The_Analyst
JF-Expert Member
- Nov 25, 2008
- 238
- 83
mmmh hii ni tamthilia gani mbona sijawahi kuiona kwenye T.V??
saa nyingine umasikini ndo unaowadhalilisha wanawake............ anakuwa mpole akijua hana pa kwenda...au hajui ataishije....au uzembe tu, kiufupi chanzo ni utegemezi
lara 1 nakuunga mkono kabisa ila ngoja nikwambie kitu kimoja hapa
mke wa ndoa alikosea sana kuachika na kurudisha majeshi. mm huwaga nasema mwiko kuondoka nitang'ang'ania hadi dk ya mwisho labda atoke yeye ila sasa nikifika mahali nimesalimu amri that will be for good ever. na hapo nitakuwa nimesha fanya hesabu ya nguvu yangu niloinvest na pia nishajua jins ya kuzirecover............MPALESTINA @work.
niliwah kuvumilia abusive life ila ambayo haikuwa na kipigo( hapa ningeuwa)..........kiasi kwamba mtu analala na hawara ndani kwangu, mm nimelala na watoto chumban kwao, asbh nawaandalia breakfast nikiwa niko poa tu na mezani tunakaa sote. sikufurukuta kwani nilikuwa napiga hesabu ya invested cost, na how am i going to recover them. sikutaka kuhamalaika manake ningekosa bara na pwani.
ila nikiwa kwenye mchakato taa ya yellow ikawaka kwamba sasa soon red itawaka ikabidi asalimu amri tena siku ambayo hakujua kama ingekuwa hivyo manake niliua moyo kabisa nikawapikia tukala meza moja, kumbe mpalestina mie nawaza returns zangu. alishindwa kujua zile guts napata wapi na hakuna ajuaye ilibidi arudi magotini kwangu...na hawara kutimuliwa. anyway it wasn't simple manake kuna mahali nafsi iliuma hadi unataka kulia lkn unajikaza kisabuni asivimbe kichwa.
Lakini na huyo mama wa ndoa nae je ni kweli amepiga ukimya tu hampi huyo hawara za chinichini? Kama ni kimya basi hawara mgonjwa wa akili unagombanaje na mtu asiyekujibu kwa masaa kadhaa?!
Lakini jamani hebu twende mbele na kurudi nyuma, hjuyo mwanaume inaelekea ni dictator flani. Kuishi na mwanamke ambaye sie tunamwita hawara kwa miaka saba hapa tunakosea huyu tunayemwita hawara ni MKEWE kwa mujibu wa sheria za nchi. Na inawezekana mume huyo amelazimisha mke wa zamani kuja na kufikia hapo na inawezekana kabisa kuwa mke wa sasa hakuwa tayari so ameresort kwenye ugomvi na tafrani kumfikishia ujumbe huyo mumewe ile ya .........si unalazimisha nakwambia hatokaa hapa huyo mkeo wa shamba!!
Kwa mantiki hii hawara (ambaye ni mke halali wa jamaa kwa sasa) anayo haki ya kufanya anachokifanya kwa huyo mke wa zamani! Yeye ndio mwenye nyumba hiyo si ndio??
gfsonwin kama sikosei sheria inasema ukiishi na mtu kama mke na mume under one roof kwa muda wa miezi sita tayari ninyi ni wanandoa hasa kama kuna majirani wanaowezakushuhudia maisha yenu. Kwa hiyo huyo mke wa pili whether anavunja vyombo vyake au vya mumewe anayo haki kuexpress hacra zake, na hatuna uhakika mlengwa ni nani hapa mume au mke wa mume.AshaDii, Badii tabia na MwanajamiiOne jamani hebu tuwazeni hivi kisheria hivi ili mtu athibitike kuwa mke kisheria kama hana ndoa ila mnaishi pamoja ni baada ya muda gani??
sasa huyu ana wake 2 kwa mtazamo wangu kwamba mke wa ndoa yupo kwasababu hajamtaliki na mke wa pili ni huyu hawara ambaye ameish nae miaka 3.
swala hapa ni je huyu hawara anavunja vya nn wakati yeye naye ni mke?? angekuwa mjanja angekaa na amani na mke wmenzie halafu akirudi mume wao ndipo sasa wayajadili
Lakini jamani hebu twende mbele na kurudi nyuma, hjuyo mwanaume inaelekea ni dictator flani. Kuishi na mwanamke ambaye sie tunamwita hawara kwa miaka saba hapa tunakosea huyu tunayemwita hawara ni MKEWE kwa mujibu wa sheria za nchi. Na inawezekana mume huyo amelazimisha mke wa zamani kuja na kufikia hapo na inawezekana kabisa kuwa mke wa sasa hakuwa tayari so ameresort kwenye ugomvi na tafrani kumfikishia ujumbe huyo mumewe ile ya .........si unalazimisha nakwambia hatokaa hapa huyo mkeo wa shamba!!
Kwa mantiki hii hawara (ambaye ni mke halali wa jamaa kwa sasa) anayo haki ya kufanya anachokifanya kwa huyo mke wa zamani! Yeye ndio mwenye nyumba hiyo si ndio??
