaya ya huyu bwana but ya mr nayajua vizuri tu
-kama mwanaume wapo wengi tu waliovutika kwake ama aliovutiwa nao
-nitakaa pembeni
-huwez kulinganisha manake ya mume imezid
-naye sipendi afanye hivyo

mkuu ngoja nikwambie kitu kama umeisoma vizuri post yangu ni metamatisha kwa kusema siyo kwamba simpendi mume wangu, na pia nimebainisha mambo ambayo mimi kama mwanamke yanaweza kunikuta na kusababisha niingie dhambini.

kaka sikuolewa staili ambayo tuichukua gest ama disco, na katika wanawake wavumulivu naweza kusema miye nami nimo na pia wanaojali familia ila nimeamini kweli kua penye miti hapana wajenzi. na kweli Mungu hakupi vyote.
 
Pole sana, vp lakini unamjali mumeo kama unavyotaka akujali, unamfungulia mlango??unamsalimu vizuri??unafanya kipi kinachoonesha uhitaji wako wa upendo uutakao??
Unajua kwamba na huyo mzee kwa mkewe ni kama mmeo kwako??
Una watoto??unahisi utawatendea haki kwa kutembea nje ya ndoa??
Tulia na Mungu wako na mwombe yeye akurekebishie ndoa yako, na tenda matendo mema naye atatenda utakavyo
Amina

niwie radhi kwa kuchelewa kukujibu, mkuu miye naweza kujiita mwanaamke na mke bora, sijisifu bali hata ndugu na marafiki wananisifu kwa hilo. Tatizo ni kwamba mwenzangu naona pesa zinamchanganya sana kiasi kwamba anathamni marafiki kuliko mimi.

mume wangu hajui hata mara ya mwisho alinunua leso lini, wala hajui hata kujifunika kitandani ni kazi yangu kuamka na kumfunika kila siku, kaka sijui dada nafanya kazi kwenye shirika la kimataifa maisha yangu kiuwezo ni mazuri sana kiasi kwamba mume hajawah kusumbuka kuombwa hela wala nini na nawajali wakwe zangu kuliko mwanamke yeyote ila jamani mume wangu na pombe na marafiki na hivi anavijisenti nakoma.
 
Kwa nini usimfanye mumeo afikie huko
Kwa nini usifikirie kubadilisha ndoa yako unafikiria kutoka nje ya ndoa
Kwa nini unamkaribisha mvamizi mdudu alaye nafaka katika ghala lako la mahindi
Unategemea huyo mdudu atakuwa na huruma na wewe wakati umemkaribisha
Kwa nini unataka kujiangusha kw amakusudi kwa wema wa siku moja na sifa za kijinga za siku moja za fisi anamsifia mwanakondoo kuwa amependeza na angependa aende nae porini akampe chakula
Jiepushe na jiweke mbali na huo wema wa fisi mwenye uchu na njaa ambaye yuko tayari kurarua kila kilicho mbele yake
Huwa tunapenda sana kutumia udhaifu kutafuta kile tukipendacho na huyo jamaa kashaona opportunity na lazima aitumie so kuwa makini sana

kaka Mr Rocky naomba nikujuze kitu fulani hivi manake post yako hii imenifanya niseme hata nisiyotaka kuyasema.

Mimi na mr tumeoana 5 yrs back by then nilikuwa na miaka 27 nilikuwa najiendeleza kielimu ngazi ya masters na ni mfanyakazi kwenye moja ya mashirika ya UN. mpaka hapo nilikwa ni binti ambaye ni virgin na huwez kuamini niliolewa na mwanaume mwenye mtoto tayari. na nilimpenda huyu binti kiasi cha yeye kuamua kuishi na mimi kama mama yake na mpaka leo naish nae. Mimi ni mwanamke wa kikristo ambaye nilisha sema sitokaa nivue nguo yangu kwa mwanaume zaid ya mmoja maishani mwangu na mpaka leo hii sijawah wala sitarajii. u can have an idea ya wanaume ambao nakutana nao ama wanaonitongoza ni wengi sana tena wenye pesa but kwangu miye hilo huwa siafiki kwani si kwamba nalinda heshima ya mume la hasha ila natunza heshima ya mwili wangu and thats all.

nilalamikapo juu ya care za mume wangu kaka nimejitahd sana, sijawah hata siku moja kutotimiza wajibu kwa familia yangu, lakini sioni mwenzangu akifanya hivyo. nafikir kwa jinsi alivyo na mihela mingi basi yeye kaamua marafiki na pombe ni bora kuliko miye mkewe. nimeshasema na kulia sana na kusali sana sasa nimefika mwisho nasubiria neema ya mungu tu ila ukweli ni kwamba wanaume mnashawish wake zenu kutoka nje ya ndoa.
 
