Brown Mduma
Senior Member
- Sep 29, 2020
- 180
- 283
Nilikutana nae mara ya kwanza ndani ya Daladala za Mbezi mwisho .Nikamuomba namba ya simu baada ya salamu na maongezi akanipa.
Tulipoachana nikampigia simu baada ya siku 2-3 nikamueleza ukweli kuw nmemuelewa na kumpenda.Baada ya mvutano wa siku nyingi hatimaye akanikubalia ombi langu.
Siku zilivyoenda nikashangaa haniombi hela wakati ananitembelea umbali mrefu kwa nauli yake kuja kuniona.
Siku moja akanitumia ujumbe kwa Mara ya kwanza akasema-:
"Baby nina shida na shilingi 15,000/= nahitaji kwenda saluni wiki ijayo nimeona nikujulishe mapema ili ujiandae taratibu"
Kwakuwa pesa nilikuwa nayo na sio kawaida yake kuniomba nikazama mfukoni nikamtumia 50,000/= kwenye namba yake akanijibu-:
"Baby asante nimepata ila nimekuomba 15,000/= inanitosha nakurudishia 35,000/= iliyobakia ili uendelee kuizungusha kwenye biashara itusaidie wote hapo baadae"
Kabla sijamkatalia kurudisha hela ujumbe ukaingia kwenye simu yangu kuwa nimepokea 35,000/= toka kwa Nancy
Nilishikwa na mshangao aliponiambia anahamu ya kukutana na Mimi maana tokea tufahamiane sijawahi kumhitaji faragha kwa hiyo 10,000/= inamtosha saluni na 5,000/= atatumia kwa nauli ya kuja kwangu na kurudi kwao.
Wakati najiandaa kumpa ratiba ya mtoko ghafla nikatoka kwenye ndoto hii ya ajabu.
Wakuu ndoto kama hii ina maana gani.. ?
Nahamin ndoto yangu itatimia siku moja..!