AshaDii, Badii tabia na MwanajamiiOne jamani hebu tuwazeni hivi kisheria hivi ili mtu athibitike kuwa mke kisheria kama hana ndoa ila mnaishi pamoja ni baada ya muda gani??
sasa huyu ana wake 2 kwa mtazamo wangu kwamba mke wa ndoa yupo kwasababu hajamtaliki na mke wa pili ni huyu hawara ambaye ameish nae miaka 3.
swala hapa ni je huyu hawara anavunja vya nn wakati yeye naye ni mke?? angekuwa mjanja angekaa na amani na mke wmenzie halafu akirudi mume wao ndipo sasa wayajadili
uchafu mtupu! huyo mke wa ndoa naye ni mjingajeeeeee?? kama ni ndugu yangu ningemwambia baba akampime DNA labda si damu yetu! yaani niletewe hawara ndani?? wakati huyo wa nje tu mwenye adabu zake HATHUBUTU HATA KUTAKA NIWAZE KAMA YUPO!!
wallahi kuna situations naombaga NISITIWE MAJARIBUNI NA MUUMBA WANGU, maana matokeo yake yatakuwa mabaya sana!!
wadada/wanawake wenzangu, tuwe wapole na wenye adabu kwa busara! na sio kuwa watumwa wa maisha in the name of MARRIAGE!!
MUNGU AZILINDE NDOA ZETU, awaongoze watoto wetu kwenye kufanya maamuzi ya busara, hasaaaa maamuzi mazito ya kutafuta mwenzi wa maisha, AMEN!!
Hagombani na huyo mke wa jamaa, yeye anagombana na vyombo na makabati!
Ila kwa sasa amekaa sebuleni anaangalia TV na mke wa jamaa nadhani yuko chumbani kapiga kimya, sijui anasali
Unaweza sema ni mke halali, lakini ana sifa mbaya za umalaya hapa mtaani, na baada ya jamaa kushikwa sikio na mwanaintelijensia wake ndio akaamua kumuacha na ndipo kikazuka kitimtim cha kudundana na ndio asubuhi akachapa lapa. Wiki moja baada ya hawara kuondoka mke wa ndoa kaja, na wiki mbili baadae hawara naye katia timu na ndio nashudia haya mauzauza hapa nyumbani

Sijaelewa kwa nini umem judge sana huyo mwanaume... People treat you the way you want them to treat you... Hapo wakushangaliwa na hao wanawake pia. Ni mambo mengi wanaume wanatufanyia na kutuchezea ambavyo wasinge thubutu kama tusingeruhusu. Upole, ustaarabu, na husuda ina mpaka wake. Matatizo yapo kwa wote...
Tatizo la Mke
Kwa kukubali kudharauliwa hadi kiwango hicho. Mume kamtelekeza kwa miaka mitatu na kumtuma mkoani yeye pamoja na watoto wake. Kamrudisha hapo nyumbani huku mke akijua fika kuwa kuna hawara alikuwa akiishi hapo na mbaya zaidi ni kuwa huyo hawara karuhusiwa kufikia hapo akiwa en route kuelekea Arusha. Kakubali Mumewe amchezee... But hata hivo sio rahisi kujudge maana ukute naye kaelewa maumivu ya moyo wa huyo mwanamke akijua fika vitu vya humo ndani sio vyake ni halali ya huyo dada. Tena WARNING; Huyo mwanaume anaonekana ni mshenzi ukute hata huyo mwanamke mpya sio mke bali ni mwanamke mpya ila kaja kujisafisha kwenu... (Labda kama kweli na hao watoto wameletwa hapo).
Tatizo la Hawara
Ok, ni kawaida kuwa mtu unaweza toka na mme wa mtu, BUT hivi kuna sababu yoyote ya kwenda mletea vituko mke wake na vujo tele hata kama ana hasira juu ya mahusiano yao kuvujika? Nashangaa... Hiyo confidence ya kulala humo ndani anaitoa wapi (mchawi??); kuwa unajua kuwa mke wake pia anajua wewe ndiye uliyekuwa mbadala na unarudi kulala humo ndani?
Kwa upande namuelewa... Kapoteza miaka mitatu kwa ajili ya huyo mwanaume. Wapo wote (ki mantiki kwa halali kabisa maana alitengana na wife); then kamfanyia visa na kumtoa humo ndani bila kitu chochote. Hasira zake ni halali ila tu nashangaa hiyo roho yake ya paka asiee... Duh!
Kwa mtazamo wangu naweza sema haya mambo magumu sana kuja na justification za hasa yupi anatakiwa lawama. Mwanaume ana makosa pia, ila hao wanawake nao sio watoto wadogo waangaliwe tu kuwa wao ndiyo wameonewa na hali wao ndio wamechangia kwa ukubwa hali kuwa ilivo. Kitu nakuhakikishia ni kuwa mwanaume angejua kuwa mke wake kichaa na hakubaliani na upuuzi usio kuwa na tija asinge thubutu, hata huyo hawara asinge thubutu...
Ila niongezee kuwa watu wa sampuli kama hiyo ya huyo mke hatari saana. Hulimbikiza mambo rohoni, siku aki react unakuta kama sio mume ama hawara ama wote maiti tu, na wala hajutii...
Mimi kwa kumalizia ni kuwa huyo mwanaume ndiye BARADHULI MKUBWA na aombe Mungu hao wanawake wasipatane kwani wakishaelewana maisha yake yako hatarini. BORA TUMKOMESHE (au potelea mbali tumkose wote) NI USEMI WA KUMUUA MWANAUME SIKUZOTE.
Thread hii na iwe fundisho kwetu sote.