Last edited by a moderator:
Dah pole sana mdada! hebu rudi usome tena ushauri wa Mr Rocky
Haya na mie nakupigilia msumari tena wa moto.... pamoja na kwamba sipo kwenye ndoa ila naomba nikupe kaushauri kadogo... kuna msemo unasema "usione soo sema naye" huu msemo ni mzuri kwa maana ya kwamba uwe muwazi kwa mumeo, usimuogope wala kuona aibu... tafuta siku moja iliyona furaha na iliyotulia toka out na mumeo mfanyie vitu ambavyo anapendelea na vitakavyo mfurahisha. then after muelezee ni jinsi gani unapenda utendewe/ufanyiwe... huenda hata yeye hajui kama ukifanyiwa hivo unafurahi.. mwambie napenda uwe unanifanyia hivi na vile.. ila usimwambie vitu vilivyocomplicated...
Chonde chonde usithubutu kuisaliti ndoa yako kisa ma-care ya siku moja tena co siku bali masaa.... huyo mbaba ni fataki na alifanya hivo ili akupate, CHEZEYA FATAKI WEWE naona hujakutana na mafataki. mwisho wa siku akikupata ana-kudump kama takataka..... USITEME BIG G KWA KARANGA ZA KUONJESHA.... kwa style hiyo utachezewa na kila takayepita mbele yake!

dada nakushukuru sana, kwakua hujaolewa siwez sema sana lakin utakapoolewa utajua kwanini nimewaza hivi. Binafsi kwa status yangu siyo mtu wa kutembea na wanaume hovyo hovyo kwani ni mke wamtu na mama na pia najipenda sana na hasa napenda kutunza heshima ya mwili wangu.

lakini jamani wanaume wanakosea sana wanapoacha kututhamini.....................jamani naomba nisiseme sana manake nalia kwa uchungu naamani siku nkulete kwangu uone hali ilivyo
 
Kwa maelezo ya kisa chako ninashawishika kwa aslimia 100 wewe ndio tatizo kwenye ndoa yako na si mumeo kwa maneno machache inaonekana HUJATULIA unahitaji KUPEPEWA.Unachokitafuta utakipata tu.

ndugu yangu TUMY sidhani kama kwa kalamu yangu waweza nihukumu, lakin sasa naamin kuwa asiyekujua hakuthamini. so ni sawa tu
 
Last edited by a moderator:
Umenishangaza sana manshiroo (hapo kwa redi), yaani wewe unachopenda ni kusifiwa, kubebewa pochi, kufunguliwa mlango wa gari .... loh! very artificial life!! wengi wenye mtizamo kama wako wameishia kuumizwa! Yaani hata unashindwa kutambua kuwa hizo zote ni gia za kukupata? kalaghabaho!

ndugu wala usishangae maneno yangu ama sentensi hiyo imeficha mengi sana ndani yake ambayo siwez kuyasema. hivi unafikir mume wangu hana mazuri anayoyafanya? ama wadahni nina underestimate mapungufu ya kibinadamu? la hasha najua fika kuwa hata hawa wanaotongoza ni hao hao but inaumiza sana pale unapojitoa kisha mwenzi wako haitoi aisee
 
kaka Mr Rocky naomba nikujuze kitu fulani hivi manake post yako hii imenifanya niseme hata nisiyotaka kuyasema.

Mimi na mr tumeoana 5 yrs back by then nilikuwa na miaka 27 nilikuwa najiendeleza kielimu ngazi ya masters na ni mfanyakazi kwenye moja ya mashirika ya UN. mpaka hapo nilikwa ni binti ambaye ni virgin na huwez kuamini niliolewa na mwanaume mwenye mtoto tayari. na nilimpenda huyu binti kiasi cha yeye kuamua kuishi na mimi kama mama yake na mpaka leo naish nae. Mimi ni mwanamke wa kikristo ambaye nilisha sema sitokaa nivue nguo yangu kwa mwanaume zaid ya mmoja maishani mwangu na mpaka leo hii sijawah wala sitarajii. u can have an idea ya wanaume ambao nakutana nao ama wanaonitongoza ni wengi sana tena wenye pesa but kwangu miye hilo huwa siafiki kwani si kwamba nalinda heshima ya mume la hasha ila natunza heshima ya mwili wangu and thats all.

