Hivi hizi Kinga za Makosa ya kijinai zina Faida gani Kwa Taifa?

Mzee Ngonyani

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
821
1,876
Moja ya vitu vinavyonishangaza katika nchi yangu mama Tanzania, ni ubunifu walionao viongozi wa serikali katika Kuhakikisha yale yanayo wahusu yanafanikiwa, au yanafanyika kadili wao wanavyopenda tena kupitia chombo muhimu kama bunge.

Sijawasikia wakipeleka muswada wa kufanyia marekebisho Sheria ya kuwabana viongozi wezi na mafisadi. Au wabadhirifu wa mali ya umma au kupunguza malupulupu yao Kwa sababu labda kutokana na matatizo ya kiuchumi mapato ya serikali yamepungua.

Mapato ya serikali yakipungua wanakimbilia kuongeza Kodi na tozo, wao wanaendelea na maisha yao yaleyale magari ya kifahari posho za kutosha. Wanao umia ni wananchi wakawaida ambao ni wakulima na watumishi wenye vipato vidogo kama vile walimu na manesi.

Sasa hilo wameona halitoshi wamekuja na sheria yenye lengo la kuwalinda wakifanya jinai, walianza na spika na naibu wake, waka waongeza na majaji leo wamekuja na Maafisa wa idara ya Usalama Taifa.

Tusishangae wakaja na sheria nyingine ya kuwapa kinga watendaji. Mimi Mzee Ngonyani ndugu yake na Komba jirani yake na Mapunda nauliza hizo Kinga mnazotafuta ni za nini mnataka kuwafanyia nini Watanzania?
 
Shida Tz wengi mnanguvu nyuma ya keyboard zenu hapo ukiambiwa ingia barabaran kudai hiyo haki yako unajifungia ndani...
 
Shida Tz wengi mnanguvu nyuma ya keyboard zenu hapo ukiambiwa ingia barabaran kudai hiyo haki yako unajifungia ndani...
Swala sio kuwa na ugomvi na serikali, Hapa tunaishauri serikali ideal na maswala ya msingi yanayo wahusu watu wengi kuliko kuwaangalia maslahi ya watu wachache ambao ni viongozi Fulani. Hakuna haja ya kuwapa kinga kwasababu baadhi yao wanaweza wakatumia vibaya madaraka yao harafu tukashindwa kuwawajibisha kisheria.
 
Back
Top Bottom