Hivi huyu mwanaume anatumia akili au makamasi kufikiri?

Lakini na huyo mama wa ndoa nae je ni kweli amepiga ukimya tu hampi huyo hawara za chinichini? Kama ni kimya basi hawara mgonjwa wa akili unagombanaje na mtu asiyekujibu kwa masaa kadhaa?!
 
saa nyingine umasikini ndo unaowadhalilisha wanawake............ anakuwa mpole akijua hana pa kwenda...au hajui ataishije....au uzembe tu, kiufupi chanzo ni utegemezi

Uko sawa kabisa Badili... Namimi pia nahisi kwa kiasi kikubwa ni hilo, ndivo nilivyomwambia hata Gfs pia, kuwa inaweza ikawa ni dependency ama tu usukule wa mapenzi. Huu umasikini na utegemezi mbaya sana.
 
dahhhhhhhhhhhh una moyo i see...

mie nahisi kitimtim chake tungegawana majengo ya serikali..... Mungu aepushe mbali

lara 1 nakuunga mkono kabisa ila ngoja nikwambie kitu kimoja hapa

mke wa ndoa alikosea sana kuachika na kurudisha majeshi. mm huwaga nasema mwiko kuondoka nitang'ang'ania hadi dk ya mwisho labda atoke yeye ila sasa nikifika mahali nimesalimu amri that will be for good ever. na hapo nitakuwa nimesha fanya hesabu ya nguvu yangu niloinvest na pia nishajua jins ya kuzirecover............MPALESTINA @work.

niliwah kuvumilia abusive life ila ambayo haikuwa na kipigo( hapa ningeuwa)..........kiasi kwamba mtu analala na hawara ndani kwangu, mm nimelala na watoto chumban kwao, asbh nawaandalia breakfast nikiwa niko poa tu na mezani tunakaa sote. sikufurukuta kwani nilikuwa napiga hesabu ya invested cost, na how am i going to recover them. sikutaka kuhamalaika manake ningekosa bara na pwani.

ila nikiwa kwenye mchakato taa ya yellow ikawaka kwamba sasa soon red itawaka ikabidi asalimu amri tena siku ambayo hakujua kama ingekuwa hivyo manake niliua moyo kabisa nikawapikia tukala meza moja, kumbe mpalestina mie nawaza returns zangu. alishindwa kujua zile guts napata wapi na hakuna ajuaye ilibidi arudi magotini kwangu...na hawara kutimuliwa. anyway it wasn't simple manake kuna mahali nafsi iliuma hadi unataka kulia lkn unajikaza kisabuni asivimbe kichwa.
 
Lakini jamani hebu twende mbele na kurudi nyuma, hjuyo mwanaume inaelekea ni dictator flani. Kuishi na mwanamke ambaye sie tunamwita hawara kwa miaka saba hapa tunakosea huyu tunayemwita hawara ni MKEWE kwa mujibu wa sheria za nchi. Na inawezekana mume huyo amelazimisha mke wa zamani kuja na kufikia hapo na inawezekana kabisa kuwa mke wa sasa hakuwa tayari so ameresort kwenye ugomvi na tafrani kumfikishia ujumbe huyo mumewe ile ya .........si unalazimisha nakwambia hatokaa hapa huyo mkeo wa shamba!!

Kwa mantiki hii hawara (ambaye ni mke halali wa jamaa kwa sasa) anayo haki ya kufanya anachokifanya kwa huyo mke wa zamani! Yeye ndio mwenye nyumba hiyo si ndio??
 
Lakini na huyo mama wa ndoa nae je ni kweli amepiga ukimya tu hampi huyo hawara za chinichini? Kama ni kimya basi hawara mgonjwa wa akili unagombanaje na mtu asiyekujibu kwa masaa kadhaa?!

Hagombani na huyo mke wa jamaa, yeye anagombana na vyombo na makabati!
Ila kwa sasa amekaa sebuleni anaangalia TV na mke wa jamaa nadhani yuko chumbani kapiga kimya, sijui anasali
 
Ya Tegereza umeleta mjadala hapa ambao kwa mtazamo wa karibu unaonekana ni kama mchezo wa kuigiza vile, lakini ki uhakika hili suala ni verry sensitive. Nawashukuru wana jamvi kama Asha dii na gfsonwin walivyoweza kulieleza kwa mtazamo wao. Ki ukweli, kwanza mwanamume ana matatizo makubwa sana, aidha ya bahati mbaya au ya makusudi.
Nasimamia kuwa niya makusudi kutokana na sababu zifuatazo; Huyu anayehasabika kama mkewe halali yawezekana hatakiwi tena na huyu bwana, sasa ili kumfanya huyu mwanamke ainue mikono yeye mwenyewe ni kumpambanisha na huyo hawala.
Kwa kufanya hivyo mwanamke ataona kama vile amedhalilishwa na kuamua kuondoka kimoja bila kuhitaji mjadala kitu ambacho kitakuwa kimewapa ushindi wa mezani mwanamke na mwanamume.
Kwa upande wa huyo hawala, yeye anacheza ngoma anayoifahamu na akijua vema mpiga tumba ni nani? Haiwezekani kama hujatiwa kiburi na muhusika ukawa na ujasiri kiasi hicho, na kama alikuwa on transit ni kipi kimemweka hadi sasa? Kwa hiyo issue nzima ni kutaka kumuondoa huyo mwanamke kwa kutumia lugha ya akufukuzaye hakwambii toka>>> Tafakalini.
 
AshaDii, Badii tabia na MwanajamiiOne jamani hebu tuwazeni hivi kisheria hivi ili mtu athibitike kuwa mke kisheria kama hana ndoa ila mnaishi pamoja ni baada ya muda gani??
sasa huyu ana wake 2 kwa mtazamo wangu kwamba mke wa ndoa yupo kwasababu hajamtaliki na mke wa pili ni huyu hawara ambaye ameish nae miaka 3.

swala hapa ni je huyu hawara anavunja vya nn wakati yeye naye ni mke?? angekuwa mjanja angekaa na amani na mke wmenzie halafu akirudi mume wao ndipo sasa wayajadili
 
Last edited by a moderator:
uchafu mtupu! huyo mke wa ndoa naye ni mjingajeeeeee?? kama ni ndugu yangu ningemwambia baba akampime DNA labda si damu yetu! yaani niletewe hawara ndani?? wakati huyo wa nje tu mwenye adabu zake HATHUBUTU HATA KUTAKA NIWAZE KAMA YUPO!!

wallahi kuna situations naombaga NISITIWE MAJARIBUNI NA MUUMBA WANGU, maana matokeo yake yatakuwa mabaya sana!!
wadada/wanawake wenzangu, tuwe wapole na wenye adabu kwa busara! na sio kuwa watumwa wa maisha in the name of MARRIAGE!!

MUNGU AZILINDE NDOA ZETU, awaongoze watoto wetu kwenye kufanya maamuzi ya busara, hasaaaa maamuzi mazito ya kutafuta mwenzi wa maisha, AMEN!!
 
hee,hivi kuna maisha ya aina hii jamani?wanawake kwa nini tunakuwa weak kiasi hicho?mwanaume ahangaike wee,akikuita unarudi.kwa hali hiyo kweli huyo mwanaume atatulia?na huyo mke si ataishi kwa maisha yasiyo na furaha?namsikitikia kwa kweli.na huyo mume ameishaijua weakness ya mke atam treat anavyotaka yeye.heka heka wako wap?wa kushikishwa adabu ni huyo mwanamme
 
Lakini jamani hebu twende mbele na kurudi nyuma, hjuyo mwanaume inaelekea ni dictator flani. Kuishi na mwanamke ambaye sie tunamwita hawara kwa miaka saba hapa tunakosea huyu tunayemwita hawara ni MKEWE kwa mujibu wa sheria za nchi. Na inawezekana mume huyo amelazimisha mke wa zamani kuja na kufikia hapo na inawezekana kabisa kuwa mke wa sasa hakuwa tayari so ameresort kwenye ugomvi na tafrani kumfikishia ujumbe huyo mumewe ile ya .........si unalazimisha nakwambia hatokaa hapa huyo mkeo wa shamba!!

Kwa mantiki hii hawara (ambaye ni mke halali wa jamaa kwa sasa) anayo haki ya kufanya anachokifanya kwa huyo mke wa zamani! Yeye ndio mwenye nyumba hiyo si ndio??

Unaweza sema ni mke halali, lakini ana sifa mbaya za umalaya hapa mtaani, na baada ya jamaa kushikwa sikio na mwanaintelijensia wake ndio akaamua kumuacha na ndipo kikazuka kitimtim cha kudundana na ndio asubuhi akachapa lapa. Wiki moja baada ya hawara kuondoka mke wa ndoa kaja, na wiki mbili baadae hawara naye katia timu na ndio nashudia haya mauzauza hapa nyumbani
 
AshaDii, Badii tabia na MwanajamiiOne jamani hebu tuwazeni hivi kisheria hivi ili mtu athibitike kuwa mke kisheria kama hana ndoa ila mnaishi pamoja ni baada ya muda gani??
sasa huyu ana wake 2 kwa mtazamo wangu kwamba mke wa ndoa yupo kwasababu hajamtaliki na mke wa pili ni huyu hawara ambaye ameish nae miaka 3.

swala hapa ni je huyu hawara anavunja vya nn wakati yeye naye ni mke?? angekuwa mjanja angekaa na amani na mke wmenzie halafu akirudi mume wao ndipo sasa wayajadili
gfsonwin kama sikosei sheria inasema ukiishi na mtu kama mke na mume under one roof kwa muda wa miezi sita tayari ninyi ni wanandoa hasa kama kuna majirani wanaowezakushuhudia maisha yenu. Kwa hiyo huyo mke wa pili whether anavunja vyombo vyake au vya mumewe anayo haki kuexpress hacra zake, na hatuna uhakika mlengwa ni nani hapa mume au mke wa mume.
 
Last edited by a moderator:
Lakini jamani hebu twende mbele na kurudi nyuma, hjuyo mwanaume inaelekea ni dictator flani. Kuishi na mwanamke ambaye sie tunamwita hawara kwa miaka saba hapa tunakosea huyu tunayemwita hawara ni MKEWE kwa mujibu wa sheria za nchi. Na inawezekana mume huyo amelazimisha mke wa zamani kuja na kufikia hapo na inawezekana kabisa kuwa mke wa sasa hakuwa tayari so ameresort kwenye ugomvi na tafrani kumfikishia ujumbe huyo mumewe ile ya .........si unalazimisha nakwambia hatokaa hapa huyo mkeo wa shamba!!

Kwa mantiki hii hawara (ambaye ni mke halali wa jamaa kwa sasa) anayo haki ya kufanya anachokifanya kwa huyo mke wa zamani! Yeye ndio mwenye nyumba hiyo si ndio??

Kuna kitu tunasahau hapa... Kuna kile kitu ya Herbert Spencer ya 'Survival of the Fittest'. Nani mshindi na nani atabaki na hiyo prize. Inaweza ikawa wapo so blinded kwa kumtaka huyo mwanaume kiasi kwamba hawaoni kuwa haijalishi awe na nini kati yao hakuna anae mheshimu kama mke stahili na hivyo wala sio ajabu kwa yeyote atakae baki kuchemka vile vile... pamoja na imani kuwa hayo mengine ni matoke.

Nakubaliana na wewe kuwa huyo sio hawara aisee.. Huyo ni mke pia kisheria. Hivo kama nilivyogusia katika post yangu ya kwanza kuwa hizo hasira zake ni za msingi huyo mke mdogo na ana haki pia, ingawa haki yake hiyo anaitumia kijinga (lkn bado narudi nyuma kuwa mapenzi upovu, utafakari hupaa na hauna mahala pake penye mapenzi ama mauvivu ya mapenzi)... Na haki yake hio bado haimpi sababu ya kumfanyie fujo mwenzie.

Hao kumuweza huyo mwanaume inatakiwa waungane... Mume akirudi home akute wamepatana na wameamua kuishi kama mke mkubwa na mdogo na kuweka taratibu za kumbana vilivyo! Ni njea pekee huyo mwanaume atakomoka kuliko yoyote ile wataamua.
 
AshaDii, Badii tabia na MwanajamiiOne jamani hebu tuwazeni hivi kisheria hivi ili mtu athibitike kuwa mke kisheria kama hana ndoa ila mnaishi pamoja ni baada ya muda gani??
sasa huyu ana wake 2 kwa mtazamo wangu kwamba mke wa ndoa yupo kwasababu hajamtaliki na mke wa pili ni huyu hawara ambaye ameish nae miaka 3.

swala hapa ni je huyu hawara anavunja vya nn wakati yeye naye ni mke?? angekuwa mjanja angekaa na amani na mke wmenzie halafu akirudi mume wao ndipo sasa wayajadili

Samahani gfsonwin nimerekebisha hapo, ameishi na hawara miaka 7, kwa mujibu wa mke wangu, ambaye ndiye anayenipa dondoo za kinachojiri nyumba ya pili...

Msishangae tuna share fence moja na tunatumia geti moja lakini nyumba tofauti.
 
uchafu mtupu! huyo mke wa ndoa naye ni mjingajeeeeee?? kama ni ndugu yangu ningemwambia baba akampime DNA labda si damu yetu! yaani niletewe hawara ndani?? wakati huyo wa nje tu mwenye adabu zake HATHUBUTU HATA KUTAKA NIWAZE KAMA YUPO!!

wallahi kuna situations naombaga NISITIWE MAJARIBUNI NA MUUMBA WANGU, maana matokeo yake yatakuwa mabaya sana!!
wadada/wanawake wenzangu, tuwe wapole na wenye adabu kwa busara! na sio kuwa watumwa wa maisha in the name of MARRIAGE!!

MUNGU AZILINDE NDOA ZETU, awaongoze watoto wetu kwenye kufanya maamuzi ya busara, hasaaaa maamuzi mazito ya kutafuta mwenzi wa maisha, AMEN!!

mwali nakuelewa. asante sana kwa maombi haya.
 
Unaweza sema ni mke halali, lakini ana sifa mbaya za umalaya hapa mtaani, na baada ya jamaa kushikwa sikio na mwanaintelijensia wake ndio akaamua kumuacha na ndipo kikazuka kitimtim cha kudundana na ndio asubuhi akachapa lapa. Wiki moja baada ya hawara kuondoka mke wa ndoa kaja, na wiki mbili baadae hawara naye katia timu na ndio nashudia haya mauzauza hapa nyumbani
Unaweza sema ni mke halali, lakini ana sifa mbaya za umalaya hapa mtaani, na baada ya jamaa kushikwa sikio na mwanaintelijensia wake ndio akaamua kumuacha na ndipo kikazuka kitimtim cha kudundana na ndio asubuhi akachapa lapa. Wiki moja baada ya hawara kuondoka mke wa ndoa kaja, na wiki mbili baadae hawara naye katia timu na ndio nashudia haya mauzauza hapa nyumbani

Bado haiondoi hadhi yake kama mke halali kwa mujibu wa sheria unless kama alipodundwa alikabidhiwa na talaka yake otherwise mume huyo anao wake wawili mpaka sasa. Kuishi na mwanamke miaka 7 kama mke ni mkewe halali. Hayo ya kutokuwa mwaminifu, sijui kicheche hayaondoi title ya mke au mume ndoani unless talaka imehusika.

Kwa taarifa hii ninaanza kupata picha mpya kabisa ya tukio hili. Inawezekana sasa mume amelitambua kosa lake la kumtelekeza mke mkubwa sasa ametaka kumrudisha lakini akajisahau kuwa ALIOA mke wa pili (hata kama hakufunga nae ndoa) so mke wa pili nae anayo haki ya kumclaim yeye kama mumewe. Ila swali ni kwamba alikuwa akiwaza nini kuwaweka mahali pamoja?

Na huyo mama wa ndoa mwambie aache ujinga anasafisha nyumba ya nini aache mumewe aje ashuhudie ukuchaa wa bi mdogo wake, ye anatupa vidhibit?
 
Sijaelewa kwa nini umem judge sana huyo mwanaume... People treat you the way you want them to treat you... Hapo wakushangaliwa na hao wanawake pia. Ni mambo mengi wanaume wanatufanyia na kutuchezea ambavyo wasinge thubutu kama tusingeruhusu. Upole, ustaarabu, na husuda ina mpaka wake. Matatizo yapo kwa wote...

Tatizo la Mke

Kwa kukubali kudharauliwa hadi kiwango hicho. Mume kamtelekeza kwa miaka mitatu na kumtuma mkoani yeye pamoja na watoto wake. Kamrudisha hapo nyumbani huku mke akijua fika kuwa kuna hawara alikuwa akiishi hapo na mbaya zaidi ni kuwa huyo hawara karuhusiwa kufikia hapo akiwa en route kuelekea Arusha. Kakubali Mumewe amchezee... But hata hivo sio rahisi kujudge maana ukute naye kaelewa maumivu ya moyo wa huyo mwanamke akijua fika vitu vya humo ndani sio vyake ni halali ya huyo dada. Tena WARNING; Huyo mwanaume anaonekana ni mshenzi ukute hata huyo mwanamke mpya sio mke bali ni mwanamke mpya ila kaja kujisafisha kwenu... (Labda kama kweli na hao watoto wameletwa hapo).

Tatizo la Hawara

Ok, ni kawaida kuwa mtu unaweza toka na mme wa mtu, BUT hivi kuna sababu yoyote ya kwenda mletea vituko mke wake na vujo tele hata kama ana hasira juu ya mahusiano yao kuvujika? Nashangaa... Hiyo confidence ya kulala humo ndani anaitoa wapi (mchawi??); kuwa unajua kuwa mke wake pia anajua wewe ndiye uliyekuwa mbadala na unarudi kulala humo ndani?

Kwa upande namuelewa... Kapoteza miaka mitatu kwa ajili ya huyo mwanaume. Wapo wote (ki mantiki kwa halali kabisa maana alitengana na wife); then kamfanyia visa na kumtoa humo ndani bila kitu chochote. Hasira zake ni halali ila tu nashangaa hiyo roho yake ya paka asiee... Duh!

Kwa mtazamo wangu naweza sema haya mambo magumu sana kuja na justification za hasa yupi anatakiwa lawama. Mwanaume ana makosa pia, ila hao wanawake nao sio watoto wadogo waangaliwe tu kuwa wao ndiyo wameonewa na hali wao ndio wamechangia kwa ukubwa hali kuwa ilivo. Kitu nakuhakikishia ni kuwa mwanaume angejua kuwa mke wake kichaa na hakubaliani na upuuzi usio kuwa na tija asinge thubutu, hata huyo hawara asinge thubutu...

Ila niongezee kuwa watu wa sampuli kama hiyo ya huyo mke hatari saana. Hulimbikiza mambo rohoni, siku aki react unakuta kama sio mume ama hawara ama wote maiti tu, na wala hajutii...

Napingana nawe AshaDii kwa kuwa hao wanawake wote hawana makosa.

Kwanini?
Kuhusu Mke wa Ndoa;

Kwa kuwa huyo mke halali wa huyo jirani wa anajua mumewe alikuwa salama kwa maana kuwa hakuwa na hawara na alikuwa anatafuta kipato kwa ajili ya familia yake. Huwezi kujua labda huyo mume alikuwa anatuma matumizi kwa familia yake na vilevile huenda alikuwa anakwenda kutekeleza wajibu wake kama mwanandoa. Aidha huenda alikuwa anapiga simu au kwa ujumla alikuwa na mawasiliano na familia yake. Hence wife is 100% INNOCENT.

Kuhusu Hawara;

Kwa kuwa huyo hawara ameishi kwenye mazingira hayo labda kwa kutokujua kuwa huyo 'mume' wake hana mke mwingine, na kwakuwa hajawahi kupata bugudha kutoka kokote hasa kwa kuwa huyo 'mumewe'; ni dhahiri kuwa huyo hawara alijijua ndio mama mwenye nyumba. Ama kwa ligha ingine alishawekeza moyo wake kwa huyo bwana na akadhani yuko ndoani hata kama siyo ya kidini au ya kiserikali basi baada ya six months alijikuta ni wife automatically.
Hapo ndipo ninamundoa makosani naye ni 100% INNOCENT (otherwise kama alikuwa anajua/ameambiwa na huyo hawara kuwa ana mke atakuwa makosani.)

Kuhusu Huyo Mume;

Huyo ndiye chanzo cha matatizo yote kwani alipaswa kuwa na msimamo kuhusu mpangilio wa maisha yake kimapenzi. Kwanza kosa lilikoanzia ni pale alipoanza kuwa na mahusiano nje ya ndoa yake ambapo alishindwa kuzuia tamaa,
Kosa lilianza kuota meno pale alipomkaribisha huyo hawara ndani kwake huku akijua fika kuwa ni mwanandoa/mwanafamilia..... Akaendelea kupalilia kosa/dhambi ile kwa kutomleta mkewe halali hata kwa muda mfupi na mbaya zaidi kafikia alikokofikia yaani kuanzisha visa/kumsingizia kwa yule hawara kwa kuwa mkewe anakuja jambo lililopelekea kumfukuza hawara.
Na kwakuwa jamaa ni dhaifu, kwanza alijianzishia safari hasahasa baada ya kujua kuwa yule hawara anakuja, hapa inawezekana alimpigia simu au ujumbe kuwa lazima anakuja na ndio kisa cha kumwambia Tegelezeni kuwa amtaarifu wife kuwa hawara anakuja na apewe huduma na eti asiruhusiwe tu kuondoka na chochote.
Mimi kwa kumalizia ni kuwa huyo mwanaume ndiye BARADHULI MKUBWA na aombe Mungu hao wanawake wasipatane kwani wakishaelewana maisha yake yako hatarini. BORA TUMKOMESHE (au potelea mbali tumkose wote) NI USEMI WA KUMUUA MWANAUME SIKUZOTE.
Thread hii na iwe fundisho kwetu sote.
 
Arushaone inapendeza kuwa umelitazama kwa mtazamo huo... Inatia moyo kuwa kuna baadhi ya wanaume wanawashawishi wanaume zao ku treat wanawake zao vizuri. Ingawa tumetofautiana kim mtazamo kwa mimi kuona wanawake wanalaumiwa pia; na wewe kuona mwanaume ndiye apewe lawama zote - nafurahi kuwa walau twakubaliana kuwa dawa yake ni hao wanawake waungane kutafuta suluhu...
 
Back
Top Bottom