nilalamikapo juu ya care za mume wangu kaka nimejitahd sana, sijawah hata siku moja kutotimiza wajibu kwa familia yangu, lakini sioni mwenzangu akifanya hivyo. nafikir kwa jinsi alivyo na mihela mingi basi yeye kaamua marafiki na pombe ni bora kuliko miye mkewe. nimeshasema na kulia sana na kusali sana sasa nimefika mwisho nasubiria neema ya mungu tu ila ukweli ni kwamba wanaume mnashawish wake zenu kutoka nje ya ndoa.

manshiroo asante sana kwa ufafanuzi wako na nimekupata
Ila naomba kabla hujaamua kutoka nje au kuupokea wema wa huyo baba aliyekuja kwako jiulize maswali mengi sana kichwani mwako. Kama uliweza kuapa kuwa hutomvulia mwanaume yeyote nguo zaidi ya mumeo nenda na kiapo chako na wala usikiache
Nilalokuambia usidanganyike huwezi jua huyo jamaa anataka nini kwako au ana matatizo gani kiasi cha kuamua kukufanyia hayo
Anaweza kwa vigezo vyako akawa mwanaume wa kukucare sana na kukupenda upendo wa dhati ila vile vile anaweza kuwa nyoka ndani ya ngozi yake
Jiulize na jihoji mara mia mia kabla ya kukuba,li kuanguka na kuusaliti utu wako
Na jingine hebu siku moja jifunge umuombe outing mumeo mwende nae mbali na hizi kelele za magari na watu mkae mahali upasuke kila lililo moyoni mwako na mweleze kwa utaratibu kuwa hili na hili haliko sawa na jishushe mwambie kama na wewe kuna sehem uko wrong anzeni upya kama wakati wa uchumba
Ikiwork out you have your husband kama sio hapo sitakuwa na la kukushauri tena
 
ahsante sana kwa ushauri mzuri najua siwez kutoka na huyu mtu nisiyemjua na ambaye si mume wangu kamwe kwani maisha hayapo kwenye kucare tu yapo pia katika sehem nyingine. ila hapo kwenye red mbona kama umenawa mikono mkuu? so inamaana hata humu jf nisitegemee mawazo ya kunijenga tena?
 
Nimetoa ushauri wangu kwa kweli manshiroo na naomba uuzingatie
Nipo kwa wakati wote na wengine wapo watakupa ushauri zaidi na zaidi hatutachoka
 
Last edited by a moderator:
itakuwaje uchanganyikiwe na mapenzi ya siku moja?unahuakika gani kama anamfanyia hivyo mkewe au mpenzi wake?mpende mumeo hayo ni mapungufu aliyonayo yaweke sawa..

MWANAMKE MPUMBAVU UIBOMOA NYUMBA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE..
 
ndugu yangu TUMY sidhani kama kwa kalamu yangu waweza nihukumu, lakin sasa naamin kuwa asiyekujua hakuthamini. so ni sawa tu

Ndugu yangu Manshiroo. inawezekana usemi wako kwamba asiye kujua hakuthamini ukawa ni sahihi in some circumstances ila kwa ishu yako naendelea kusimama kwenye kile nilichokisema kwa kuwa umeonyesha udhaifu wa kupitiliza na kwa maneno mengine wewe pia si mwaminifu, sina lengo la kumtetea mumeo ila kaa ukijua kwenye ndoa kuna ups and down sasa kama wewe tatizo kidogo tayari umeshaanza kuonyesha ufa kiasi cha kukiri wazi unaelekea kutaka kuanguka dhambini huoni kama hilo ni tatizo, sasa huyo umekutana nae siku moja ungekuwa na unakaa huko wiki nzima sio ndio ungesahau na nyumba yako kabisa, kaa chini na mumeo mumalize matatizo yenu huko unakoona wewe ni salama usikute wenzako nao wanatafuta watatokaje.
Hivi kama wewe ni mtu mzima na una akili timamu kabisa unataka kuniambia hujui what is behind that man,use ur common sense utaruka ruka hivyo mpaka lini, angalia kuna magonjwa ndugu yangu lakini pia kumbuka mwanamke mjinga ataivunja nyumba yake yeye mwenyewe vivyo vivyo kwa mwanaume.
Pamoja na kwamba hatujui una miaka mingapi kwenye ndoa yako, ila hata kama mumeo ana matatizo text yako imetoa picha ya wewe ni mtu wa aina gani na kweli unahitaji ushauri tena serious ama kama si hivyo kuna mengi yako nyuma ya pazia labda.
My take:Tulia jenga ndoa yako wacha hayo mawazo ya kuruka ruka hayatakufikisha popote.
Bye.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom